Iraq:Ujumbe wa Kardinali Sako kwa ajili ya Noeli:Amani na upatanisho
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Kati ya wasi wasi mbele ya hali halisi ya kisiasa iliyojaa mivutano, migogoro na changamoto zilizotokana na uchaguzi, uchafuzi wa mazingira, mabadilio ya tabianchi na janga la UVIKO-19, kuzali kwa Kristo ni njia ya kutaka kukumbusha nguvu ya ujumbe wa matumaini, amani, udugu, upendo, mshiakamano na Mungu. Noeli ni fursa kwa ajili ya kuongeza nguvu imani na kupyaisha matumaini na shauku kuu, na ni wito wa amani na usalama, huruma, hadhi, mapatana na kuongeza uhusiano zaidi ya kidugu. Ndivyo unaanza Ujumbe wa Noeli wa Patriaki wa Kikaldayo, Kardinali Louis Raphael Sako, uliochapishwa na Upatriaki wa Kikaldayo.
Kuzaliwa kwa Kristo ni ukumbusho wa Mungu katikati ya watu wake
Katika ujumbe huo, unabainisha kwamba kwa kuzaliwa kwa Kristo inakumbusha uwepo wa Mungu katikati ya watu wake. Kuzaliwa kwake ni kieleleza cha upendo wa Bwana kwa watu wote wa mataifa yote, tamaduni na rika zote, ikiwa ni pamoja na ukaribu wake kwa ajili yao wote. Kutokana na Noeli ndipo zinakuja jitihada za wakristo kujikita katika kutoa huduma kwa Ndugu hasa wale ambao ni maskini zaidi na wadhaifu. Kuzaliwa kwa Kristo ni kurudi katika kisima kwa ajili ya kukabiliana na kusahihisha masuala muhimu katika maisha na kuhamasisha kwa ukomavu na utambuzi zaidi wa kidugu, uvumilivu, amani na upendo!
Noeli ni chemi chemia ya tumaini
Kwa mujibu wa Kardinali Sako anasisitiza kwamba Noeli ni chemi chemi la tumaini ikiwa linajikita kwa undani katika utume wa kisiasa na katika huduma kwa matazamio na matarajio ya wazalendo kupitia maono ya kweli ya kitaifa na nafasi moja thabiti ya mazungumzo na upendeleo wa usalama, demokrasia na hadhi ya watu wa Iraq. Kwa upande wa Kardinali Sako, matumaini haya yanapaswa kwa hakika kutafsiriwa kwa raia na kwa ngazi ya juu ili kukataa tofauti, kuvunja kila aina vipingamizi kwa kudumisha ushiriki wa kitaifa na kutafuta kwa pamoja kujenga Taifa la kiraia, Taifa moja la kizalendo, la haki na usawa.
Taifa moja la kuishi kwa uhuru, hadhi, usawa na usalama
Kardinali Sako anaongeza kusema kuwa liweze kuwa Taifa moja ambamo wazalendo wanaishi kwa uhuru, hadhi, usalama na usawa. Kwa kuhitimisha, anaomba kwamba katika siku ya Noeli wasali kwa ajili ya amani na msimamo wa Nchi yao Iraq na ulimwengu mzima kwa kuacha kila mmoja aangazwe na thamani za uvumilivu, upendo, amani maisha na udugu ili utukufu wa Mungu aliye juu mbunguni na amani duniani uwe kwa watu wenye mapenzi mema, na Bikira Maria awaombee.