Nigeria:Ask.Kaigama:Nchi inahitaji wahubiri wema kama Mchungaji Yesu
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.
Askofu Mkuu Ignatius Kaigama, wa Jimbo Kuu katoliki la Abuja nchini Nigeria, wakati wa mahubiri yake katika Misa ya Jumapili tarehe 25 Aprili 2021, sambamba na Siku ya Kuombea Miito ulimwenguni, akiwa katika Parokia ya Roho Mtakatifu ya Saburi, amesema kwamba yanahitaji Maandalizi mema lakini hata kuwa na dhamiri safi kwa ajili ya dini nyingine, wachungaji wenye uwezo wa kufanya mazungumzo na Jumuiya nyingine za dini. Haya ni mambo muhimu ya kuwa kiongozi wa dini hasa katika Nchi yenye dini nyingi sana na inayokatishwa na mivutano ya kijumuiya kama Nigeria. Kardinali amesema “Mhubiri nchini Nigeria lazima ajue juu ya masuala ya dini na awe na uwezo wa kutazama mambo ya dini, kuyapima bila kuonesha chuki za kiwendawazimu na hisia za chuki.
Kwa hakika sio ufasaha wa kutosha wa kuwa na uwezo wa kuvutia umma wakati wa kuhubiri ili usadikike unachohubiri, walakini ni ujumbe wake ambao unaotakiwa kuheshimu na kuhamasisha upendo, amani na ubinadamu wetu wa pamoja,ameonya. Askofu Mkuu Kaigama katika siku hiyo ya Mchungaji Mwema alielekeza, hata mfano mwingine wa kuigwa wa Yesu Mchungaji Mwema wa kweli ambaye alitunza zizi lake. “Mhubiri mwema, lazima ahuburi ujumbe wa matumaini na wokovu bila kushawishi zizi lake kuingia katika vurugu, mivutano, au kuwatazama vibaya wafuasi wa dini nyingine. Hii inawahusu wote hasa wenye kuwa na uwajibikaji wa kuongoza jumuia yoyote, kuanzia wazazi, walimu, wakuu wa kazi, mawaziri wakuu wa vijiji na viongozi wa kidini”.
Kwa bahati mbaya, Askofu Mkuu wa Abuja ameongeza kwa kuonya kuwa viongozi wengi wa Afrika badala ya kujitoa sadaka kwa ajili ya zizi lao, wanapendelea wafuasi wao ndiyo wafe kwa ajili yao. Hata Kanisa leo hii limejaa wanaojiita wachungaji, lakini ambao hupima mafanikio yao kwa suala la ununuzi wa vifaa, wakionesha hadhi na sifa yao badala ya kufikiria juu ya wokovu wa roho. Baadhi ya viongozi wa dini wanataka wawe ndiyo kitovu cha tahadhari na umakini, wakikuza aina fulani ya ibada ya kuabudiwa au ibada ya sifa yake tu”, askofu Mkuu amebainisha.
Kinyume chake, Askofu Mkuu emesisitiza, mfano wa Mchungaji Mwema hufundisha viongozi wasitafute kutawala kwa mabavu, wasipande ugomvi, wasijinufaishwe kwa faida ya madhara jumuiya waliyokabidhiwa. Ili kuwa mhubiri mzuri, hata hivyo, lazima mtu awe na mafunzo ya kutosha kwa sababu kutokuwa tayari kunaweza kusababisha kueneza ukweli wa imani ya kijujuu na potofu uliokusudiwa kusababisha kutokuelewana na mivutano ya kidini. Kwa mfano, kama vile daktari ili aweze kufikia maarifa kamili ya kitaalam lazima ajifunze kwa ufasaha kabla ya kuweza kutekeleza taaluma hiyo, na ndivyo hivyo wahubiri lazima wakamilishe mafunzo yao ya kidini vema kabla ya kuweza kuhubiri, kwa sababu amesema “ignorantia legis non excusat”. yaani ,“kutokujua sheria hakuwezi kutumiwa kama kisingizio”, amesisitiza.
Askofu Mkuu Kaigama ameeleza kwa mfano njia ya malezi ya wanaopenda kujiunga na mchakato wa ukuhani ambao unahitaji karibu miaka tisa ya masomo kama vile falsafa, taalimungu, lakini pia dini nyingine. “Nchini Nigeria, hasa, utafiti wa Uislamu ni wa lazima katika seminari zote. Askofu amebainisha kwamba hii kusimika mizizi ya imani yao, lakini pia kupanua upeo wao wa kiakili na kijamii ili waweze kuhubiri na kufundisha dini wakati wanaheshimu maoni ya dini za wengine. Kwa njia hiyo katika hitimisha lake ni mwaliko kwa viongozi wote wa dini nchini humo ili kufuata sauti ya Mchungaji Mwema Yesu. Kwa makuhani, hasa, Askofu Mkuu Kaigama amekumbusha kama Baba Mtakatifu Francisko kwamba wachungaji wema lazima wawe na arufu ya kondoo.