Tafuta

03-04-2022 Askofu Mkuu Scicluna mbele ya Papa wakati wa kukabidhiana zawadi mara baada ya Misa katika huko Floriana katika ziara ya kitume ya Papa nchini Malta na Gozo. 03-04-2022 Askofu Mkuu Scicluna mbele ya Papa wakati wa kukabidhiana zawadi mara baada ya Misa katika huko Floriana katika ziara ya kitume ya Papa nchini Malta na Gozo. 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Scicluna,changamoto itazaa matunda

Makaribisho,unjilishaji,furaha na ubinadamu,ndiyo maneno muhimu sana ya Papa katika ziara yake ya kitume huko Malta na Gozo ambayo yanaweza kuwa ufunguo mzuri zaidi na uwepo wake ukitoa matumaini na neema katika Roho.Amethibitisha hayo Askofu Mkuu Scicluna wa Malta katika mahojiano na Vatican News kuhusiana na ziara ya kitume ya Papa Francisko,Aprili 2-3,2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maneno, ishara, mikutano ya Papa kwa watu wa Malta na Gozo yameacha nyayo ya kina na hisia yenye nguvu ya uponyaji. Ndivyo amethibitisha Askofu Mkuu Charles Jude Scicluna mara baada ya mkutano wa kina wa Papa Francisko aliyetembelea Kisiwa hicho kikubwa cha Kimediteranea katika Hija ya 36 ya kitume 2-3 Aprili 2022. Askofu Mkuu wa Malta amesema kwa njia ya maneno yake yamegusa na kuwasha joto na furaha ambayp imeonekana na kusindikizwa na Mfhasi wa Mtume Petro katika hija yake ya kitume kwenye nyayo za Mtakatifu Paulo, Mtume wa Watu. Askofu Mkuu Scicluna amethibitisha anavyokumbuka ile hisia ya nguvu ya watu ambao wamepata uzoefu wa kusikia neno lake na kupokea ishata zake, uwezeokano wao wa upendo na urithi mkubwa ambao kwao unabaki kuwa uwajibikaji.

Misa ya Papa huko Malta
Misa ya Papa huko Malta

Kwa sas amara baada ya Papa kuondoka wanapsswa kufanya mbegu hiyo ikue ambayo Bwana, kwa huruma yake amepanda katika Kanisa lao ambalo ni Malta na Gozo. Askofu Mkuu amesimulia jambo ambalo limemgusa zaidi katika ziara ya Papa Francisko kwamba ni mambo emngi sana, ambayo ni vigumu kuelezea. Lakini anakumbuka mara tu Papa alipotua uwanja wa ndege jambo la kwanza alimwomba maombezi ya uponywaji kimwili na kiroho kwa wote kwa sababu ndani ya moyo wake alikuwa amejaa maombi mengi ya watu wengi. Na alimweleza kuwa kama angeweza kumpatia zawadi hiyo ya uponyaji kwa sababu wanahitaji. Na kwa hakika uhusiano na Papa na watu, mikumbatia ya watu na Papa imepelekea hisia hizo za nguvu katika upatanisho, usiolezeka, lakini pia shukrani kwa uwepo na neema ya nguvu ya Roho Mtakatifu.

Misa ya Papa huko Malta
Misa ya Papa huko Malta

Kile ambacho kilikuwa kinampa nguvu Askofu Mkuu Scicluna ni ile furaha ya nyuso za watu wengi wakimsalimia Papa katika njia. Barabara za Kisiwa cha Malta ma Gozo kulikuwa na furaha kwa wazee, kwa wagonjwa, vijana, watoto na  furaha ambayo inametolewa kwa njia ya roho Mtakatifu. Kuhusiana na mada ya uponyaji ambayo inahusiana na makaribisho ni katika kutazama historia iliyomo kwenye kitabu cha Matendo ya mmitume ambapo Mtume Paulo alipokaribishwa huko Malta, jambo la upyaji linaonekana bayana. Askofu Mkuu Scicluna amebainisha kuwa awali ya yote, Papa alikaribishwa kwa joto la kibinadamu maalum ambalo ni jibu la joto la kiroho kwa mchungaji mkuu ambaye ni Papa. Na makaribisho kama alivyo sema yeye mwenyewe kwenye mahubiri ya Domikoa tarehe 3 Aprili 2022 ni kwamba hayaji hivi kwa urahisi. Makaribisho yana gharama, yanahitaji uwajibikaji, jitihada na uvumilivu na hivyo ndiyo chanagamoto ambayo wao kama Kanisa la Malta wanapaswa kufanya hivyo kwa sababu ndiyo hata maana ya ukristo.

Misa ya Papa huko Malta
Misa ya Papa huko Malta

Askofu Mkuu amesema, kwa sasa wao wanajiandaa na Pasaka takatifu, na uzoefu wao waliuoishi na Papa katika ardhi ya Malta katika moyo wa mediteranea, inawafanya waweze kutoa matunda ya Roho ya Mfufuka ambayo haiwezi kuondolewa na yeyote. Furaha ya uinjilishaji ndiyo wanapaswa kuiishi katika vipindi vyote. Baba Mtakatifu alirudia mara nyingi katika tafakari yake kwenye madhabahu ya Bikira Maria huko Ta Pinu, Gozo, na kukumbusha kuwa ili kuwa mkristo haina maana ya kushikilia wakati uliopita. Na kwa maana hiyo Askofu Mkuu Sccluna amesisistiza kuwa mara moja aliweza kuwambia ndugu zake maaskofu kuwa katika hilo wao wako tayari na mpango wa kichungaji wa wakati ujao, wa kutangaza Habari Njema, kwa ushuhuda wa amani ya kina ambayo haikimbii, isio tambua msalaba, lakini inayobeba msalaba kuupeleka katika kushindwa kwa maisha, kwa utulivu na hata kwa furaha.

Misa ya Papa huko Malta
Misa ya Papa huko Malta

Na hatimaye Askofu Mkuu wa Malta akifafanua kile ambaco Baba Mtakatifu Francisko amekuwa na umakini wa ulimwengu hasa kwa kutaja ajali iliyotokea huko Libya ambayo walinusurikawatu 9 tu na wengine wakafa baharini, na juu ya suala la vita vya ukraine. Askofu Mkuu amesisitiza kuwa hakika maneno yake yanagusa sana, si tu katika dhamiri ya kijamii ya Malta lakini hata dhamiri ya Nchi zote ambazo zinatazama Bahari ya Mediteranea na Ulaya, kwa sababu ni wito wa kuwa na ustaarabu wa kibinadamu. Baba Mtakatifu Francisko alisema wazi kwamba “Ikiwa tunaacha kaka na dada zetu wanakuwa waathirika wa ajali, hata sisi tu waathirika wa ajali ya ustaarabu wenyewe, kwa sababu utakosa ursataabu ambao unatufanya kuwa kile tulicho sisi wenyewe.”

05 April 2022, 15:46