Tafuta

Baba Mtakatifu akitembelewa na Rais wa Zambia Baba Mtakatifu akitembelewa na Rais wa Zambia 

Zambia:Maaskofu washauri majimbo kuhakikisha ulinzi wa watoto

Maaskofu nchini Zambia wanahimiza majimbo ili nchi nzima iweze kuhakikishwa na kulinda watoto na watu walio katika mazingira magumu.Hayo yalielezwa na Padre Mukosa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu akizungumza hayo kwa niaba ya maaskofu,atika fursa ya kufunga Semina ya siku nne kuhusu ulinzi wa watoto,kwa wahusika wa majimbo wanaojikita katika masuala ya ulinzi wa watoto.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Majimbo katoliki ya nchi lazima yakikishe kuwa watoto wanawelewa mchakato wa Sinodi ili waweze kuhakikishwa wao ushiriki wa maana. Amesema hayo Fidelis Hamweemba, mhusika wa ulinzi wa Watoto wa Baraza la Maaskofu nchini Zambia (ZCCB), katika wito wake katika muktadha wa kuwahusisha watoto katika mchakato wa Sinodi ya Kanisa inayoendelea.

Miundo inayofaa kwa ajili ya kulinda watoto

Naye Padre Francis Mukosa, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Zambia, ameshauri kwamba ni muhimu kuwa upamoja unajikita juu ya uundaji wa miundo inayofaa kwa ajili ya kulinda utoto katika majimbo yao katoliki. Na amebainisha kwamba wote wanapaswa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha kuwa Zambia inakuwa salama kwa ajili ya watoto na watu walio katika mazingira magumu.

Kusaidia watoto na watu wali katika mazingira magumu

Padre Mukosa amezungumza hayo kwa niaba ya maaskofu, katika fursa ya kufunga Semina ya siku nne kuhusu ulinzi wa watoto kwa wahusika wa majimbo wanaojikita katika masuala ya ulinzi wa watoto. Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zambia (ZCCB) limebainisha juu ya jitihada ya ulinzi wa haki za watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu kwa njaia ya siasa iliyozinduliwa mnamo 2017 na amewatia moto katika mchakato wa sheria ya serikali inayofaa katika kukabiliana na haki za binadamu.

16 March 2022, 15:02