2022.03.17 Ukraine: Mtoto akimwaga baba yake. 2022.03.17 Ukraine: Mtoto akimwaga baba yake. 

Moyo safi wa Bikira Maria utashinda

Ujumbe wa Mama Yetu wa Fatima haukusudii kukidhi udadisi wa (apocalyptic)yaani kuhusu mwisho wa dunia,lakini unazindua wito wa dhati wa uongofu ili ubinadamu waokolewe kutokana na ubinafsi unaoharibu.Katika wakati huu wenye vita vikali, tarehe 25 Machi Papa ataweka wakfu nchi ya Urusi na Ukraine kwa Moyo Safi wa Maria.

Sergio Centofanti

 “Moyo Wangu Safi utashinda”: haya ni maneno ya Mama Yetu kwa wachungaji wadogo wa Fatima yaliyotamkwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Maneno ambayo yanatoa tumaini katikati ya kishindo cha vita. Tarehe 25 Machi, Papa Francisko ataziweka wakfu nchi mbili Urusi na Ukraine kwa Moyo Safi wa Bikira Maria. Jana aliomba sana kwa ajili ya amani: “Bwana Yesu, ambaye alikufa katika mikono ya mama yake kwenye bunker huko Kharkiv, utuhurumie ... Simamisha mkono wa Kaini!”. Upole wa maombi unashinda kiburi cha uovu. Lakini bado leo kuna vita vingi duniani, na mara nyingi husahauliwa: huko Siria, Yemen, Ethiopia ... Kwa Ukraine, jeshi la Kirussi linaendelea kuwapiga mabomu raia, wakimbizi, watu rahisi wanaopanga mstari kununua mkate, wanawapiga na kuharibu nyumba, hospitali, makanisa. Mwanamke mjamzito alikufa akiwa na mtoto wake katika shambulio la bomu katika hospitali ya watoto ya Mariupol. Vita husababisha mateso na uharibifu kila mahali.

Vituo vya kukaribishwa wakimbizi kutoka ukraine
Vituo vya kukaribishwa wakimbizi kutoka ukraine

Wengi wapo wanaomba amani. Katikati ya vita, maombi sio ya bure. Hatutawahi kujua ni kiasi gani sala rahisi, iliyo ndogo, ya kimya inaweza kufanya katika ulimwengu. Ni nguvu ya upendo, nguvu ya Roho ambayo inapuliza kila mahali na kubadilisha na kuongoa.  Kwa Mungu kila kitu kinawezekana, kinachohitajika ni ufa ndani ya moyo unaofunguka na kubadilisha mikono ya mauaji. Maombi hayambadilishi Mungu kwa nguvu ya maneno, lakini maombi hubadilisha mioyo na kuwaongoa kuelekea kwa Mungu ili hatimaye waweze kukaribisha zawadi zake. Zawadi ya Mungu ni Roho ambaye huponya ulimwengu wa chuki kwa upendo. Papa Francisko aliuliza: Je tunasali sala zetu namna gani katika vita? Maombi yenyewe huruhusu kugeuza kuwa matendo, upendo, imani tendaji. Sala, katika udhaifu wake, inaweza kuonekana kama kushindwa. Hata Mungu anaonekana kushindwa kwa Yesu pale msalabani: badala yake, pale pale alishinda chuki, uovu, kifo, na kuanzisha historia mpya, uumbaji mpya.

Inatia huzuni kuona baba anavyowaaga familia yake mara baada ya kuawasindikiza ili arudi vitani na wao wakimbie vita
Inatia huzuni kuona baba anavyowaaga familia yake mara baada ya kuawasindikiza ili arudi vitani na wao wakimbie vita

Ujumbe wa Fatima hautaki kukidhi udadisi wa ‘apocalyptic’ yani kuhusu mwisho wa dunia, bali unazindua wito wa dhati wa uongofu tu ili ubinadamu uokolewe kutokana na ubinafsi unaoharibu. Katika wakati huu mgumu tunasindikizwa na neno hili la kufariji la Maria: “Moyo Wangu Safi utashinda”. Mnamo mwaka wa 2000, wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafudisho Tanzu ya Kanisa, Kadinali Joseph Ratzinger, alieleza maana ya maneno haya kama ifuatavyo: “Moyo Wangu Safi utashinda”. Ina maana gani? Moyo ulio wazi kwa Mungu, uliotakaswa na tafakari ya Mungu, una nguvu kuliko bunduki na silaha za kila aina. Fiat ya Maria yaani ‘tazama mimi hapa’, neno la moyo wake, lilibadilisha historia ya ulimwengu, kwa sababu alianzisha Mwokozi katika ulimwengu huu, na kwa sababu shukrani kwa hiyo “Tazama mimi hapa” Mungu angeweza kuwa mwanadamu katika nafasi yetu na sasa anabaki hivyo milele. Yule mwovu ana nguvu katika ulimwengu huu, tunauona na kufanya uzoefu wa kuendelea; ana uwezo, kwa sababu uhuru wetu hujiruhusu daima kukengeushwa kutoka kwa Mungu. Lakini kwa vile Mungu mwenyewe ana moyo wa kibinadamu na hivyo amegeuza uhuru wa mwanadamu kuelekea wema, kuelekea kwa Mungu, uhuru kwa uovu hauna neno la mwisho tena. Tangu wakati huo neno hili limekuwa halali: “Mtakuwa na dhiki ulimwenguni, lakini jiaminini; Nimeushinda ulimwengu” (Yn16:33). Ujumbe wa Fatima unatualika kujikabidhi wenyewe kwa ahadi hii.

MOYO WANGU SAFI UTASHINDA
17 March 2022, 14:35