Tafuta

2021.09.15 Misa katika Kilima cha Kayungu,Jimbo katoliki Kayanga, Tanzania, katika Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba tarehe  14 Septemba 2021. 2021.09.15 Misa katika Kilima cha Kayungu,Jimbo katoliki Kayanga, Tanzania, katika Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba tarehe 14 Septemba 2021. 

Tanzania:Pd.Kiiza,kuweni Wakristo wa msamaha!

Jimbo katoliki Kayanga,Tanzania limeadhimisha Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba katika kituo maalum kiitwacho Kalvario Kayungu,sambamba na maadhimisho ya Misa ya Papa huko Prešov,Slovakia katika Hija ya kitume.Mahubiri ya Makamu Askofu Pd.Kiiza yamejikita katika Fumbo la Msalaba na kuwaalika wakristo kusamehe.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika siku ambayo Mama Kanisa anasheherekea Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba,  tarehe 14 Septemba ya kila mwaka, Papa Francisko alikuwa huko Prešov nchini Slovakia  akiwa katika Hija ya Kitume  kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba 2021 ambayo imeongozwa na kauli mbiu “Pamoja na Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu. Njia ya Kwenda kwa Yesu. Papa alitoka asubuhi Bratislava Jimbo kuu la Prešov, na kuadhimisha Liturujia Takatifu katika Madhehebu ya Kibizantina. Katika mahubiri yake amesisitiza juu ya maana ya msalaba na hasa kutoa onyo la kuwa na kishawishi cha kutokubali Fumbo la Msalaba. Papa amewaomba Wakristo kwamba kamwe wasiupunguzie msalaba katika mambo rahisi iwe katika kwa ishara ya kisiasa au ishara muhimu ya kidini na kijamii. Papa pia amebanisha jinsi ambavyo tuko hatarini ikiwa hatukubali mantiki ya msalaba, kwamba “Mungu anatuokoa kwa kuruhusu uovu wa ulimwengu umgeukie hata yeye.

Msalaba ni ushindi
Msalaba ni ushindi

Jimbo la Kayanga katika Kituo cha Hija cha Kalvario Kayungu:msalaba ni wokovu: Na katika Jimbo katoliki la Kayanga nchini Tanzania, limeungana na Kanisa liote la ulimwengu na pia na Baba Mtakatifu Francisko kuadhimisha Siku Kuu hiyo katika Kituo chake Maalumu kiitwacho ‘Kalvario Kayungu’, ambacho kiliwekwa wakfu kwa ajili ya hija hiyo ya kila mwaka kwa karibu miaka 12 iliyopita. Tukio ili limewajumuisha maelfu ya waamini kuanzia watoto, vijana watu wazima, watawa na mapadre kutoka sehemu mbali mbali za Jimbo la Kayanga, lakini pia hata nje ya jimbo la Kayanga ili kushirikia Ibada ya Misa Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo katika kilima hicho pamoja na kuwa na msukosuko unaotishia wa janga la UVIKO-19. Nyimbo ziliongozwa na kwaya ya Mtakatifu Cecilia, wa Parokia ya Nyakatuntu. Wakati huo huo waratibu wa hija hiyo walikuwa ni Gambera wa Vituo vya Hija Jimboni: Padre Nicodemus Byakatonda akishirikiana na Parokia ya Kimkakati Kayungu ambayo inaongozwa na Padre Thadeus Waako.

Mapadri wa Jimbo la Kayanga katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Mapadri wa Jimbo la Kayanga katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Waamini watu wa Mungu katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Waamini watu wa Mungu katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021

Waamini wanapaswa kuwa watu wa msamaha kama wakristo: Katika tukio hili takatifu, Ibada ya misa iliongozwa na Makamu wa Askofu Padre Ibrahimu Kiiza akishirikiana na mapadre wengine waliofika katika hija hiyo. Katika mahubiri yake Padre Kiiza amewataka wakristo kujipima, kujitafiti na kuembea kupitia mchakato wa njia ya msalaba kwa sababu hija ni safari ya kiroho kwa wakristo. Akiendelea kusistiza zaidi amesema hija ni tafakari ya ndani na ni upatanisho na mungu na jirani ili kuwa na mshikamano na Yesu, huku akitolea mfano halisi alio ufanya Yesu Kristo akiwa katikati ya wanyang’anyi wawili msalabani mmoja kule na mwingine kushoto. Kwa hakika waamini wanapaswa kuwa watu wa msamaha kama wakristo.  Kwa kufanya hija hiyo inawasaidia kutafakari kwa kina juu ya ukombozi wao na kuonja kwa dhati msamaha kupitia Msalaba ambao unatoa mafundisho yampendezayo Mungu anayetoa kitulizo. Kutokana na hiyo ndipo Padre amewasihii kuishi maana ya Fumbo la Msalaba ambao ni alama ya ushindi.

Kwaya katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Kwaya katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Watawa katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Watawa katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021

Wanadamu msipenda kulalamika na kutotambua mpango wa Mungu: Padri Kiiza akiendelea na mahubiri yake amwaonya wanadamu wasipende kulalamika na kutotambua mpango wa Mungu kama wana wa Israeli walivyonungunika katika safari yao bali wawe watu wanaopaswa kuwajibika na kujituma kwa kutumia akili aliyowapatia Mwenyezi Mungu na kuacha kupoteza hofu ya Mungu ili hatimaye wanaweza kupata suluhisho la matatizo. Hata hivyo kama ilivyo kiutamaduuni, kwa kila mwaka ifikapo tarehe 14 septemba hufanyika tukio hilo la hija mahali ambapi hutanguliwa na mkesha wa sala kwa waamini katika kujiandaa kikamilifu na siku kuu hiyo; kwa bahati mbaye, mwaka huu haukufanyika mkesha huo kutokana na janga la UVIKO-19 ambalo bado linaendelea kutesa mamilioni ya watu ulimwengu mzima.

Waamini watu wa Mungu katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Waamini watu wa Mungu katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Waamini watu wa Mungu katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
Waamini watu wa Mungu katika maadhimisho ya misa tarehe 14 Septemba 2021
KALVARIO KAYUNGU-KAYANGA TANZANIA
15 September 2021, 11:42