Ukraine,Pizzaballa:Ushiriki wa Mashariki ya Kati katika mzozo ni udanganyifu
Na Angella Rwezaula - Vatican
Patriaki wa Kilatino wa Yerusalem, Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, katika mahojiano na Tv2000, ya Baraza la Maaskofu Italia kuhusu watu wa kujitolea 16,000 kutoka Mashariki ya Kati ambao inasadikika walionesha nia yao ya kuandikishwa katika Donbass ili kuweza kupigana pamoja na jamhuri zinazojiita kujitenga za Donetsk na Lugansk, amesema : “Ninatumaini si kweli bali ni mzaha tu. Sote tunajua vyema kwamba katika maeneo ya vita, hasa Iraq na Siria, bado kuna wapiganaji wengi wanaosubiri, wameegeshwa hapo. Ninatumaini sivyo hivyo kwa sababu itakuwa ni ongezeko lisiloeleweka na zaidi ya yote na pia jaribio la kuhusisha Mashariki ya Kati”.
Upatanishi wa Bennet?
Lipo suala kubwa sana la kutokuaminiana Mashariki ya Kati aliongeza Patriaki Pizzaballa kuwa daima wanajaribu kuihusisha kidogo katika kila kitu moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Lakini hali ya Israeli sio rahisi kwa sababu ina uhusiano mkubwa na Urusi. “Hapa Israeli kuna Warusi wengi lakini pia kuna uhusiano na Ukraine kwa sababu kuna Waukraine wengi hapa pia”. Kuhusiana na suala la upatanisho amesema “Inaeleweka kuwa Bennet anataka kujionesha kuwa mpatanishi kati ya pande hizo mbili, hata hivyo nikiamini kuwa haitakuwa rahisi kwa sababu hali ya kutoaminiana sasa ni kubwa sana kuweza kufanikisha lolote. Ninatumaini kwamba sababu itatawala, hata kama haitaonekana hivyo kwa sababu tunaona matokeo ya hali hiyo hapa Mashariki ya Kati ni maafa kamili ya uaminifu kati ya watu na karibu kutowezekana kujenga upya uhusiano kati ya jamii”, alihitimisha Patriaki Pizzaballa.