Tafuta

 Watoto katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Msumbiji Watoto katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Msumbiji  

Cypus:zawadi ya kuunga mkono kampeni ya chanjo ya UVIKO kwa ajili ya Msumbiji &CAR

Imetolewa zawadi ya kutoka Serikali ya Nocosia huko Cyprus kwa ajili ya Kampeni ya Chanjo barani Afrika.Hii ni mara baada ya ziara ya kitume ya Papa Francisko.Msaada huo utakwenda kwenye mpango wa DREAM wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Msumbiji na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Serikali  ya Jamhuri ya Cyprus imeunga mkono kwa kutoa zawadi katika kampeni ya chanjo kwa ajili ya UVIKO-19, kwa nchi mbili za Bara la Afrika: Msumbiji na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ushirikiano na Mpango wa DREAM ambao ni wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio unaoshika kasi kubwa katika uhai wake kwa miaka sasa hasa katika harakati za mapambano ya kutibu na kuzuia Virusi vya UKIMWI barani Afrika.

Uamuzi huo kwa upande wa serikali ya Nicosia umetolewa mara baada ya ziara ya kihistoria ya Papa Francisko hivi karibuni na kama kielelezo cha kutoa shukrani na mshikamano ambao kutokana na maneno ya Papa yaliweza kwa hakika kuibua hisia za ndani na kugusa moyo wa watu wa Cyprus.  Huo ni wito wa nguvu kwa ajili ya wakimbizi ambao wamo ndani ya kisiwa hicho na sehemu kubwa hasa ni wale wanaotoka katika bara la Afrika.

Fedha hizo zilizotengwa kwa mujibu wa taarifa ni kwamba zitaruhusu kuongezea chanjo ya kuzuia UVIKO-19, katika vituo vya DREAM vinavyoendeshwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika wakati huu mgumu sana wa mahangaiko na wasi wasi kwa ajili ya wimbi jipya na shughuli  ambayo inaendelea kurekodiwa visa kwa kasi katika nchi nyingi za Afrika hasa kwa sababu ya usambaaji wa aina hii mpya ya Omicron.

21 December 2021, 16:33