Tafuta

Mafuriko yaliua watu zaidi ya 448 nchini Afrika Kusini hivi karibuni katika Fukwe za Durban na maeneo yanayozunguka. Mafuriko yaliua watu zaidi ya 448 nchini Afrika Kusini hivi karibuni katika Fukwe za Durban na maeneo yanayozunguka. 

Afrika Kusini:Hitaji la ukaribu wa watu waathirika wa mafuriko

Zaidi ya Juma mmoja tangu mafuriko yaikumbe Afrika Kusini,nchi hiyo inajaribu kupambana kusaidia watu ambao wanateseka.Caritas nchini humo pamoja na mashirikia mengine yanaendelea kutoa msaada kwa waliopoteza yote.Hayo yamethibitishwa kwa Vatican News na Mratibu wa Caritas Afrika Kusini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wahanga wa mafuriko nchini Afrika Kusini wamezungumzia juu ya mvua ya kutisha na ambayo imefagilia mbali nyumba, madaraja na barabara kwa kuwaua watu karibia 480 na kuwacha maelfu na maelfu bila kuwa na makazi. Kwa karibu masaa mawili tu kati ya tarehe 11 na 12 Aprili, mvua kubwa ilinyesha utafikiri ni ya mwaka mzima. Mafurikio yalikumba wilaya ya KwaZulu-Natal, ambayo inajumuisha mji ulioko pwani wa Durban. Hata Baba Mtakatifu Francisko aliwakumbuka watu wa Afrika Kusini wakati wa kutoa  baraka yake ya Urbi et Orbi ya Pasaka, akiomba kuwa watu hao wasikose kuwaombea na kuwa na mshikamano kwa watu hao  wa Afrika Kusini Mashariki, ambao wamekumbwa na mafuriko makali yalitokana na mvua kubwa sana.

Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini
Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini

Zaidi ya watu elfu nne wamesabambatishwa na nyumba elfu nene kuharibika kabisa

Madhara yaliyotokana na mafuriko hayo hayasemekani, kwa mujibu wa maelezo ya Sr. Maria de Lurdes Rissini, mmisionari wa Scalabrini nchini Afrika Kusini tangu 2011 na tangu mnamo 2018 ni Mratibu wa Kitaifa wa Caritas Afrika Kusini. Akizungumza na Vatican News, ameelezea madhara makubwa ya miundo mbinu katika maeneo ya kipigo hicho ambacho kimefagia nyumbana barabara,  na kwa sasa hakuna maji ya kunywa na umeme. Ni shule 78 ambazo zimepata kipigo. Na zaidi ya watu mia 4elfu wamesambaratishwa,  wakati nyumba elfu nne zimeharibika kabisa na zaidi ya elfu nane kupata maafa makubwa. Hivi karibuni kwa njia ya nguvu kazi iliyoandaliwa na Caritas, wamekutana na zaidi ya watu wa kujitolea 50 na wamefanya kazi katika maeneo yaliyoharibiwa na mafuriko. Walishirikishana uzoefu mbali mbali na jumuiya hasa familia nyingi zilizokumbwa na mafuriko. Ushuhuda wao ni wa kutisha amesema Sr Maria.

Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini
Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini

Watu 70 bado hawajapatikana

Uchungu mkubwa zaidi ni ule wa kupoteza familia nzima za ndugu. Nyumba ambazo zilichukuliwa na mito na bahari na watu wakiwemo ndani. Wazazi ambao walikuwa wamebeba watoto wao wakikimbia lakini hawakuweza kuokoka. Ni hali ya kuogopesha na kuna haja ya kupewa  msaada wa kibinadamu kwa hali zozote zile na si tu katika ujenzi wa majengo. Moja ya matizo makubwa katika eneo hilo ni ujenzi wa nyumba katika ardhi dhaifu, ambapo zingepaswa kujengwa katika ardhi ngumu yenye uwezekano, amesisitiza Sr Maria. Na hii ndiyo moja ya changamoto kubwa ya kukabiliana yao na kwamba watahakikisha wanaona ni jinsi gani ya kuweza kujenga kwa upya nyumba mpya. Lakini kwa wakati huu na kulingana na tamaduni na imani za kimila, familia nyingi ziko bado zinaomboleza kwa ajili ya wapendwa wao, wakisubiri ardhi zikauke ili wapate kufanya maziko rasmi. Kuna watu zaidi ya 70 ambao bado hawajapatikana na wakati vifo vya watu kwa sasa ni 448. Ni upotezaji wa maisha ya watu, thamani na uhusiano kwa kiasi kikubwa.

Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini
Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini

Kuna haja ya kutengeneza miundo mbinu stahiki ya ujenzi wa nyumba

Kwa mujibu wa Sr. Maria ameeleza jinsi ambavyo watu wa Afrika kusini walivyo karibu sana na kusaidiana kwa karibu na ndiyo uzuri wa mshikamano ambao unaendelea zaidi kuonekana kati ya watu na madhehebu mbali mbali. Caritas Afrika Kusini tangu mwanzo imekuwapo karibu, kwani walituma fedha kununua mambo muhimu na ya lazima kama vile chakula na mablanketi na  sasa kuna makampuni na watu ambao wanaendelea kuchangia.  Caritas Afrika Kusini iko inakusanya majina yote ya Jumuiya ambayo kuna familia ambazo zimeguswa ili ziweze kusaidiwa.  Na kwa mujibu wa maelezo ya Sr, Maria ni kwamba kila mtu aliyepotea au atakuwa amefariki atalipwa fidiwa kwa kiasi flani zilizotolewa na kampuni moja katoliki. Na kwa wakati huo huo nchi inaendelea kudanya kampeni mbali mbali hasa kwa upande wa kifedha na nyingine zinazohusiana na hukusanyaji wa chakula, nguo na mablanketi. Kardinali Wilfred Napier, Askofu Mkuu Mstaafu wa Durban, ametoa maoni yake kuwa kile ambacho kinaendelea kuwa wazi ni kwamba haya ni majanha ya kiasili makubwa ambayo hayajawahi kutoke huko KwaZulu Natal  katika historia na kwamba matokeo yake mahitaji yanaendelea kila siku kushangaza zaidi. Ikumbukwe mara baada ya kuzungumza mnamo tarehe 18 Aprili 2022 akitangaza dharura ya kitaifa, Rais wa wa Sudan Kusini Bwana Cyril Ramaphosa,  amezungumza tena Jumanne tarehe 26 Aprili usiku.

Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini
Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini
27 April 2022, 10:56