Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kwa njia ya maisha yao adili na matakatifu. Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kwa njia ya maisha yao adili na matakatifu. 

Tafakari Jumapili 15 ya Mwaka B: Uinjilishaji na Ushuhuda!

Tumwombe Mwenyezi Mungu tuweze kuwa na maelewano mazuri katika familia zetu sehemu zetu za kazi na zehemu zetu biashara kama kielelezo cha ushuhuda wa Kristo Yesu kati yetu na kama chachu ya unjilishaji mpya unaojikita katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko! Mitume hata katika tofauti zao msingi, lakini kwa pamoja waliungana kumtangaza na kumshuhudia Kristo.

Na Padre Nikas Kiuko, Mwanza, Tanzania.

Utangulizi: Karibuni katika adhimisho la misa takatifu. Leo ni dominika ya 15 mwaka B wa Kanisa. Masomo yetu leo yanatualika kushirikiana, kuchukuliana na kusaidiana katika kazi zetu na kuweka pembeni tofauti zetu kama tutakavyo sikia katika Injili. Tunapo kosa kuelewana utendaji unakuwa mgumu kama somo la kwanza linavyoeleza mfarakano kati ya Amazia na Amosi. Tunapo elewana Mungu anatubariki kama tutakavyo sikia katika somo la pili. Tumwombe Mwenyezi Mungu tuweze kuwa na maelewano mazuri katika familia zetu sehemu zetu za kazi na zehemu zetu biashara kama kielelezo cha ushuhuda wa Kristo Yesu kati yetu na kama chachu ya unjilishaji mpya unaojikita katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko! Mitume hata katika tofauti zao msingi, lakini kwa pamoja waliungana kumtangaza na kumshuhudia Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kutoka kwa wafu! Si tu kwa maneno, bali hata kwa njia ya ushuhuda wa maisha yao!

TAFAKARI: Yesu aliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili. Kwa nini awatume wawili wawili sio mmoja mmoja waende maeneo mengi? Au kwa nini hakuwapeleka watatu watatu ili wasaidiane utume. Maandiko matakatifu yanasema, alianza kuwatuma wawili wawili. Kwa sababu ya sheria za Kiyahudi inasema “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili (Wahebrania 10:28) Kwa sababu ushaidi wa mtu mmoja anaweza kukosea. Yesu hakutuma watatu kwa sababu angetuma watatu aliona binadamu ni dhaifu wangeungana wawili katika uovu na watatu anaye jua ukweli angebaki pekeake na ukweli wangeupotosha. Akawatuma wawili wawili wakamshuhudie kwa mataifa, wakafundishe ufalme wa Mungu. Sababu ya pili aliwatuma wawili wawili ili mmoja akipatachangamoto asaidiwe na mwingine, waweze kusaidiana. Walindane katika maeneo hatarishi na kupeana ushauri na faraja katika magumu, katika kukataliwa au kupokelewa. Wawili watapata tuzo lao, “Ikitokea mwenzake ameanguka huyo mwenzake atamwinua” lakini akiwa peke yake huyo mtu hatakuwa na mtu wa kumwinua. (Mhubiri 4:9-11) Lengo ni kukabiliana na majaribu katika maisha. Yesu amewatuma wawili wawili katika mitume wake kumi na wawili. Hebu jiulize alitumia vigezo gani? Mitume walikuwa katika makundi sita nani alikuwa nan ani?

 Ukiangalia waliitwa katika mazingira tofauti, tabia tofauti na desturi tofauti.  Mfano Simoni Petro alikuwa mtu wa maamuzi ya haraka, shupavu na jasiri haogopi hali ya hatari, mwenye kuthubutu “Bwana mimi nipo tayari kwenda pamoja na wewe Gerezani n ahata kufa (Luka 22:33) Mwenye hasira “Simoni Petro alikuwa na upanga, basi akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu (Yohane 18:10) Mwenye uaminifu na upendo mkubwa kwa Yesu, “Bwana wewe wajua yote, wewe wajua nakupenda” (Yohane 21:15-17). Maskini Thomaso mtume yeye ni mtume mwenye mashaka, anajulikana kwa jila la Pacha, wanataalimungu wanamtaja kuwa Mtume mwenye mashaka.  Kwa sababu ya kutoamini kwakwe ufufuko wa bwana wetu Yesu Kristo, “Mimi nisipoona mikononi mwake alama za misumari na kutia kidole change katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki” (Yohane 20:24-29), mtu anayetaka kuona ili aamini, mwenye mashaka utampanga na nani? Yuda anajulikana kwa tabia ya usaliti. Utampanga na nani? Je, Simoni Petro alipangwa na Andrea kaka yake? Maana akiwapanga Yakobo pamoja Yohane mwana wa ngurumo (Marko 3:17) Patakuwa fujo, vurugu na nguo kuchanika!

Kushirikiana, kuchukuliana na kusaidiana katika kazi zetu na kuweka pembeni tofauti zetu kama tulivyo sikia katika Injili ni muhimu sana. Tunapo kosa kuelewana utendaji unakuwa mgumu kama somo la kwanza linavyoeleza mfarakano kati ya Amazia na Amosi. Tunapo elewana Mungu anatubariki kama tulivyo sikia katika somo la pili. Tumuombe Mungu tuweze kuwa na maelewano mazuri katika familia zetu sehemu zetu za kazi na zehemu zetu biashara. Tabia ya kila mtume anawakirisha tabia zetu katika jamii ya leo. Wapo wenye hasira, maamuzi ya haraka na wenye mapendo ya kweli. Wapo wasaliti katika ndoa, katika Maisha ya kila siku, wapo watulivu na wanaopenda amani na wenye maamuzi sihii katika Maisha yao. Sasa tunatumwa tukaihubiri injili kwa matendo yetu. Utaenda na nani?

Tunakumbushwa naona gani ugumu unajitokeza kwa wakubwa wetu kupanga majukumu ya kazi. Nani nimpange na nani? Kina nani wakaa wawili watafanya vizuri, patakuwa na amani, pataleta matunda mazuri, hapo ni neema na nguvu ya Mungu inahitajika. Hapo panakuwa pagumu katika kuchukua uamuzi, niolewe na nani? Nimuoe nani? Watu wanachukua miaka mingi kuchunguzzana tabia na mwenzake. Akihofia atakaye muoa au kuolewa naye atarithi tabia ya mtume gani? Petro, Yohane au Yuda? Kumbe tuna alikwa kupokeana tulivyo. Kuheshimiana, kuthaminiana na kuchukuliana katika mapungufu yetu.  Tofauti na hapo, daktari atashindwa kufanya kazi na nesi, mwali hawezi fanya na mwalimu mwenzake, padre atashidwa kukaa kwenye jumuiyani, sista atashindwa kukaa katika jumuiya. Hivyo Yesu kwa kuwatuma wafuasi wake nao wakaweka tofauti zao pembeni. Anatualika nasi tuwe na mahusiano mazuri sehemu zetu za kazi.  

Yesu akawapa amri juu ya pepo wachafu (Marko 6:7) Mwinjili Marko hatasema kuhusu kufundisha kama wainjili wengine kuwa kitovu cha utume wa Yesu. Marko amesisitiza katika safari yao mitume wakahubiri kwamba watu watubu, wakatoe pepo, wakapake Mafuta wagonjwa, (Marko 6:12) Hapo hapo akawakataza wasichukue kitu cha njiani. Wamtegemee Mungu katika mahitaji na utume wao. Lakini hata kama walikuwa na tofauti zao, tabia zao walikamilishana mmoja na mwingine, walisaidiana katika utume walopewa na Yesu, walichukuliana katika utendaji wao. Hivyo baada ya kazi wanaleta ripoti kwa Yesu. Wali tii kwenda walikoambiwa na Yesu. Wakiwa dhaifu lakini walifanya mambo makubwa kwavile walimtegemea Mungu. Walihubiri watu watubu kwa umoja wao (Marko 6:12) Walitoa pepo (Marko 1:25-26) Waliponya wagonjwa.  Tuanaalikwa kushirikiana katika majukumu yetu, ofisi tulizo kabidhiwa, majukumu tuliyopewa. Tunatakiwa kuweka pembeni tofauti zetu na kuchapa kazi kwa bidi. Haijarishi umepangwa na nani. Mpokee alivyo mfanye kazi ya Mungu.

08 July 2021, 15:00