Nigeria:Maaskofu watoa wito wa amani na upatanisho
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kujenga amani kwa kusameheana na kuelimishana, huo ndiyo wito uliozinduliwa katika jumbe nyingi za Kwaresima kutoka kwa Maaskofu mbalimbali nchini Nigeria. “Viongozi wetu hapa kaskazini wanapaswa kufanya elimu kuwa kipaumbele badala ya kupigania madaraka”, alisema hayo Askofu Mkuu Matthew Man-Oso Ndagoso, wa jimbo kuu la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria, ambako vuguvugu kubwa lilizaliwa la Boko Haram ( ikiwa na maana Elimu ya Magharibi ni marufuku), na zaidi ni vurugu zinazoendelea kudhoofisha eneo hilo la nchi. Maasi hao wa Boko Haram Kaskazini-mashariki yanatokana na ukosefu wa elimu, eneo la kaskazini la nchi limeshikilia mamlaka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya nchi hii na kwama kuna sehemu ya Nigeria ambayo inapaswa kufurahia 'elimu,badala yake, amesema kwamba maaskofu ndiyo wanaonekaka kuwa wabaya zaidi katika karibu kila kitu, alishutumu Askofu Mkuu wa Kaduna.
Hata hivyo vurugu (za kimwili, za matusi na kisaikolojia) pia zinaongezeka kusini-mashariki mwa nchi kama alivyosema Askofu Peter Ebere Okpaleke, wa jimbo la Ekwulobia, Nigeria. Askofu wa jimbo hilo amebainisha kwamba “uchokozi na vitisho vimepanda zaidi na kuwa moja ya mtindo wa maisha na mbinu ya kuendelea kuishi. “Bado kiini cha wito wetu wa Kikristo ni kuingizwa kwa ustaarabu wa upendo” ameongeza na kwamba, kama Papa Mtakatifu Yohane Paulo II alivyosema. Askofu Ebere alithibitisha kuwa ni muhimu kupitia upya mtazamo wao kuhusu vurugu kwa upande mmoja, upatanisho, kuheshimiana, ukarimu na mshikamano kwa upande mwingine kuwa na uongofu unaanzia kujidhihirisha katika lugha inayotumika kwa sababu maneno ni madirisha ya mioyo ya kila mtu.
Naye Askofu Mkuu wa Lagos Alfred Adewale Martins, wakati wa kutoa tafakari yake ya kwanza ya Kwaresima iliyopewa mada: “Safari ya kurudi”, katika tukio la Jumatano ya Majivu, aliwaalika wanasiasa na wahubiri wa uwongo kutubu. Askofu mkuu Martins pia aliwataka viongozi wa serikali wafisadi, na wale wanaofanya uhalifu wa kikatili na utekaji nyara, watubu kwa kuwa ni wakati wao. Na hatimaye, Askofu Mkuu aliwaalika waamini kuombea amani nchini Ukraine.