Austria:maaskofu wamesali kwa ajili ya amani na wakimbizi wa Ukraine
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ni jambo ambali liliwagusa sana wakati wa sala kwa ajili ya Ukraine ambapo maaskofu wa Baraza la Maaskofu nchini Austria walioungnika huko Matrei am Brenner katika mkutano wao na waliweza pia kufanya hija katika Monasteri ya Maria ya Waldrast, moja ya Madhabahu ya kufanya hija maarufu katika kilele cha Tirolo nchini humo. Kati ya washiriki walikuwapo Yuriy Kolasa, Mkuu wa waamini wa Ibada ya Mashairiki ambaye alisema kuwa wakati wao wako pamoja, makombora yanazidi kupiga majengo ya wakati katika maeneo mengi ya Ukraine.
Mapokezi ya watoto 50 viziwi
Ndani ya kikundi kilicho sindikizwa na Padre Kolasa, wakiwemo mama wa ukraine na watoto wao,na vijana hata watoto 50 viziwi ambao kwa sasa wamekaribishwa katika nyumba ya Marillac, katika jimbo katoliki la Innsbruck ambapo wote walishiriki. Akizungumza Padre aliyetoka huko Lviv chini Ukraine alisema, kuwa maelfu ya waathirika, wakiwemo wanawake, watoto na wazee kwa hakika wamepata janga la kibidadamu ambalo linazidi kuonegeza katika nchi na mamilioni ya watu wakikimbia, huku maelfu na maelfu mengine ya wanawake na watoto wanatafuta usalama hata nchini Austria. Padre huyo alizungumza kwa niaba ya wakimbizi kuhusiana na kuguswa kwa kina kwa mshikamano mkubwa na utashi wa msaada kutoka Austria. Akiwageukia maaskofu kwa kuwashukuru sana kwa mwaliko wa kusali pamoja alisema kwa hakika katika wakati huo wameweza kuwapatia familia za wakimbizi hadhi ya kibinadamu na furaha ya kuishi.
Tumaini kwa njia ya sala na wimbo
Katika wakati wa sala na maaskofu, kikundi kidogo cha Jumuiya ya Ukraine cha huko Innsbruck kilichoongozwa na Padre Kolasa, kiliimba wimbo wa Hymnos Akathistos: wimbo huo wa Maria wa Costantinopoli unaozingatiwa kuwa wa zamani sana ulimwenguni, kwa sababu umeimbwa kwa miaka zaidi ya 1200 katika utamaduni wa kibizantino mashariki, nchini Ukraine na hata Urusi, kama alivyoeleza Padre. Eneo liliochaguliwa kuadhimisha, siku hiyo ni madhabahu ya Bikira Maria waWaldrast, ambayo imekuwa ikufuatiliwa kwa hija hata na jumuiya ya Ukraine ambayo inaishi Innsbruck , madhabahu iliyoanza kutumika tangu 1899. Ni moja ya Monasteri ya kizamani sana na ya juu barani Ulaya, ambayo inajulikana kama “Altare kuu ya Tirolo”.