Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Patetico
Ratiba Podcast
Maombi kila sehemu ulimwenguni hata watoto wanasali kwa ajili ya amani Ukraine na ulimwengu mzima Maombi kila sehemu ulimwenguni hata watoto wanasali kwa ajili ya amani Ukraine na ulimwengu mzima 

Mapadre wa Kiorthodox Urusi:wito wa amani haupaswi kukataliwa

Maridhiano,msamaha,mazungumzo na utambuzi kamili ambao hauwezi kuwa nafasi ya vurugu ndiyo wiito kwa ajili ya amani kutoka katika kikundi cha Mapadre na masjemasi 233 wa Kanisa la Kiorhodox nchini Urusi wakiwatakia mema wanajeshi wa Urusi na Ukraine kurudi nyumbani kwa haraka.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kundi la mapadre na mashemasi 233 wa Kanisa la Kiorthodox la Urusi limezindua wito wa nguvu  kwa wale wote ambao wanataka uwepo mwisho wa vita huko Ukraine, unaofafanuliwa kama “mauaji ya kindugu” wakiomba upatanisho na kusitishwa kwa mapigano mara moja. RWito huo unakuja baada ya Dominika ya Hukumu ya Mwisho na katika juma linalotangulia Juma la Msamaha.  “Tunaomboleza mateso ambayo kaka na dada zetu nchini Ukraine wamepatwa nayo isivyostahili.” Kwa kukumbuka kuwa maisha ya kila mtu ni zawadi ya kipekee na ya Mungu, mapadre na mashemasi wanasisitiza jinsi ambavyo Hukumu ya ulimwengu inawasubiri wote.

Maombi kwa ajili ya Ukraine
Maombi kwa ajili ya Ukraine

“Hakuna mamlaka ya kidunia, hakuna daktari, hakuna mlinzi atatulinda kutokana na hukumu hii. Kujali wokovu wa kila mtu anayejiona kuwa mtoto wa Kanisa la Kiorthodox la Urusi, hatutaki  aingie hata mmjoja katika  hukumu hiyo, akibeba mzigo mzito wa laana za mama. Tukumbuke kwamba damu ya Kristo, iliyomwagwa na Mwokozi kwa ajili ya uzima wa ulimwengu, itapokelewa katika sakramenti ya Ushirika na wale wanaotoa maagizo ya mauaji, si kwa ajili ya uzima, bali kwa mateso ya milele”.

Matashi mema kwa wanajeshi wa Urusi na Ukraine

Katika wito wao, kuna hata wazo linalowageukia hata wale ambao wako kwenye mapambano, hasa wanajeshi. Matumaini yao ni kwa ajili ya warusi na waukraine wote ili waweze kurudi kwa haraka katika nyumba na familia zao. Wanaonesha huzuni sana kufikiria giza ambalo watoto wao na watoto wa ndugu zao nchini Urusi na Ukraine wanaweza kujazwa kwa ajili ya kuanza kwa upya kuwa marafiki kwa kuheshi na kupendana. Kwa njia hiyo wanaamini kuwa watu wa Ukraine wanapaswa wawe wa kwanza kuwa na uchaguzi kwa namna huru kwani sio chini ya macho ya bunduki, bila shinikizo kutoka Magharibi au Mashariki.

Wajumbe wa Ukraine wakiwa wanasali na kuimba huko Kaskazini mwa Uingerza
Wajumbe wa Ukraine wakiwa wanasali na kuimba huko Kaskazini mwa Uingerza

Wakiwa wanasubiri Dominika ya msamaha, mapadre na mashemasi 233 wa Kanisa Kiordhox nchini Urusi wanakumbuka kuwa milango ya mbinguni itakuwa imefunguliwa kwa wote hata wale wenye dhambi kubwa, ikiwa wataomba msamaha, kwa wale waliowadharau, wanatukana au kuua kwa mikono yao au kwa utashi wao. Hakuna lolote linaolonesha mbadala wa upatanisho wa pamoja. Katika  mtashi yao ya  kuanza kipindi cha Kwaresima, katika roho ya imani, matumaini na upendo, ujumbe umehitimishwa: “hakuna ombi lisilo la vurugu la kutaka amani na kukomesha vita likataliwe kwa nguvu na kuchukuliwa kuwa ni uvunjaji wa sheria, kwa sababu hii ndiyo amri ya kimungu: Heri wapatanishi”. Kwa hivyo mwaliko wao ni wa  mazungumzo, “kwa sababu uwezo  wa kumsikiliza mwingine tu  unaweza kutoa tumaini la njia ya kutoka kwenye shimo ambalo nchi zetu zimetupwa ndani ya siku chache".

03 March 2022, 14:40
Prev
January 2025
SuMoTuWeThFrSa
   1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031 
Next
February 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
232425262728