Mshuhudieni Yesu Mfufuka: Kwa Ekaristi, Neno, Sala na Matendo!
Na Padre Nikas Kiuko, - Mwanza
UTANGULIZI: Karibuni katika adhimisho la Misa Takatifu leo dominika ya tatu ya pasaka mwaka B wa Kanisa. Jumapili hii tunaalikwa kumshuhudia Kristo mfufuka katika maisha yetu. Kumshuhudia Kristo katika familia zetu, sehemu zetu za kazi, na sehemu zetu za biashara. Mwaliko huo tunaupata katika kitabu cha matendo ya mitume sura ya tatu. Mitume Petro na Yohane wanavyo mshuhudia Kristo mfufuka kwa Waisraeli, Katika hotuba hiyo ya Petro ana anza na kuwataja walio mshuhudia Mungu katika maisha yao. Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Kwanini aanze na watu hao? Tutasikia kwenye maandiko matakatifu. Katika Injili wafuasi wanamshuhudia Kristo mfufuka kwa Mitume kwamba walimtambua katika kuumega mkate. Yohane katika waraka wake wa kwanza kwa watu wote anasema kuwa kumshuhudia Kristo kumejikita katika kuepuka dhambi na kuwa watu wa watoba.
TAFAKARI: Karibuni katika tafakari ya Neno la Mungu. Leo tunaalikwa kumshuhudia Kristo katika maisha yetu, katika familia zetu, katika sehemu zetu za kazi na katika maeneo yetu ya biashara za kila siku. Mwaliko huu tunaupata kwanza katika somo la kwanza. Katika somo la kwanza hotuba ya Petro ameanza na kusema Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa Baba zenu katika kusanyiko la Wayahudi kuwa ndiye alimfufua bwana wetu Yesu Kristo. Ushuhuda huo wa Petro aliutoa baada ya kumfanya kiwete aliyekuwa ombaomba, tegemezi kutembea na kuanza kujitegemea na kujitafutia riziki yake mwenyewe. Petro aliwambia Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ndiye aliye mfufua Kristo. Kwa nini ameanza na kuwataja wazee hawa watatu? Njia ya kuwakumbusha mahusiano kati yao Wayahudi na Mungu ulianzia kwa hao wazee. Uhusiano kati ya Wayahudi na Ibrahimu ni mkubwa, Ibrahimu ndiye aliyeweka agano na Mungu.
Mungu wa Ibrahimu ni baba yao wa Imani, na anapo mtaja Mungu wa Isaka anawarudisha katika historia yao, historia ya Yakobo na uzao wake, (Mwanzo 28:13) Kwa kuwataja Ibrahimu, Isaka na Yakobo inavuta hisia ya Wana wa Israeli walivyo kombolewa na Musa (Kutoka 3:15). Kutoka kwao Taifa la Isreal ndiko liliko anzia. Maneno Mungu wa Baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika hotuba ya Petro ni kuwakumbusha maisha ya furaha wanawaisraeli walivyo ishi. Mahusiano mazuri yaliyokuwepo kati yao na Mwenyezi Mungu kipindi cha hawa wazee. Nasi katika familia zetu wazee waliishi na kuishudua hii Imani nyakati zote ziwe za raha au shida, magonjwa au uzima walidumu kumshuhudia Kristo. Kuwakumbusha nyakati walizoishi Imani thabiti kwa Mungu na nyakati walizoteteleka katika Imani kwa Mungu. Sisi nasi kuna kipindi tunakuwa motomoto katika Imani na kuna kipindi tunalegea.
Alitaka kuwakumbusha maneno walosema kumwambia Yesu (Yohane 8:33) Sisi tu uzao wake Ibrahimu wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wowote nawe wasemaje mtakuwa huru? Mungu huyo huyo Ibrahimu, Isaka na Yakobo ndiye aliye mtukuza mtumishi wake Yesu. Nyinyi mlimuua Asiye na kosa mwenye haki. Kwa maneno mengine mmemua ndugu yenu. Hapo ikawachoma mioyo yao. Mtume Petro kaigawa hotuba yake sehemu mbili sehemu ya kwanza amewakumbusha historia ya maisha yao, makosa waliyoyafanya na sehemu ya pili anawapa faraja na ushauri kwamba, Msiumie najua mlifanya hayo kwa kuto kujua na hata watawala wenu walikuwa hawajui. Kama huyo ni mzao wa Ibraimu. Sasa milango iko wazi. Huruma na neema ya Mungu ni kubwa mlongo wa msamaha uko wazi,Yesu mwenyewe alisema msalabani baba wasamehe maana hawajui watendalo Luka 23:34)
Kutokujua sheria sio tiketi ya kuvunja hizo sheria cha maana ombeni msamaha mkatubu. Japo mambo haya si mageni kwenu yalihubiriwa na Mungu tangu nyakati za manabii. Manabi gani? Nabii Isaya 52:13, Mungu asema hivi: “Mtumishi wangu atafanikiwa; atatukuzwa na kupewa cheo, atapata heshima kuu. Mtume Petro anamshuhudia kristo mfufuka kwa kuwaalika watubu dhambi zao. Amewatoa gizani na kuwaweka katika mwanga. Katika Injili wafuasi waliokuwa wamechoka wanaenda Emausi wamekutana na Yesu mfufuka njiani na walimtambua katika kuumega mkate. Wanarudi kumshuhudia Kristo Mfufuka Yerusalemu. Na walipoendelea kueleza yeye mwenyewe akatokea katikati yao.
Kanisa la mwanzo lilijitabanaisha katika Fumbo la Ekaristi takatifu yaani katika kuumega mkate. Mwinjili anataka kutukumbusha uwepo wa Yesu katika maumbo ya mkate na divai. Ekaristi ni asili na kilele cha maisha yetu ya krioho. Fumbo ambalo tunatakiwa kulitafakali na kuliishi katika maisha yetu ya kila siku. Yesu anawazawadia wafuasi wake zawadi ya Amani. Msiogope muwe na Amani. Msifadhaike nasi tunalikwa tunapewa iyo zawadi Imani tuishuudie katika familia zetu, na maaeneo yetu ya kazi. Anawatuma Mitume wawe mashuhuda wakiaanzia Yerusalemu. Nasi tunaalikwa kuwa mashuhuda wa Kristo Yesu, ili kuwavuta wengine, kumfahamu, kumpenda na kumtumikia Mungu na mwisho wafike kwake mbinguni. Katika somo pili tunapewa muuongozo kuwa kumshuhudia Kristo mfufuka kwa kuacha dhambi. Tumsifu Yesu Kristo,