Tafuta

Ekaristi Takatifu ni chemchemi ya umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa Wakristo! Ekaristi Takatifu ni chemchemi ya umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa Wakristo! 

Ekaristi Takatifu ni Chemchemi ya Umoja na Upendo wa Wakristo!

Matunda ya Fumbo la Ekaristi Takatifu: Kukuza na kuimarisha muungano wa waamini na Kristo Yesu. Ekaristi Takatifu inawasaidia waamini kujitenga na dhambi. Ekaristi Takatifu inaimarisha umoja wa Mwili wa Fumbo: Ekaristi inaliunda Kanisa na kuwahamasisha waamini kujitoa mhanga kwa ajili ya huduma kwa maskini. Ni Sakramenti ya uchaji, Ishara ya umoja na kifungo cha mapendo!

Na PadreNikas Kihuko, Mwanza, Tanzania.

Ekaristi ni Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo. Aliyo tuachia katika maumbo ya Mkate na Divai siku ya Alhamisi Kuu.  Ekaristi ni chemchemi ya umoja wa Wakristo. Mtakatifu Augustino, Askofu na mwalimu wa Kanisa alisema, Sakramenti ya uchaji, ishara ya umoja, kifungo cha mapendo.” Ekaristi ni chemchemi na kiunganishi cha waliotawanyika, waliogawanyika walio enda mbali na Mungu hurudia kwa nguvu ya Ekaristi (KKK 1398). Umoja huo wa wakristo unajidhihirisha zaidi katika adhimisho la Fumbo la Ekaristi Takatifu. Mkristo anatakiwa ashiriki na waamini wengine, ikiwa kuna sababu za kuumwa au kuuguliwa na mototo, au kwa ruhusa ya paroko, hizo sababau zinaweza kuvumilika, isipo kuwa mtu asiye shiriki na wengine siku ya Jumapili anatenda dhambi kubwa. Mara ngapi tumetenda dhambi ya kutoshiriki katika Ekaristi kwa kutokuja Kanisani? (KKK 2181). Katika somo la kwanza Kitabu cha Kutoka 24:3-8. Musa akawambia watu wa Mungu maneno yote ya Bwana na hukumu zake zote watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, maneno yote aliyosema Bwana tutayatenda.  Musa akaandika maneno ya Bwana, akamjengea madhabau Mungu, alitoa sadaka ya kuteketezwa, akamchinjia Bwana sadaka za amani za ng’ombe. Akachukua damu akawanyunyizia madhabahu, kisha akachukua Kitabu cha Agano akawasomea watu, wakasema hayo yote tutayatenda na tutayatii. Kisha Musa akaitwa ile damu, akawanyunyizia watu akasema” Hii ni damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maaneno maneno hayo yote.

Wapendwa, Mwenyezi Mungu alifanya Agano na Waisraeli kwa damu ya wanyama. Walisraeli walitii. Agano hilo leo Mungu anafanya nasi tunao kili ukuu wake, tunao amini uwepo wake kwa Damu ya mwanae wa pekee Yesu Kristo. Tumekombolewa kwa Damu Azizi ya Bwana wetu Yesu Kristo. Damu ya wanyama ilinyunyuziwa katika madhabahu, katika kitabu cha Agano na kunyunyuziwa watu bila kujalisha nyadhifa zao, tabia zao, huduma zao, ndivyo neema na baraka zilivyo miminwa kwako bila kujalisha nafasi na vyeo vyao. Kwa Damu ya Kristo, damu ya thamani inawarudishia wakosefu na wasio na haki kuwa wana wa Mungu. Kinachotakiwa kutii kama walivyosema wanawaisraeli hayo yote tutayatii. Somo la pili Waraka kwa Waebrania 9:11-15, linasisitiza tuliyoyasikia katika somo la kwanza. Kwamba kama Waisraeli walinyunyuziwa damu ya mbuzi, na mafahali na majivu ya ndama ng’ombe, walionyunyuziwa wenye uchafu wakatakasika Damu Azizi ya Kristo ni zaidi ya damu ya wanyama. Sio kwamba haikuwa na nguvu bali ilitakiwa na nguvu. Ila damu ya Kristo ina nguvu zaidi, kama damu za wanyama ziliwakatisha waizraeli, damu ya Kristo inatakatisha dhamili zetu, zambi zetu, udhaifu wetu na kutuunganisha kuwa wana wa Mungu. Kuishi kwa umoja na ni chemichemi ya umoja katika maisha yetu.

Katika somo la Injili kama ilivyo andikwa na Marko14:12-16,22-26. Wafuasi wa Yesu, wanamuuliza ni wapi utakapo tuende tukakuandalie uile Pasaka? Maandalizi yalijikita katika mambo matatu, kwanza mkate usiotiwa chachu, pili mboga za majani, na kitu cha tatu ni mwana kondoo wa Pasaka. Pasaka ya Waisraeli walitumia vitu hivi vitatu mboga zenye uchungu kuonyesha machungu ya utumwani Misri. Akatuma wa wili katika wanafunzi wake akawambia nendeni zenu mjini, atakutana nanyi mwamamume amechukua mtungi wa maji. Mwinjili Luka 22:8 amesema hao wanafunzi wawili walikuwa Petro na Yohane. Wataalamu wa Maandiko Matakatifu wanasema Yesu alishapanga kabla ya kuwatuma wafuasi.  Wengine wanasema Yesu alikuwa anauwezo, nguvu na ukuu wa Yesu wa kujua mambo ya mbele yatakayo endelea na matukio ya mbele.

Maana mila na desturi za Kiyahudi kumwona Mwanaume kujitisha mtungi sio kawaida. Kazi ya kuchota maji kwa mtungi ilikuwa ya akinamama na wafanyakazi. Leo baba kabeba mtungi kichwani sio kwenye baiskeli wala pikipiki. Yawezekana Yesu alimwandaa kama utambulisho wa Mitume waweze kujikita katika Injili ya huduma ya upendo. Lakini Mwinjili Marko ameonesha kama ishara Mitume waweze kutofautisha na kina mama walio beba mitungi. Chakula kwa Wayahudi ni ishara ya upendo na ishara ya urafiki. Chakula kiliwaunganisha katika umoja wao. Ekaristi ni chemchemi ya umoja, upendo na mshikamano wa udugu wa kibinadamu. Wayahudi walishiriki Mlo wa Pasaka hatua kwa hatua!

1.     Kubarikiwa kwa kwa sherehe na divai,

2.     Kikombe cha kwanza cha divai kililetwa na kunyweka

3.     Kililetwa chakula yaani mkate usiotiwa chachu,

4.     Mboga za majani yenye uchungu, matunda na kondoo.

5.     Watoto waliuliza maswali na wazazi waliwajibu huku mlo ukiendelea.

6.     Baba alikuwa na wajibu wa kuwaeleza simulizi la kutoka utumwani,

7.     Lilifuata neno la shukrani kwa kukombolewa kutoka utumwani.

8.     Wimbo uliimbwa kutoka zaburi ya 113-115,  Kisha kikombe cha pili cha divai kilizungushwa. 

10.   Walichukua mkate na matoleo,

11.   Waliumega mkate kwa pamoja.

12.  Walikula mkate na mboga chungu.

13.  Kula mwanakondoo waliomlosti.

14.  Kikombe cha tatu kilifuata na sala maalumu ya shukrani. 15.Waliimba zabuli 116-118.

16.  Kisha walimalizia kikombe cha nne cha divai. 

Wakristo wa Kanisa la mwanzo walibadili sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi wakijikita zaidi kwa Kristo. Kanisa iliazimisha pasaka ikijikita zaidi kwa Yesu badala ya kukumbuka kutoka utumwani. Walipo kuwa wakila Yesu akachukua mkate, akabariki, akaumega akawapa akasema. Twaeni huu ni mwili wangu.Ukiangalia mfululizo wa matukio ya huo mlo inaonyesha hapo ni kati kati ya mlo, katikati ya sherehe. Katika sherehe hiyo Yesu amechukua nafasi ya wazazi ya kubariki, kufafanua maswali mbali mbali ya wanafamilia kama hatu za sherehe zinavyo onesha, kuumega mkate na kuwagawia wanajumuiya au mitume.  Hii aliifanya baada ya kunywa kikombe cha pili cha divai. Katika kila familia ina mkuu wa kaya, anaye simamia taratibu zote za familia kama familia za Kiyahudi zilivyofanya. Twaeni mle; huu ni mwili wangu (Matthayo 26:26) Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akawapa akasema “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yeu. Fanyenyi hivi kwa kunikumbuka” (Luka 22:19). Mtume Paulo anasema Yesu alisema, “Akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: Huu ndio mwili wanguulio kwa ajili yenu: fanyeni hivi kwa kunikumbuka” (1Kor11:24).

Kanisa Katoliki linafafanua maneno hayo kama (Transubstantiation) maana yake mkate na divai vinakuwa mwili na damu ya bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama kwa macho yanabaki maumbo ya mkate na divai. Hii ina maana kwamba Yesu ameipa maana mpya mkate na divai. Kwamba, yupo pamoja nasi katika maumbo ya mkate na divai. Ekaristi ni Sakramenti ya uwepo. Yesu yupo pamoja nasi akiuunganisha mataifa yote ni chemchemi ya umoja wetu. Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema, “Hiki ni kikombe cha agano jipya linathibitishwa kwa damu yangu. Fanyani hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka (1Kor11:25).  Mathayo anasema “Kisha akatwaa kikombe cha divai akashukuru, akawapa akisema, “Kunyweni nyote, maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuondolewa dhamb.(Mathayo 26:27-28)  Luka naye amesisitiza kuwa, “Akafanya hivyo hivyo na kikombe cha divai baada ya chakula, akasema,” Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayo mwagika kwa ajili yenu” (Luka 22:20)

Yeremia alitabiri kwa agano jipya litakalo andikwa katika mioyo ya watu.  “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya Agano Jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.” Nami nitakuwa Mungu wao (Yeremia 31:31-34). Hiki ni kikombe cha tatu katika mfululizo, baada ya hiki inafuata nyama iliyorostiwa ya kondoo. Agano ni makubaliano baina ya pande mbili. Makubaliano yanaoyo weka wazi faida ya sehemu zote mbili na fursa zilizopo pande zote mbili. Kuna maagano mengi, ya aina nyingi, ya namna mbali mbali. Mungu ameweka maagano na Nuhu (Mwanzo 6:18; 9:9-15), pia Mungu aliweka agano na Abraham atakuwa baba wa mataifa, atakaye mbariki atabarikiwa atakaye mlaani atalaaniwa, (Mwanzo 12:1-3). Mungu akafanya tena Agano na Musa (Kutoka 24), na Yoshua (Yoshua 24) Daudi (2Samueli 7:12-17). Mapokeo yanasema hata wazee wetu walikuwa wanaweka maagano ya urafiki na familia nyingine, mataifa wanawek maangano ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, baina ya mataifa mengine. Mume na mke wana weka agano nitakuwa wako milele. Hapa Yesu kwa kuweka Ekaristi anaseme hili ni Agano Jipya.  Litakalo unganisha watu wote, mataifa yote fanyeni hivi kwa ukumbosho wangu. Agano litakalo wavutia watu wote kwa Yesu. Wataungana na Yesu.

05 June 2021, 08:27