Sinodi ya Jimbo Napoli:Ask Mkuu Battaglia,Kanisa lioshe miguu ya maskini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Si jambo lile lile kusema juu ya haki kutoka juu ya usalama wetu wa kijamii na kiuchumi au kufanya hivyo wakati, kwa upande mwingine, tunapitia hali za hatari, mateso, umaskini. Wakati wa msimu wa baridi, wakati huna chochote cha kula, wakati haujui jinsi ya kujikinga na baridi, wakati haulali, na unajikuta umekandamizwa, umebandikwa lebo na kuepukwa na kila mtu, basi unaelewa kuwa hii ni tofauti kabisa jambo la kuongelea haki, hadhi na haki ya kunyimwa. Amesema hayo Askofu Mkuu Domenico Battaglia, wa Jimbo Kuu Katoliki la Napoli nchini Italia akifunga Sinodi ya XXXI kijimbo iliyoudhuriwa na mamia elfu ya wanajimbo kuu la Napoli nchini Italia. Katika hotuba yake amesisitiza kwamba kama vile si jambo lile lile kusali katika usalama wa hekalu ukisema Bwana, Bwana, ukiwa mbali na maisha ya kila siku ya wale wanaohangaika, mbali na historia ya watu na salama kutokana na udhaifu, umaskini, na taabu zinazowakandamiza na kukoksa kuwepo kwako karibu nao. Kwa hiyo Askofu Mkuu ametoa mwaliko kwamba ni lazima tujielimishe kujua mahitaji kama haki zisizozingatiwa, kujifunza kufanya kila maskini unakuwa wazi na kutafuta haki yake kwa sababu ananyimwa.
Akiwageukia maskini, waliotengwa, walioachwa, peke yao, wenye njaa, waliokandamizwa, alisema: “Wewe unaweza kunifundisha kupenda. Unaweza kunifundisha kushiriki maisha. Unaweza kunifundisha kuamka. Unaweza kunifundisha kutumaini, wewe unaweza kuelekeza wakati ujao, na unaweza kweli kunikumbusha kuwa ni upendo tu unaobaki. Askofu mkuu vile vile vile alijikita kusema kuwa ushirika ni zawadi inayoomba kukubaliwa kwa kuwajibika. “Wote tumeitwa kujenga udugu, kujenga upya magofu ya kale na miji mikiwa. Chaguo la upendeleo kwa maskini, kuwa na tahadhari angalau, ambayo inakuwa mtindo wetu wa maisha, mtindo na shauku halisi ya ukaribu, ili mwingine, maskini, aweze kuwa ndugu. Uongofu kwa ushirika wa kindugu ni njia endelevu katika uhuru”. Kwa kuwashauri kusikiliza kila mtu na kufanya hivyo hasa barabarani, askofu mkuu kwa hakika alikiri na kusema: “Ni mara ngapi, hata hivyo, tunabaki kufungwa katika hekalu letu, kuzungumzia katika hali ya juu ya imani yetu bila kujiweka karibu na kila mmoja wetu mwenye kuhitaji, bila kuunda uhusiano huo wa mlalo na ambao Yesu mwenyewe ni mwalimu na shuhuda”.
Askofu Mkuu Battaglia aliomba kupeleka bembelezo la Bwana, bembelezo ambalo hutia ujasiri kwa wale wanaoishi kwa hofu. Mabembelezo yanayowapa matumaini wale waliofunikwa na kivuli cha kukatishwa tamaa na kujiuzulu. Kubembeleza kunaonesha njia kwa wale wote waliopotea. Mabembelezo yanayohuisha nguvu kwa wale waliochoka na kukata tamaa. Kubembeleza kunamfanya ndugu aliyeachwa na aliyetengwa hasijisikie kuwa peke yake. Bembelezo ambalo linajaza zawadi yetu na uwepo karibu. Kanisa linalomtangaza Mfufuka kwa njia hii haliwezi kuishi bila Bwana, haliwezi kuishi bila ndugu. Ni Kanisa ambalo linajua jinsi ya kusimama kidete na kusubiri, ili mtu yeyote asibaki nyuma. Ni Kanisa ambalo hupitia taabu ya kibinadamu ya kufadhaika, wasiwasi na kushiriki na kila mtu mateso makali zaidi, ukosefu wa usalama. Kanisa lililo hakika tu na Bwana wake, na dhaifu, dhaifu, linalohitaji kila kitu. Ni Kanisa la Injili.
Wakati wa Ufunguzi wa Sinodi hiyo Askofu Mkuu Bataglia alisema kwamba katika maadhimisho ambayo Mungu wa Yesu Kristo ni Mungu wa watu, wa wadhaifu na maskini wanahitaji ujasiri na uthabiti. Wanahitaji nguvu za kurudia mambo yale yale nje ya hekali, kushuhudia kweli ule ujumbe mkubwa ambao ni Roho anayetoa zawadi na kuwakabidhi. “Ni ujumbe ambao unatuita kutoka nje ya wazo, nje ya busara zetu na hali salama zetu, ili kufanya huduma ya mwanadamu, kwa jina la Injili, kurejesha neema ya uwazi, bila kufifisha lengo kwa kuogopa maisha ya utulivu, na ndipo inaaminika, matendo na kuna uharaka wa kwenda kwa kila mtu”. Askofu mkuu Battaglia alikumbuka uso wa maskini, wanaoteseka, na waliotengwa. “Kuwepo kwa maskini miongoni mwetu si matokeo ya kubahatisha tu lakini ni matokeo ya muundo wa dhambi wa mahusiano. Jamii zetu zinahitaji uwajibikaji wa pamoja kwa sababu maskini wapo na lazima tujiulize kwa nini wanaendelea kuwapo?”
Askofu Mkuu aidha alitazama hata vita vinavyoendelea na kusema kuwa “Janga na vita hivi vya kipuuzi vinasisitiza uwepo wa mfumo wa kiugonjwa ambao unaendelea kuzalishwa kifo. Hatuwezi tena kufunga macho yetu, hatuwezi tena kuahirisha, lazima tuchague mtindo gani wa maisha tunapendelea. Imani yetu inatutaka tuangalie kwa uaminifu. Kanisa linalotaka kuwa maskini, sinodi, katika hali ya kudumu ya utume, linaitwa kujiweka sawa na maisha, pamoja na Bwana, kwa juhudi za wanaume na wanawake wa wakati huu. Mwanafunzi wa Yesu haukimbii umaskini na maskini bali anawachagua. Utunzaji huu muhimu wa kuishi na kuchaguliwa ni ishara ya kweli ya upendo wa Mungu ndani yetu. Tumeitwa kuishi katika utata wa wakati huu”, alisisitiza Askofu Mkuu Mimmo.
Akiendelea kiongozi mkuu wa Kanisa la Napoli alisema: “Ikiwa tunakaribisha tumaini la maskini na kujitolea maisha yetu kuyasikiliza na kuyatumia katika matendo, kwa haki ya Mungu itafichuliwa kwetu na kwa ulimwengu mzima, maisha ya haki, ya misalaba ya historia, kama chachu ya mabadiliko, tangazo la maisha yaliyokamilishwa katika kuwafanya watu waishi. Siku zote maskini huwa na nafasi ya kwanza katika haki. Njia ni ndefu kwa sababu inahusisha mabadiliko ya mtazamo, mawazo, na vigezo”, alisisitiza Askofu Mkuu Battaglia. Ishara thabiti za upyaishaji huu zitakuwa mazungumzo, majadiliano, kusikilizana, kwenda kukutana na kila mtu bila kutabiri hali na watu. Mungu hayuko katika ugumu, Mungu hayuko nyuma, Mungu hayuko katika kujifungia. Ni katika kutokuwa na usawa, ambayo ni kutokuwa na usawa wa upendo. Na anashughulikia umaskini wote, njaa ya mkate na njaa ya maana. Na hujaza maisha sio kwa vitu, lakini kwa watu. Kulipenda Kanisa la Napoli na ndiyo sasa litajua wapi pa kuanzia tena, alisema na lusema kwamba ni kuanzia katika vitongoji vya kila mtu anapoishi, kwa wanaume wa mkate wa uchungu, kutoka katika njaa ya huruma, kutoka kwa wale walio tengwa. Na kukusanya tena vipande vya ulimwengu huu uliolipuka kuwa umoja”, ndiyo umekuwa mwaliko wa Askofu Mkuu wa Napoli na kwamba “Kila kitu kiwe na nguvu, cha kipekee, kisichoweza kuepukika na msingi wa Injili.
Askofu Mkuu lakini, alionya, kuwa ushuhuda ni wa wote na wa kila mtu. Kwa kila mmoja wao, watu wa Mungu ambao wamekabidhiwa kwake, anahisi anaweza kusema kwamba kazi ya ukuhani ya Kristo haijahamishwa tu kwa kundi la watu lakini kwa watu wote wa Mungu. Kwa hiyo, watu wote wa Mungu, kila mmoja wao lazima ajisikie kuwa amepakwa mafuta na Bwana na kuitwa kumtangaza katika njia za ulimwengu, kupeleka tumaini lake, neema yake na upendo wake. Askofu Mkuu Battaglia alionesha ni Kanisa gani analotamani kuishi ndani yake kwamba: Kanisa lililo na milango wazi kwa wote, kwa sababu wanalihitaji. Kanisa ambalo sio tu la kufanya ibada lakini ambapo maisha ya wanawake na wanaume wanaishi na kuadhimishwa, yaliyojaa furaha na huzuni. Kanisa linaloondoka kwenda nje, Msamaria, huru, aminifu katika Injili, Kanisa maskini, Kanisa la Sinodi, likimsikiliza Roho Mtakatifu. Katika wakati huu yeye anaota ndotoo ya moyo wa Kanisa mama ambalo ndani ya tumbo lake la uzazi linazaa, linafanya kukua, kuponya na kufanya maisha kuchanua maisha mapya.
Kwa kuhitimisha Askofu Mkuu Mimmo anatamani Kanisa linaloosha miguu ya wanaume na wanawake yaani maskini bila kuomba malipo yoyote, hata bei ya kumwamini Mungu, au ushuru wa kwenda kwenye Misa ya Dominika au sehemu ya maadili yasiyofaa, maisha na zaidi kulingana na Injili. Kanisa ambalo ni karibu kweli, Kanisa lililo wazi ambalo linakaa nafasi ya ukaribu kwa njia ya kukaribisha bila dhamana ya hapo awali. Kwa ufupi, Kanisa lisilo na uwezo, Kanisa lisilohesabu, lisilojilinda, halijifichi nyuma ya maadili potofu na mikakati ya kichungaji, bali linaakisi taswira ya Kanisa, ni ushirika katika kutafuta mara kwa mara waratibu wa baraza, hiyo inafanya iwe jumuiya ambalo linaweza kutembea na anataka kutembea pamoja, bila kujali gharama! Ni Kanisa linalofunguka. Na Kanisa hili linaomba unabii na kwenda nje na kupaza sauti ya neno linalotoa uhuru na uwezo wa ukaribu wa kweli, halisi katika njia za ulimwengu kupeleka tumaini lake, neema yake na upendo wake.