Cameroon:Monsinyo Julius Agbortoko Agbor ameachiwa huru
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Padri wa jimbo katoliki la Mamfe, kusini magharibi mwa Camroon aliachiliwa bila kulipa fidia na alikuwa ametekwa nyara siku ya Jumapili tarehe 29 Agosti. Taaifa hii imetangazwa tarehe 31 Agosti 2021 na Kansela wa Jimbo huko Cameroon, Padre Sébastien Sinju.
“Tunamshukuru Aliye Juu Zaidi aliyemweka Monsinyo Julius Agbortoko Agbor kuwa salama wakati wa kifungo chake na kumrudisha kwetu salama salimini”, inasema taarifa hiyo iliyosainiwa na Padri Sinju, ambaye alinukuliwa na Shirika la Habari za kimisionari Fides. Kansela ameshukuru jumuiya za Kikristo na wale wote ambao, wakiwa nyumbani na nje ya nchi, walikuwa nao bega kwa bega wakati wanaunganika katika maombi. Na kwamba Mungu wabariki.
Kwa kuachiliwa kuhani huyo, watekaji nyara walikuwa wameomba fidia ya faranga milioni CFAi 20 (kama euro 30,489). Inavyoonekana hata hivyo jumla isingeweza kulipwa. Monsinyo Agbortoko Agbor alikamatwa na kutekwa nyara Jumapili tarehe 29 Agosti 2021 na baadhi ya vijana wenye silaha, ambao walikuwa wamehitimu kama watenganishaji, na ambao walikuwa wameshambulia seminari kuu ya Mamfe. Kusudi lao, kwanza lilikuwa kumnasa Askofu Francis Teke Lysinge, Askofu Mstaafu wa jimbo la Manfe. Lakini kutokana na uzee wa Askofu huyo, wahalifu hao walipendelea kumuondoa msimamizi wa jimbo hilo Monsinyo Agbor.