Brazil:Mafuriko yasababisha maafa makubwa kwa watu
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Katika wiki za mwisho, mafuriko makubwa yamekumba Mikoa 10 nchini Brazil, kuanzia Kaskazini hadi Kusini na kusababisha maelfu ya mrundikano wa watu ambao wamepoteza kila kitu na kujikuta hawana makazi. Inasadikika ni watu 25 waliopoteza maisha wakati mafuriko makakali huko Kaskazini Mashariki mwa Minas Gerais. Hata eneo la Brumadinho, ambalo linakumbukwa manmo tarehe 25 Januari 2019, kutokana na kupasuka kwa Bwawa kubwa, lilisababisha vifo vya watu 270. Kwa sasa umebaki wasi wasi mkubwa wa kuweza kuleta madhara makubwa ya mabwawa 42 yaliyomo katika Nchi hiyo na miongoni mwake yale ya Usina de Carioca, Parà de Minas na kwa maana hiyo zaidi ya watu 100,000 wameombwa kwenda mbali na maeneo hayo.
Katika Mkoa wa Minas Gerais, bado pia hivi karibuni kulitokea ajali ya kuanguka kwa mwamba ndani ya mto Furnas tarehe 8 Januari 2022 na kusababisha vifo vya watu 10 miongoni mwa watalii waliokuwa kwenye mitumbwi ya kutalii. Matatizo makubwa pia yako katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Bahia mahali ambapo watu 25 walipoteza maisha kutokana na mafuriko. Mwanzoni mwa mwaka huu nchini Brazil kwa maana hiyo wamerekodi hali ngumu sana ya matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi na madhara kama hayo.
Waliokumbwa zaidi ya hayo hata idadi kubwa ya jumuiya za kiasiliali. Mafuriko hayo yanafuata Janga la Uviko -19 ambalo ni dharura inayoendelea kuenea kila kona ambalo kwa sasa limekwisha sababisha vifo vya watu 620,000 katika eneno hilo. Mbele mahitaji ya watu wengi namna hiyo wameanzisha mpango wa kimataifa. Caritas internationalis ambayo inaratibu misaada ikiwa inawasiliana na Caritas ya Brazil. Hata nchini Marekani na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa wameanza kutoa misaada ya kwanza.