Historia ya kusisimua ya Padre Livinus:Papa amesema Ndiyo haraka
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Kuna historia nyingi katika Maisha ambazo hazina mambo mengi ya kuelezea kutokana na uwepo wa nguvu yake ya kina ambayo inajionesha wazi. Ni hiistoria ambazo imani na matumaini vinakutana, vinasukana katika shauku kubwa ambayo baadaye inakuwa huduma. Huo ni mkutano wa kina na nguvu yake! Ni historia ya kijana mtawa Livinus Esomchi Nnamani, aliyepewa daraja la ukuhani siku ya Alhamisi Kuu iliyopita. Hii ni simulizi ya mtu ambaye kwa hakika alijibu wito wake na baadaye akagundua kuwa ana ugonjwa mbaya sana na kuomba kuwa mchakato wake wa imani uweze kuwekwa taji hata kabla ya kumaliza mchakato mzima wa majiundo yake ya kufikia ukasisi. Alituma ombi lake ambalo lilipata jibu la NDIYO kubwa na kwa haraka iwezekanavyo!
Ndani ya masaa 24
Kwa sasa ni Padre Livinus, baada ya kupokea draja hilo kwa haraka, ambaye alifika nchini Italia kutoka Nigeria mnamo 2019. Aliendelea kupambana kwa nguvu zake zote ili kuweza kushinda ugonjwa mbaya lakini wakati huo huo akiendelea na mafunzo yake. Kwa bahati mbaya kutokana na mabadiliko ya hali yake ya kiafya kuendelea kudhoofika siku hadi siku kutokana na ugonjwa huu mbaye, umempelekea hatua ya kuomba ruhusa kwa Baba Mtakatifu ili atimize ile shauku na ndoto ya wito wake hasa wa kuwa Kuhani hata milele kama wa Melkizedeki. Kwa kufanya hivyo ilimbidi aandika barua kwa mkono wake ambapo alindika barua ya maombi kwa Baba Mtakatifu Francisko, siku ya Jumatano ya Juma Kuu Takatifu, tarehe 31 Machi 2021. Aliandika barua hiyo akiwa katika jengo ambalo amelazwa la Kiafya liitwalo “Medica Group Casilino”, jijini Roma kutokana na ugonjwa wake wa saratani ya damu. Labda kijna huyo mtawa hakuwa anafikiria kwamba ndani ya masaa 24 tu, shauku yake ingeweza kutulizwa na kuwa halisi!
Upendo wa Baba:Shauku, maombi, jibu la kutoka kwa Baba Mtakatifu.
Upendo wa Baba kwa ajili ya mwanaye ambaye anakuwa mhudumu wake kwa maana ya shauku yake na maombi yake, yalipata majibu ya haraka kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko. Katika historia hii ya kusisimua, amesimulia kwa njia ya mahojiano na Radio Vatican, Askofu, Msaidizi Daniele Libanori wa Jimbo la Roma kwamba, alimtambua kijana huyo mtawa, alivyo mgonja na aliyelazwa hospitalini Roma. Na ili kutimiza shauku yake ya wito huo wa kuwa kuhani, kulihitajilakini ruhusa maalum. Kwa maana hiyo alimshauri Mkuu wake kuwa yeye ndiye alipazwa kumwombea ruhusa ambayo baadaye Askofu angeweza kufanya imfikie Papa. Askofu Daniele Libanori akiendelea, amesimulia kuwa baada ya saa moja au kupita kidogo kabla ya masa mawili, Papa Francisko alimpatia ruhusa ili aweze kupewa daraja hilo. Yote hayo yalitokea tarehe 31 Machi 2021, asubuhi Jumatano Kuu, kwa maana hiyo kabla ya kutimia masaa mawili baada ya Papa kupokea barua ya huyo mtawa.
Liturujia ya daraja la ukuhani
Siku moja baadaye, yaani Alhamisi Kuu, asubuhi, Askofu Msaidizi Libanori alikuwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya maadhimisho na Papa Francisko katika Misa ya Krisma (kubariki mafuta). Wakati alikuwa akivaa, mtu mmoja alikuja kumwita na kusema kuwa Papa alikuwa anataka kumwona. “Nilikwenda Sakrestia na hapo alinipatia hati ambayo ndani mwake kulikuwa na ruhusa ya kupatiwa daraja la ukuhani Livinus”. Siku ya Alhamisi Kuu, ilikuwa sasa siku ambayo haitasahulika kwa kijana mtawa Livinus kutoka Nigeria. “Alhamisi mchana huo huo, katika Jengo la kiafya, tuliadhimisha Liturujia ya Daraja ya Upadre, Livinus alifurahi sana na hisia kubwa, japokuwa alikuwa amejaribiwa sana na mateso ya afya yake na udhaifu. Tuliadhimisha Misa kwa heshima, tukijaribu kutomchosha sana. Alifurahia hilo. Nadhani ilikuwa wakati wake wa kina ndani ya moyo wake”. Wakati wa liturujia, Askofu alimpaka mafuta kuhani huyo ya Krisma ambayo yalibarikiwa na Papa asubuhi hiyo hiyo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Asili ya ukuhani
Kwa mujibu wa Askofu Libanori akielezea juu asili ya ukuhani amesema kwamba: “walio wengi wanachukulia ukuhani kama leseni ya uwezo wa kuadhimisha Sakramenti katika huduma ya watu wa Mugu. Ndiyo hii bila shaka ni muhimu, lakini kuhani awali ya yote ni mtu ambaye anafananishwa na Kristo, yaani Kristo mwingine”. Maneno ambayo Askofu alipendelea kusema kwa kuhani mpya ni haya: “Nilimwambia Livinus kwamba anaishi ukuhani wake pia katika kujitoa kwake mwenyewe, katika ugonjwa unaomwelemea, labda hata kumdhalilisha na kumnyenyekesha, hakika hunamzuia kuishi huduma yake kama wengine wengi. Lakini Misa pekee ya kweli na Misa kubwa ambayo kila Mkristo huadhimisha ni ile ambayo anajitoa mwenyewe binafsi kwa kuishi maisha yake ya kila siku hadi wakati Mungu atakapotaka kifo chake katika muungano na Kristo. Kwa maana hiyo ukuhani wa Livinus haujashushwa kwa hali yake, badala yake umeinuliwa kwa sababu ni dhahiri zaidi kwamba kuhani ni nani”.
Ukaribu wa madaktari na wauguzi
Kuwekwa wakfu kwa huyo kijana mtawa, uliandaliwa katika wadi ya Jumuiya ya Kifya ya Casilino Roma, ambapo kuhani mpya amelazwa hospitalini akiendelea na matibabu ya saratani ya damu. Waamini ambao Padre Lavinus amewapa baraka yake ya kwanza walikuwa madaktari na wauguzi ambao wanamtunza kwa upendo mkuu. Pia waliokuwepo karibu naye watawa wa Jumuiya yake ya Campitelli na Mtakatifu Giovanni Leonardi huko Torre Maura Italia. Historia ya Padre mpya Livinus inakumbusha ile ya kijana mwingine mtawa Salvatore Mellone, aliyestaajabisha Italia mnamo 2015. Yeye naye alikuwa ni mwathiriwa wa saraani aliye wekwa wakfu wa kuhani katika Jimbo kuu la Trani-Barletta-Bisceglie miaka miwili mapema kabla ya kumaliza mchakato wa majiundo yake. Papa Francisko alimwita na kumambuia kuwa “Baraka ya kwanza utakayotoa kama kuhani unibariki mimi”. Ni ahadi aliyoweka kuhani mpya, ambaye aliendelea kuadhimisha Ekaristi kila siku kwa miezi miwili hadi aliporudi Nyumbani kwa Baba Mungu.