Mwenyezi Mungu anaita watu kutokana na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kutoka katika mazingira mbalimbali Mwenyezi Mungu anaita watu kutokana na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kutoka katika mazingira mbalimbali 

Mwenyezi Mungu Anaita Kwa Huruma na Upendo Ili Kutangaza Injili Kwa Watu Wote

Tunaalikwa na Kristo Yesu kwenda kufanya kazi ya Mungu kwa njia Ubatizo wetu. Tunabatizwa na tunatumwa kwenda kuwa wavuvi wa watu. Kwenda kuwahubiria na kuwashuhudia watu Habari njema kwa matendo na maneno pasipo kuogopa. Kwenda kuponya majeraha ya ndoa zilizo umizwa, kuwafariji wagonjwa. Huo ndio wito alopewa Simoni Petro kwenda akawe mvuvi wa watu.

Na Padre Nikas Kiuko, - Mahenge, Tanzania.

Injili ya Jumapili ya 5 ya Kipindi cha Mwaka C wa Kanisa, Lk 5:1-11, tunaalikwa kwenda kufanya kazi ya Mungu kwa njia Ubatizo wetu. Tunabatizwa na tunatumwa kwenda kuwa wavuvi wa watu. Kwenda kuwahubiria watu Habari njema kwa matendo na maneno pasipo kuogopa. Kwenda kuponya majeraha ya ndoa zilizo umizwa, kuwafariji wagonjwa. Huo ndio wito alopewa Simoni Petro kwenda akawe mvuvi wa watu. Mwinjili Luka namna yake alivyoiweka kuwaita mitume wa Yesu ni tofauti na injili Pacha tatu, ukisoma mwinjili Mattayo na mwinjili Marko wanasema Yesu amawateua wanafunzi wake akiwa anatembea kando ya ziwa Galilaya mara akanza kuwaita Simoni, Andrea, Yakobo na Yohane wamfuate (Mathayo 4:18-22) (Marko 1:16-20) Mwinjili Luka anatupa simulizi la Yesu anawateua wafuasi wake katika tukio la kuvua Samaki. Mwinjili Luka simulizi la kuwateua wafuasi wake wa linafanana kabisa na simulizi la Mwinjili Yohane baada ya ufufuko Yesu anakutana na wafuasi wake Ziwa Galilaya (Yohane 21:1-10) Wanaona utamburisho wa Yesu.

Tofauti ya Mwinjili Luka na Yohane kwamba Simoni Petro haikuwa mara ya kwanza kumwona Yesu kama Mwinjili Yohane anavyosema, bali Simoni Petro alishakutana na Yesu alipomponya mama mkwe wake (Luka 4:38-39). Simoni Petro amejaribu kuvua Samaki usiku kucha asipate kitu, kachoka, anasafisha zana za kazi, kwa vile amechoka anajiandaa kwenda kupumzika akalale, Yesu anaingia na kwenye Mtumbwi aende naye mpaka ufukweni na Petro anatii. Cha kusangaza Mwinjili Luka hajatuambia Yesu alifundisha nini makutano kwa ile asubuhi. Mkazo ulikuwa ni kupata wafuasi. Usiogope kwanzia sasa mtakakuwa wavuvi wa watu. Yesu anampa Petro wito mpya, utume Mungu amewapa kwa wokovu wa watu wote. Kuanzia hapo akabadirisha Maisha yao, mtazamo wao na kazi zao.  Hapa tunapata ujumbe jinsi Mungu anaita watu wa mzingira yetu, watu wa kawaida, hawakuwa na chaziada na jamii ya wavuvu, wao pia walikuwa wavuvi kama wavuvi wengine, wameitwa wakiwa na mapungufu yao nao wanajua kuwa hawakuwa wathamani. Haku mwambia akajiandae kisha aje, akamwambia tu usiogope. Na kumpa utume mpya.

Kristo anaita na kuwatuma watu kutangaza na kushuhudia Injili ya huruma na upendo.
Kristo anaita na kuwatuma watu kutangaza na kushuhudia Injili ya huruma na upendo.

Katika Maandiko Matakatifu tukisoma tunakuja na mang’amuzi kuwa dhambi, mapungufu, sio sababu ya kutoitika wito wa Mungu. Mungu anaita watu dhaifu na wenye mapungufu ili wakafanye kazi zake. Watu wanatambua mapungufu yao na hata kujiona hawafai. (Kutoka 3:10-12 wito wa Musa), (Isaiya 6:1-6 wito wa Isaya) Yeremia 1:6-8 wito wa Yeremia). Mungu hasubiri uanze kwanza kuwa mwema, kumbe hata hivyo katika madhaifu yako anakuita. Simoni Petro akaanza kubisha Tumevua usiku kucha hatukupata kitu. Nasi mara nyingi kwa kuangalia ugumu wa kazi tunaweza sema hatuwezi, hatufai ni dhaifu haina uharisia. Hatutaweza leta matunda mazuri. Kila siku Yesu anatuita tukafanye kazi yake, kwa vipaji vyetu, kwa kalama zetu. Kwa sakramenti ya Ubatizo sote tunaitwa tukatumie vipaji vyetu tulivyojaliwa na Mungu kwa ajili ya wengine, kushirikishana Habari Njema kwa watu wote, kwa matendo na maneno yetu. Tuepuke visingizio kwamba mimi nina kigugumizi, mimi ni mtoto au mimi siwezi kila mmoja ananafasi yake katika jamii. Usiogope , umebatizwa kaponye majera ya ndoa za watu zilizo jeruhiwa, kawaponye walioshindikana, katembelee wagonjwa, yatima, wajane na wazee, ili waonje huruma na upendo wa Mungu unaoganga na kuponya.

02 February 2022, 17:42