Uvamizi wa Kirussi nchini Ukraine unaendele na mabomu kuharibu miji. Uvamizi wa Kirussi nchini Ukraine unaendele na mabomu kuharibu miji. 

Patriaki Bartolomeo:Ubinadamu ni mshindi mkuu wa Vita

Katika Ujumbe wake wa Pasaka kwa Makanisa ya Mashariki,Patriaki wa Kiekumene wa Constantinopoli ameomba amani na haki na kukemea ukimya usiofikirika wa Wakristo mbele ya udhalilishaji wa utu wa mwanadamu.Patriaki amesema ni wazo tu la Kikristo ambalo linaweza kugeuza ukosefu wa haki.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Ujumbe wa Patriaki wa Kiekumene Bartolomeo I katika fursa ya Pasaka ya Kiorthodox na Makanisa mengine ya Kristo ya Mashariki, ameonesha uchungu katika hali ambayo leo hii zinasikika silaha na kilio cha uchungu cha watu katika  vurugu za vita na wakimbizi, ambao miongoni mwao kuna idadi kubwa ya watoto wasio na hatia. Patriaki ameandika kuhusiana na vita nchini Ukraine na anazungumza kuhusu waamini na thamani ya watu wa Ukraine ambao wanabeba msalaba mzito, wa wakimbizi ambao ameweza mwenyewe binafsi kuwatembelea nchini Poland. Patriaki amesema: “Tangazo la kung'aa la ufufuko na Kristo limetokea leo hii kwa sauti kubwa ya silaha na kilio cha uchungu cha waathirika wasio na hatia wa ghasia za vita na wakimbizi, ambao miongoni mwao ni idadi kubwa ya watoto wasio na hatia”.  Patriaki ameomba kuendelea kuwaombea na kupambana kwa ajili ya amani na haki, na kwa wale ambao wamenyimwa. Na hivyo amekemea ukimya wa wakristo wengine mbele ya uharibifu huo wa hadhi ya binadamu.

Sala ya pamoja kati ya Patriaki na Askofu Gadecki wa Poland

Kwa mujibu wa mchambuzi Nikos Tzoitis wa Upatriaki wa Kiekumene wa Costantinopoli amesema, Patriaki I na Gadecki wa Poland, walisali pamoja kwa ajili ya Amani wakiwa katikati ya wakimbizi wa Ukraine. Uchungu wa Patriaki, inatokana na ukweli kwamba, ingawa binadamu daima anajaribu kuishi kwa amani, licha ya hayo, ubinadamu unaishi katika vita vinavyoendelea, ambapo hadhi na utu wa  mwanadamu na amani duniani vinaharibiwa na ni mbaya sana. Wanafalsafa wote wakubwa, katika historia ya mwanadamu, wamesema kwamba maisha ya mwanadamu yamo katika matamanio yake ya uhai, katika kuishi katika ulimwengu wa haki, hata hivyo tunazingatia mambo ya hivi karibuni ya metudi kuleta swali ambalo linajionesha kifo kutawala katika ulimwengu.

Ubinadamu ni ushindi mkubwa wa vita

Pamoja na waathirika, ubinadamu ni ushindi mkubwa wa vita, kulingana na maandishi ya Patriaki Bartolomeo, kwamba ubinadamu ambaye katika historia yake ndefu hajaweza kukomesha vita na ambaye sio tu kusuluhishi shida, lakini anaunda  kwa upya  mpya vilivyo vigumu zaidi. Anapanda mgawanyiko na chuki, anaongeza pengo kati ya watu. Kwa mujibu wa mchambuzi huyo Tzoitis ameelzea kwamba  Patriaki Bartolomeo - anataka kuelekeza  kwa sauti hai na ya dhati kabisa, kwamba ni mawazo ya Kikristo pekee yanayoweza kubadili dhuluma hizi, lakini kwa bahati mbaya migawanyiko hii kati yetu Wakristo hairuhusu Makanisa yetu kuwa na sauti moja na kuiinua kwa nguvu dhidi ya udhalimu huu unaosababisha kifo ”. Hayo ndiyo maelekezo ya Patriaki  Bartolomeo, ambaye hata hivyo anakumbuka, zaidi ya yote, jinsi inavyofaa kwa Mkristo kuwa kwanza kabisa, mtunza amani , na kama Kanisa la Kristo, kwa asili yake kama watunza amani.

Ubinafsi umetawala hata katika Kanisa na ubinadamu unalipa gharama

Kwa bahati mbaya, ubinafsi umetawala katika Kanisa na ubinadamu unalipa kwa hili pia, yaani, Kanisa lililogawanyika ambalo halijui jinsi ya kupaza sauti yake dhidi ya kifo . Tumaini ambalo Patriaki Bartolomeo anakabidhi katika ujumbe wake liko katika ukweli, na anawakumbusha waamini, kwamba Ukristo si itikadi, bali ni ukweli wa maisha. “Tunahitaji kugundua tena maana ya Kanisa, kuwa kanisa, ambalo lina maana mimi nipo kwa sababu jirani yangu pia yupo na ambapo maana kwamba kuvumilia haimaanishi kumkubali mwingine kwa kiburi, bali kujitoa mwenyewe kwa ajili ya utunzaji  wake. Hili ni muhimu sana kulielewa kwa sababu kila mtu, kama vile Papa Francisko alivyosema wakati akimkumbuka Mtakatifu Yohane Grisostom, asemaye:“kwa Bwana wetu sisi ni sehemu ya kundi moja, sisi sote ni watoto wa Mama Kanisa moja na tunapaswa kukutana kwa unyenyekevu, si kwa ubinafsi

26 April 2022, 15:52