Tafuta

Tafakari ya Neno la Mungu, Dominika ya VII ya Kipindi cha Mwaka C wa Kanisa. Sisi kama wafuasi wa Kristo Yesu njia yetu ni njia ya upendo. Na upendo huu unatualika kuushinda uovu kwa wema. Tafakari ya Neno la Mungu, Dominika ya VII ya Kipindi cha Mwaka C wa Kanisa. Sisi kama wafuasi wa Kristo Yesu njia yetu ni njia ya upendo. Na upendo huu unatualika kuushinda uovu kwa wema. 

Dominika VII ya Mwaka C wa Kanisa: Kanuni ya Dhahabu: Haki

Somo letu la Injili Lk. 6:27-38 linatualika tuwatendee wangine yale ambayo sisi tunapenda tutendewe. Hii ndiyo Kanuni ya Dhahabu. Sheria hii inagusa kwenye maeneo yetu ya kali siku ya kimaadili, kijamii na kiuchumi. Yesu anasema ufisanye jambo ambalo wewe ukifanyiwa linakuumiza, linakuletea hasira nina acha majeraha katika nafsi yako.. Shindeni ubaya kwa kutenda mema.

Na Padre Nikas Kihuko, - Jimbo Katoliki la Mahenge.

UTANGULIZI Karibuni katika Tafakari ya Neno la Mungu, Dominika ya VII ya Kipindi cha Mwaka C wa Kanisa. Somo letu la Injili Lk. 6:27-38 linatualika tuwatendee wangine yale ambayo sisi tunapenda tutendewe. Hii ndiyo Kanuni ya Dhahabu. Sheria hii inagusa kwenye maeneo yetu ya kali siku ya kimaadili, kijamii na kiuchumi. Yesu anasema ufisanye jambo ambalo wewe ukifanyiwa linakuumiza, linakuletea hasira nina acha majeraha katika nafsi yako. Dominika ya leo tunaalkwa kuwatendea wenzetu yale ambayo tungependa tutendewe. Sheria hii tangu mwanzo inajulikana kama sheria ya dhahabu. Sheria ya dhahabu, huwa inatumiwa na watu katika kuongoza mfumo wa Maisha. Inamtaka mtu amtendee mwingine matendo ya haki, mazuri na ya amani akiamini kuwa siku moja naye atakuwa muhitaji wa huyo mtu atendewe matendo ya amani mazuri na ya upendo. Kwa kifupi ni sheria inayo mtaka mtu amtendee mwingine kama yeye angependa atendewe. Aina ya sheria ya dhahabu zipo tatu. Ya kwanza inasema kuwa watende wengine yale ambayo ungependa wao wakutende. Mfano kama unapenda watu wakuheshimu nawe unajukumu la kuwaheshimu, kuwapenda na kuwajali.

Aina ya pili ni kwamba katazo usiwatendee wengine yale ambayo hutaki wao wakutendee wewe. Kama hupendi kutukanwa usitukani, hupendi mchepuko usichepuke hupendi kuibiwa usiibe. Aina ya tatu ni katika baraka, yale yote unayowatakia wengine wayapate hata wewe utayapata, ukiwatakia mema nawe utayapata mema, ukiwatakia mabaya waumie, aachane katika ndoa yao nawe kama ni mabaya utayapata yakiwa mazuri utayapata. Mafundisho ya Yesu aligusa tamaduni za watu wengi na kujikumbusha mifumo yao ya Maisha. Kwa mfano Kile usichokipenda ufaniwe, usimfanyie mwenzako (Zoroaster), Epicetus wanasema masharti magumu tunayowawekea wengine tukubalii pia wao wakituwekea. John Stuart Mill Mwingereza anasema maadili yenye faida na mazuri kufanya kile ambacho ungependa ufanyiwe na kupenda mwingine kama unavyojipenda. Wahindi wakaendeleza ili kuleta radha katika Maisha yenye thamani kwa wote ni lazima kuwatendea watu kama unavyotaka utendewe. Usifanye jambo kama wewe mwenyewe ukifanyiwa linakuachia majeraha. 

Kanuni ya dhahabu usaidie kujenga na kukuza upendo na udugu wa kibinadamu
Kanuni ya dhahabu usaidie kujenga na kukuza upendo na udugu wa kibinadamu

Fadhila iliyo kuu ni kuepuka kitu ambacho hukipendi kufanyiwa. Zaidi usilipe mabaya hata kama umetendewa ubaya badala yake adhabu iliyo kuu ni kulipa jambo jema kwa yule aliye kuhumiza. Lipa uaminifu kwa aliyekosa uaminifu, lipa ukarimu kwa aliye kosa ukarimu kwako. Binadamu tunatabia ya kulaumu, kulalamika na kununa, Thales anasema epuka kuyatenda yale unayoyalaumu wanapotenda wengine. Wazee wenye hekima zao walisema usiwafanyie wengine yale yanayokuletea hasira wewe unapofanyiwa (Socratese). Sheria hii inagusa hadi sehemu zetu za kazi kama vile watendee wachini yako yale ungependa wao wakutendee, kama hupendi wanaochelewa kazini, hupendi janja janja, hupendi uongo katika mapato na matumizi basi wewe uwahi, kama hupendi mtu mvivu kazini basi wewe chapa kazi (Stoicism). Katika Maandiko Matakatifu, Walawi 19:18 Mpende Jirani yako kama nafsi yako. Mathayo 7:12 Mtende mwingine vile unavyo penda wao wakutendee, hii ni sheria ya manabii. Sheria ya dhahabu ni dira ya kimaisha katika kila jambo jema la maadili na utu wema.

Wanaomwamini Mungu na hata wasiomwamini Mungu wanaiishi hii sheria pasipo kuifahamu. Kwa wanaoongozwa na Maandiko Matakatifu wanatakiwa waiishi vizuri zaidi kwa kuwa wanaijua.  Tangu Agano la Kale tunasisitizwa kuwa kinacho kuchukiza wewe usimfanyie mwingine (Walawi 19:18). Yesu aliwaambia wafuasi wake watendee wengine yale ambayo ungependa utendewe.  Anatuambia hata sisi tuliobatizwa na kumfuasa Kristo kwa karibu. Msemo huo huo tunaupata katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki namba 1567 wakiitoa katika Agano la kale kitabu cha Walawi 19:34 Inawasisitiza Waisraeli wawatendee wasio Waisraeli yale ambayo wao wangetendewa, wawatendee wageni mema, mambo ya haki maana hata wao walikuwa wageni nchini Misri. Luka 6:31 watendee wengine vile unavyopenda wao wakutendee. Sheria hii sote tunaijua, tunaifahamu tumeisikia kwa sababu ni msemo maarufu katika bibilia lakini unaweza ukawa mgumu kuushi katika mazingira yetu, siyo wote tunayaweza hayo kuyashika. Tuombe neema ya Mungu ili tupate ujasili ya kuiishi Injili.

19 February 2022, 07:52