Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:John(Ofm),Kanisa maskini kwa ajili ya maskini
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Mkutano wa Papa Francisko na wakimbizi katika kisiwa cha Lesbos ulikuwa ni muhimu sana, kwa sababu Papa Francisko tangu mwanzo wa upapa wake alikuwa amebainisha anavyotaka Kanisa maskini kwa ajili ya masikini na sio maneno bali kwa vitendo halisi, na hayo ndiyo yanakuwa mwendelezo wa kuonesha kwa matendo. Amethibitisha hayo Padre John-Luke Gregory, Mwakilishi wa Nchi Takatifu huko Rodi, kiswani Ugiriki, akifafanua vipindi muhimu na vyenye maana katik safari ya Kipapa huko Cyprus na Ugiriki ikiwa ni ziara yake ya 35 ya kitume kimataifa ambayo imehitimishwa Jumatatu tarehe 6 Desemba 2021.
Padre Gregory, ambaye anatoa huduma ya kichungaji kwa wahamiaji na wakimbizi, pamoja na Ndugu zake wengine wadogo Wafranciskani (OFM) wanaoishi katika Jumuiya ya Rodi kwenye Wilaya ya Usimamizi wa Nchi Takatifu, (www.custodia.org) amesimulia hisia yake juu ya ziara ya kipapa. Padre Gregory ameonesha furaha kubwa kwa ziara hiyo ya kipapa kwa sababu mbili: Kwanza ikiwa ni ya kuongeza nguvu na moyo kuhusu uhusiano na Kanisa la Kiorthodox na pili kwa sababu ya kutoa sauti kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi ambao mara nyingi wana sahulia na kuachwa pembeni. Siku za hivi karibuni amesema kwamba Meya wa Rodi alimwambia kuwa hadi sasa wamepita watu 25,000 katika kisiwa chao, ambayo ni idadi kubwa sana. Na kwa watu wote hao, amebanishani kwamba Kanisa Katoliki, ikiwa na maana wao wamekuwa mstati wa mbele kujibu kila aina ya hitaji la kila siku kwao na yeye ni shuhuda wa kwanza kuona hayo yakitendeka.
Akikumbusha juu ya mahubiri ya Papa Francisko aliyofanya katika Uwanja wa Mpira wa Nikosia, ametaja jinsi alivyopendezwa naye sana kwani Papa alisema: “tunapaswa kujifunza kuchukuliana majeraha kwa pamoja.”Kwa maana hiyo Padre Gregory ameongeza kusema kwamba suala hili kwa hakika ndiyo ufupisho mzuri wake katika Waraka wa Fratelli tutti, yaani wote ni ndugu, kwa sababu kila mmoja kwa hakika ana majeraha yake na kwa kushirikishana inakuwa si rahisi kuhisi pweke na kuachwa pekee. Suala hili pia ni msingi katika utunzaji wa wahamiaji na wakimbizi ambao wanahisi kuachwa peke yao. Kukarimu wote na kwa ufunguzi wazi kwao ndizo tabia muhimu zaidi na ambazo kwa mujibu wa Padre Gregory amethibtishwa kwamba Papa anajaribu kuonesha kwa ukamilifu sana.