Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
MISA KWA KILATINI: MUBASHARA
Ratiba Podcast
Mgogoro mbaye wa kati ya Urussi na Ukraine. Mgogoro mbaye wa kati ya Urussi na Ukraine. 

Comece/Cec:Wito wa makanisa ya Ulaya ili kusitisha moto wa silaha nchini Ukraine

Marais wa kanisa Katoliki na Kiinjili Barani Ulaya wameomba marais wa nchi mbili za migogoro kusimamisha vita ili kuruhusu wakristo washerekehe Pasaka kwa utulivu na amani.Wameunga mkono wito wa Papa Francisko mnamo 10 Aprili na pia kutoa wito pia umetolewa kwa Patriaki Moscow Kirill.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Zimebaki siku chake wakristo ulimwenguni wayakumbuke Mateso kifo na   hatimaye kuadhimisha Ufufuko wa Bwana Yesu Kristo. Sherehe hizi za Pasaka ni moyo wa  waamini wakristo , kiini cha mwaka wa liturujia. Ni kiini cha maisha ya waamini, kwa maana hiyo tunaomba kusimamisha moto huo wa mgogoro kati ya nchi zenu mbili ili kuwapa waamini wa Urussi na Ukraine, Kaka na dada katika Kristo uwezekano wa kuadhimisha Pasaka kwa amani na hadhi.  Kuzima vita  vita hiyo  kungewezesha wazalendo wote na kuwapa uwezekano kidogo kutulia kutokana na ukosefu wa uhakika wa usalama wa  maisha ya ndugu zao, wapendwa ambao wanaendelea kupambana katika migoro au wamekumbwa kwa namna moja.

Vita nchini Ukraine na Urussi
Vita nchini Ukraine na Urussi

Hayo ndiyo yaliyomo kwenye barua ya pamoja ya Kardinali Jean-Claude Hollerich, Ris wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Ulaya (Comece) na Mchungaji Christian Krieger, Rais wa Baraza la makanisa ya Ulaya (Cec) wakiwatumia viongozi wa Serikali ya Urussi na Ukraine Putin na Zelensky, wakiomba kusitishwa kwa silaha katika Nchi ya Mashariki mwa Ulaya, kuanzia saa sita usiku tarehe 17 Aprili hadi Usiku wa tarehe 24 Aprili ili kuwaruhusu wakristo wa tamaduni zpte za Mashariki na magharibi waweza kuishi  Pasaka Takatifu kwa amani na hadhi. Wito huo huo unafanya mwangwi au kuunga mkono wito uliotolewa na Papa Francisko mnamo Dominika tarehe 10 Aprili 2022 wakati wa sala ya Malaika wa Bwana ambayo ilikuwa ni Dominika ya Matawi katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Vita nchini Ukraine na Urussi
Vita nchini Ukraine na Urussi

Baba Mtakatifu Francisko alisema: “Silaha ziwekwe chini! Ianzishwe mchakato wa Pasaka; lakini sio kupakia tena silaha na kuanza tena kupigana, hapana! Makubaliano ya kufikia amani, kupitia njia ya azungumzo ya kweli, kuwa pia tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya manufaa ya watu”. Mwaka huu Pasaka ya kigregoriani ni tarehe 17 Aprili Ulaya Mashariki, na wakati Ulaya ya Magharibi wanaofuata kalenda ya kijuliani wataadhimisha tarehe 24 Aprili 2022 na ndiyo maana maaskofu wa Ulaya wanaomba kusitisha vizingiti hivyo kwa kipindi kizima cha tarehe ziliotajwa.

Maaskofu wanapanua ujumbe wao kwa viongozi wote wa Ulaya lakini pia sehemu nyingine ya barua ya tarehe 11 Aprili, Kardinali Hollerich na Mchungaji Christian Krieger wanatoa wito moja kwa moja kwa Patriaki wa Kiorthodox wa Moscow, Urussi, Kirill, ili aweze kushirikiana katika kuunda dirisha la amani mahali ambapo pasisike tena vifo, mabomu na milipuko ya mizinga. “Tunakuandikia kwa kuuomba msaada wako kwa umma katika mpango huu. Kwa kufanya hivyo unaweza kuonesha nini maana ya umuhimu wa tarehe hizi kwa wakristo wa Urussi na Ukraine, kaka na dada katika Kristo… Baada ya miaka miwili ambayo Pasaka imeadhimishwa kwa vizuizi vikali kwa sababu ya janga la uviko, ni matumaini kwa msaada wako, unaweza kuunda hali ambayo inaruhusu sherehe hizi katika kipindi muhimu kwa wakristo”.

14 Aprili 2022, 15:09
Prev
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031     
Next
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930