Tafuta

2021.09.28 Katika ziara ya kichungaji ya Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa  Jimbo katolili la Bukoba Tanzania katika Parokia ya Bumbire, alitoa Sakramenti ya kipaimara na Komunio tarehe 26 Septemba 2021. 2021.09.28 Katika ziara ya kichungaji ya Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo katolili la Bukoba Tanzania katika Parokia ya Bumbire, alitoa Sakramenti ya kipaimara na Komunio tarehe 26 Septemba 2021. 

Tanzania,Askofu Kilaini:Kila mbatizwa awe mtu sala na kumtanguliza Mungu kwa kila kitu

Katika ziara ya kichungaji katika Parokia ya Bumbire inayojumuisha visiwa vya,Kerebe,Goziba,Makibwa,Nyaburo na Rushonga,Jimbo la Bukoba ,Tanzania,Askofu Msaidizi Kilaini ameshauri waamini kulinda na kuitetea imani ya Kikristo bila aibu ya ishara ya Msalaba na nyingine.Katika ziara hiyo ametoa sakramenti ya Kipaimara na Komunio.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican na Patrick P. Tibanga - Radio Mbiu,Kagera.

Wakristo wakatoliki wameombwa kuilinda na kuitetea Imani ya Kikristo kwa kumtanguliza Kristo na kuweka visakramenti na picha Takatifu ambayo ni alama ya ukristo katika nyumba zao na kujiunganisha na Mungu kwa njia ya sala. Wito huo umetolewa na Askofu msaidizi wa jimbo Katoliki la Bukoba Askofu  Methodius Kilaini wakati wa ziara yake ya kichungaji katika visiwa vya Parokia ya Bumbire iliyoambatana na utoaji wa Sakramenti ya Kipaimara pamoja na Ekaristi takatifu katika Parokia ya Bikira Maria Nyota ya Bahari Bumbire Jimbo Katoliki la Bukoba kwa watoto na watu wazima.

Askofu Kilain akiwa katika boti Kuelekea Parokia ya Bumbire na Mapadre
Askofu Kilain akiwa katika boti Kuelekea Parokia ya Bumbire na Mapadre
Askofu Kilain akiwa katika ziara ya kichungaji Parokia ya Bumbire
Askofu Kilain akiwa katika ziara ya kichungaji Parokia ya Bumbire

Hata hivyo Askofu Methodius Kilaini akiwa katika ziara yake ya kichungaji katika visiwa vya Parokia ya Bumbire kuanzia tarehe 23 hadi 27  Septemba 2021 alianzia katika kisiwa cha Kerebe, Goziba, Makibwa, Nyaburo na Rushonga ambapo aliweza kufurahishwa zaidi na ushuhuda wa imani ya waamini wa visiwa hivyo kwa namna wanavyoishi na kumtanguliza Kristo katika maisha yao ya  sala licha ya changamoto mbali mbali walizo nazo za maisha  katika visiwa hivyo.

Askofu Kilain akikaribishwa na waamini kisiwani
Askofu Kilain akikaribishwa na waamini kisiwani
Misa ya Sakramenti ya Kipaimara na Komunio katika Parokia ya Bikira Maria Nyota ya Bahari
Misa ya Sakramenti ya Kipaimara na Komunio katika Parokia ya Bikira Maria Nyota ya Bahari
Misa ya Sakramenti ya Kipaimara na Komunio katika Parokia ya Bikira Maria Nyota ya Bahari
Misa ya Sakramenti ya Kipaimara na Komunio katika Parokia ya Bikira Maria Nyota ya Bahari

Katika mahubiri yake Dominika tarehe 26 Septemba 2021, Askofu Kilaini amesema kuwa kila mkristo mbatizwa anatakiwa kuwa kweli mtu wa sala na kumtanguliza Mungu katika nyakati mbali mbali za maisha na kuweka alama ama picha takatifu na visakramenti ambavyo vinampeleka mkristo kwa Kristo mwenye huruma anayewapa nguvu  na kuwataka wakristo kutumia visakramenti hivyo kwa kuilinda na kuitetea imani ambayo itawasaidia kuyaishi maisha matakatifu. Askofu ametoa mifano kadhaa  kuhusiana na hayo ndani na nje ya familia namna ya kuishi ushuhuda wa ukikristo asa akisisitiza kuwa “ Usiwe na nyumba isiyo na picha  ya kikristo kama ni mkatoliki”.

Askofu Kilain akiwa na Chama cha Utoto Mtakatifu
Askofu Kilain akiwa na Chama cha Utoto Mtakatifu
Askofu Kilain anapokea zawadi ya mbuzi
Askofu Kilain anapokea zawadi ya mbuzi
Askofu Kilain anapokea zawadi
Askofu Kilain anapokea zawadi

Askofu Kilaini katika mahubiri hayo amesema kuwa kila mkristo mkatoliki anatambulika kwa ishara ya Msalaba ambayo ni nguzo kuu ya Utatu Mtakatifu bila kuona haya mbele ya watu, na kwa maana  anatakiwa kufanya ishara ya msalaba na kuishi maisha ya maadili mazuri na kuwataka waimarishwa kuyaishi mapaji saba ya Roho Mtakatifu ili yapate kuwasaidia katika maisha yao na zaidi kumshirikisha Mungu kwa kila jambo wanalo litenda katika maisha yao ya kila siku, pamoja na kuhudhuria Misa Takatifu.

MAHUBIRI YA ASKOFU MSAIDIZI KILAINI JIMBO LA BUKOBA
28 September 2021, 17:06