Tafuta

2019.04.13 Padre  Dante Carraro, Mkurugenzi Mkuu wa Madaktari na Afrika ( CUAMM) 2019.04.13 Padre Dante Carraro, Mkurugenzi Mkuu wa Madaktari na Afrika ( CUAMM) 

Afrika ya Kati:Cuamm imefikia hata watu zaidi ya 200elfu waliosahauliwa!

Katika maeneo ambayo hakuna mtu anayetaka kufika,huko Afrika ya Kanisa ndiyo lengo la Kikundi cha Madaktari na Afrika(Cuamm)ambao wameweza kuwafikia watu zaidi ya 200,000 katika utume wao,kwa mujibu wa maelezo ya Padre Dante Mkurugenzi wa Cuamm.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hatimaye wamefikia mbio za mwisho, kwa maana walianza mbio zao miaka minne kutoka Bangui katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mahali ambapo inapatikana Hospitali pekee ya watoto katika Nchi hiyo. Katika eneo hilo, waliitwa kujibidisha katika kazi ngumu na nyeti ambayo lakini imepelekea lmatokeo muhimu. Ndivyo anavyojulisha katika barua ya Padre Dante Carraro, Mkurugenzi Mkuu wa Kikundi cha Madaktari na Afrika(Cuamm) ambaye amesimulia  juu ya mitazamo ya kwanza waliyofika katika pembe ya Kaskazini Magharibi mwa Afrika ya Kati, kati ya Chad na Camerun.  Kila mwaka ni karibia watoto 20,000 wanaolazwa katika hospitali na 70,000 ambao wanapokea tiba katika vituo vya maeneo hayo. Katika kabarua hiyo anaendelea kwamba wataendelea na huduma hiyo muhimu sana katika Hospitali ya watoto huko Bangui kwa kusaidia hasa mafunzo ya watu wauguzi na madaktari. Na zaidi, Padre Dante amesisitza kuwa hata madaktati bingwa wa upasuaji na kwa maana hiyo wanayo furaha kuanza hatimaye  hata kazi yao nje yake,  katika maeneo ya vijijini zaidi vya ndani ambavyo vimeachwa na vigumu katika nchi na mahali ambapo hakuna anayetaka kwenda huko. Na ndiyo mbio yao ya mwisho ambayo wanajikita nayo.

Msaada wa Madaktari na Afrika (CUAMM) huko Afrika ya Kati.
Msaada wa Madaktari na Afrika (CUAMM) huko Afrika ya Kati.

Mkurugenzi wa Cuamm ameeleza kuwa katika wilaya mbili za Bocaranga na  Ngaundaye wanaishi watu zaidi ya 200,000. Ni maneo yasiyo na usalama. Tangu 2013 yalianza mapigano kati ya waasi wa kiselikali ambao wanasaidiwa na Ufaransa na jeshi la kawaida linalosaidia na Urusi, kama  wanavyosema. Licha ya hayo katika maeneo hayo ndipo yanapatikana malighafi za kwanza, lakini utashangaa kwamna maeneo hayo ni ya kimasikini sana. Katika Wilaya ya Bocaranga kwa mara ya kwanza hawakuweza kupata hata mkate wa kula na wala  maji yenyewe shida kubwa  na waliweza kula chakula cha jioni, shukrani kutoka kwa msamaria mwema mama mmoja aliyejitolea . Katika hospitali, anasema  nafasi zipo za kulala mia moja lakini kwa zaidi ya watu elfu moja kwa mwaka wanapitia hapo,na kusaidiwa vipimo na tiba shukrani kwa muuguzi mmoja mwenye umri wa miaka 20 mwenye ujuzi wa kikunga ana anayewasaidia wajawazito.

Msaada wa Madaktari na Afrika (CUAMM) huko Afrika ya Kati.
Msaada wa Madaktari na Afrika (CUAMM) huko Afrika ya Kati.

Hakuna maabara, famasi ndiyo hivyo kidogo na wala hakuna daktari hata mmoja. Ukarimu kwa upande wa mamlaka ya kiafya katika hospitali walipofika ilikuwa nzuri sana iliyogusa na ya kidugu. Hata mashine kwa ajili ya Uviko zimeanza kutumiwa. Dozi mwishoni mwa mwaka 2021 zilifika hata Bocaranga. Waliweza kuthibiti na kurekodi katika Hospitali kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 3 Februari 2022 wamepata chanjo watu 958 kuanzia na wahudumu wa Kiafya. Walijikita kuwasaidia kufungua hata visehemu vingine vya kutolea chanjo katika vituo 32 vya vijijini kabisa ambavyo vinahusiana na wilaya hiyo. Kwa namna hiyo wanafungamanisha Chanjo ya UVIKO-19 na chanjo nyingine kwa ajili ya magonjwa mengine. Inatosha kufikiria kuwa ni asilimia ya  25%  tu ya watoto katika eneo hilo ambao wapepata chanjo dhidi ya surua.  Padre Dante, katika barua yake amesisitiza kwa nguvu kuwa chanjo dhidi ya Uviko-19 barani Afrika lazima iweze kusaidia kwa namna moja, mbali na uarahisi unaolewzwa katika vyombo vya habari na magazeti. Lazima kufanya hivyo kwa sababu ni haki, kujilinda na nguvu za kulinda hata mifumo ya kiafya mahalia iliyo midhaifu kabisa, kwa malengo yao matatu katika moja tu.

16 February 2022, 15:31