Tafuta

 Ndani ya Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu huko Yerusalemu. Ndani ya Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu huko Yerusalemu. 

Nchi Takatifu:Ruhusu kwa Wakristo 722 wa Gaza kwenda Yerusalemu

Katika fursa ya Maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu ya Mateso,kifo na ufufuko wa Bwana,Mamlaka ya Israeli imetoa ruhusu kwa wakristo wa Ukanda wa Gaza kushiriki Maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.Kwa maana hiyo Wakristo Wapelestina wameanza kuingia nchi Takatifu ili kusheherekea na wakristo wengine kutoka pande zote za ulimwengu katika tukio kuu la ukombozi wa mwanadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwaka huu wakristo 722 wa kipalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza, wataweza kusheherekea Pasaka ya Bwana jijini Yerusalemu, katika maeneo ambayo yameona mateso, kifo na ufufuko wa Kristo. Amesema hayo Padre Gabriel Romanelli, Paroko wa Parokia Katoliki ya Familia Takatifu wa huko Gaza akizungumza na Shirika la Habari za Kimisionari Fides, na kupongeza Mamlaka ya Israeli kwa kuwezesha kutoa ruhusa ya idadi kubwa ili kufika Mji Mtakatifu mwaka huu. Kwa maana hiyo Wabatizwa wa Ukanda wa Gaza, katika fursa ya Siku Kuu ya Juma Kuu Takatifu na Ufufuko wa Bwana wameanza kufika Nchi Takatifu.

Wakristo 722 wameruhusiwa 

Huo ni Ukanda wa Gaza, mahali ambapo wanaishi zidi ya milioni moja na laki nane ya wapalestina, wakristo karibia ni 1,070, ambao karibu ni wa Kanisa la Kigiriki Kiorthodox. Wakatoliki ni 133. Kama Parokia iliwakilisha orodha ya maombi kwa mujibu wa Padre Gabriel, kuhani wa Taasisi ya Neno lilifanyika Mwili, lakini hadi sasa wameruhusiwa watu 722. Hata hivyo ni idadi kubwa hiyo amesisitiza. Watu wengi wana furaha hata wote wanaowakaribisha. Parokia yao ya kilatini imeruhisiwa na baadhi wameanza kusafiri tayari. Kwa maana hiyo Juma takatifu la maahimisho katika parokia yao itakuwa na waamini wachache sana lakini kuwa na furahi kuona kaka na dada zao wanaweza kushiriki siku kuu ya kufufuka kwa Kristo katika Mji Mtakatifu, pamoja na wakristo wengine weni kutoka ulimwenguni.

Ishara nyanya katika kipindi hiki

Paroko huyo wa Gaza, amefurahi hata kwa sababu mwaka huu, ruhusa ilitolewa hata kwa idadi ya familia, na kwa maana hiyo familia nyingi kuweza kuishi pamoja katika Juma hili Takatifu huko Yerusalemu. Miaka mingine haikuwa hivyo, wakati mwingine walikuwa wanatoa ruhusa labda kwa baba na sio mke au watoto na wala wazazi wao kwa pamoja. Na zaidi ruhusa zilizotolewa zimewekwa muda mrefu wa kukaa.  Hizi zote ni ishara chanya ansisitiza Padre huyo, na kwamba mtindo huo unaweza kuboreshwa hivyo na kuendelea. Wakatoliki wa kilatini huko Gaza, wanaadhimisha Pasaka  mnamo Dominika tarehe 17 Aprili. Na kwa Makanisa mengine ya Mashariki wanafuata Kalenda ya Juliani, mwaka huu Pasaka yao itaadhimishwa Juma litakalofuata, tarehe 24 Aprili 2022.

Mabadiliko yamekuwapo 

Kabla ya vizingiti vilivyosababishwa na janga la UVIKO, ruhusu kutoka Mamlaka ya Israeli kwa wakristo wa Ukanda wa Gaza kusheherekea Siku Kuu kubwa ya Kuzaliwa kwa Bwana na Pasaka ya Maeneo Matakatifu ya Yerusalemu, Betlehemu na Nazareth ilikuwa imeibua malalamiko na kukatana tamaa. Mnamo 2019, ruhusu zilikuwa zimetolewa kidogo kwa ajili ya maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Bwana, wakati wengi walikuwa tayari wamekata tamaa ya kwenda huko. Katika fursa hiyo, ruhusu zilitolewa kwa mtu aliyekuwa na umri zaidi ya miaka 55. Mnamo mwezi Desemba 2015 hapakuwapo na ruhusu yoyote kwa wakristo wa Ukanda wa Gaza kwenda  kuadhimisha Siku Kuu za Kuzaliwa kwa Bwana huko Yerusalemu au Betlehemu waliokuwa na umri wa miaka kuanzia 12 hadi 30.

13 April 2022, 15:41