Italia,Comigi:Shauku ya vijana kutembea njia za ulimwengu ili kutangaza Injili
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Giovanni Rocca, Katibu wa Vijana wamisionari kitaifa wakati wa kuhitimisha Kongamamo la Kimisionari la vijana (COMIGI) lililofanyika huko Sacrofano, Roma kuanzia tarehe 22-25 Aprili 2022 na katika fursa hiyo hata kuweza kukutana na Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 23 Aprili, alisema: “Mwanzoni mwa kongamano hili, Baba Mtakatifu Francisko alitupatia vitenzi vitatu ambavyo tumevitafakari katika siku hizi na akatutaka tuvirudie: simama, tunza na shuhudia kwa kuzungumza na maisha yako. Lakini sisi pia tumetoa kitu kwa Baba Mtakatifu, shauku isiyozuilika ya kutembea katika njia za ulimwengu kutangaza Injili”. Kwa hakika hawa walikuwa ni vijana zaidi ya vijana mia tatu kutoka Majimbo ya Italia na ambao walikutanika kwa pamoja. Rocca aliendelea kusema kwamba: “Jumuiya zetu zinaogopa kwa sababu zinahofu kwamba kwa kukimbia tunaweza kufika mbali hata tusirudi tena. Lakini sisi tumejitolea na ikiwa watatutafuta watatupata katika viunga vya ubinadamu dhaifu na ilikuwa pia ni ahadi ya vijana wa majimbo yote ambao wamekuja kusherehekea miaka 50 ya Harakati ya Wamisionari Vijana kwa kuthibitisha tena matendo yao ya kimisionari.
Vijana wasiwe na hofu ya majeraha
Vijana wanapaswa kuwa wamisionari miongoni mwa watu wasio na uwezo na miongoni mwa maskini, kama Kanisa linavyofanya na ambalo wanaliamini. Kanisa ambalo ni Maskini na kuvunjika, lakini lililojaa utajiri wa kukutana, alisema Rocca. Ni kweli, si rahisi kutembea katika Kanisa hilo, kwa sababu pia wao vijana wanajua nini au watafanya nini au mbaya zaidi lakini wasiende kusikiliza kwa mradi tu. Kongamano la kimisionari kwa vijana liliongozwa na mada:“Utume unaanza na wakati uliopita. Na kitenzi muhimu cha simama kutoka katika Injili ya Luka “Kijana nakuambia simama kiliongoza watoa mada katika fursa hiyo ya Kongamano la vijana wa Kimisionari. Kati ya waliotoa shuhuda alikuwa ni Padre Crescione, Mmisionari wa Pime huko Marekani ambaye aliwasisitizia vijana wasiwe na hofu ya majeraha yao na udhaifu wao badala yake wayasikilize. Wao hawaombwi kuamka peke yao, kwa sababu Yesu yuko pamoja nao.
Mara nyingi vikwazo vya kimwili vinapata nguvu
Akiendelea na ufafanuzi huo alitoa mfano halisi wa ujumbe huo, hasa kwa kutazama filamu ndogo unayohusu tamasha la kipepeo, huku akionesha vikwazo vya kimwili ambavyo havijahukumiwa. Badala yake vinapopata nguvu husimama. Vijana walishauliwa na wataalimungu wengine waliwaomba kusaidia wale ambao wanawazunguka. Yesu alitambua wakati muafaka na kuamka kuanza safari, lakini muda huo ulikuwa ubatizo wake. Na tangu wakati huo maisha yake hayakuwa yale yale bali yalibadilika. Padre Crescione alisimulia utume wake katika sehemu ya Kaskazini mwa dunia kwamba “karibu yake hata katika nchi tajiri ya Marekani kuna watu wengi sana ambao wanatatizika kuandaa mlo na wanahitaji kila kitu ili kuishi. Pia alifikiria maelfu ya ubaguzi wa watu wanaoteseka. Na aliwatakia wao ili weweze mara moja kusimama kidete na kusaidia wengine kuamka.
Kwenda njia za ulimwengu kushuhudia Injili
Kongamano la kimisionari la vijana limeandaliwa na Mfuko wa Missio la Baraza la Maaskofu Italia (CEI) kwa kuhitimishwa Jumatatu tarehe 25 Aprili 2022 ambapo kwa siku tatu wamewezesha kuishi vipindi vya kina vya kushirikishana mada tatu ya kusimama, kutunza mwingine na hatimaye kushuhudia kwa pamoja na ambavyo ni muhimu kwa sababu ya kwenda ulimwengu kushuhudia Injili. Vijana zaidi ya 300 waliohudhuria Kongamano hiko huko Sacrofano walitoka majimbo yote ya Italia na katika mikoa ya Puglia, Campania, Basilicata, Triveneto, Emilia Romagna, ilikuwa ni kati ya mikoa yenye uwakilishi zaidi. Miongoni mwa vijana pia kulikuwa na familia kadhaa za wamisionari, kama ile ya Fabio na Giulia Cento pamoja na watoto wao wanne, kwenye utume wa kimizsiona huko Piombino, Toscana ambapo wanasimamia nyumba ya familia. Na ile ya Alex Zappalà na mkewe na mtoto mdogo Lorenzo. Utume wao unaitwa: “Kilometa sifuri” ambapo walsema kwamba walikuwa haou kwa ajili ya kupumua pumzi ya umisionari na kujiweka katika uhusiano wake.