Maandamamo ya Ufufuko katika  Madhabahu ya Mama wa Medali ya Miujiza huko  Zakopane-Olcz nchini Poland Maandamamo ya Ufufuko katika Madhabahu ya Mama wa Medali ya Miujiza huko Zakopane-Olcz nchini Poland 

Ujasiri na amani ndiyo matashi mema ya Pasaka kutoka kwa Maaskofu wa Poland

Ujumbe wa maaskofu nchini Poland,uliochapishwa na Askofu Mkuu Stanisław Gądecki,katika fursa ya Ufufuko wa Bwana 2022,anawatakia waamini wote ndani ya Poland,nje yake na wakimbizi ili wawe na ujasiri na amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, Askofu Mkuu Gądecki wa Jimbo Kuu Katoliki la Poznań, nchini Poland amechapisha ujumbe wakekatika  Tovuti ya Baraza la Maaskofu akiwageukia wapoland  nchini  humo na wale walioko nchi za nje, ikiwa ni pamoja na wakimbiz ambao wanaishi kipindi hiki  kwa cha siku kuu katika nchi yao kutokana na vita nchini mwao ili wasikate tamaa. Askofu Mkuu anaandika kwamba: “Katika wakati huu mgumu uliotokana na vita nchini Ukraine, watu wengi wamekumbwa na wanateseka na mbele ya macho ya ulimwengu wote, na kwa maana hiyo ni matashi mema kutoka kwetu ili wawe na ujasiri na amani”.

Imani, tumaini na upendo

“Bwana mfufuka ajaze mioyoni mwetu imani, matumaini na upendo ili tuweze kuadhimisha muujiza wa asubuhi ya Pasaka, kwa kuwa na  imani kuwa Yeye alishinda ubaya, hata ule ambao umekumba ulimwengu wa kisasa”. Askofu ameongeza kuandika kuwa uzoefu wa fumbo la Pasaka unasaidia kukumbatia kwa uthabiti Kristo ambaye analeta wokovu na wakati huo huo kuwa shuhuda wa upendo wa huruma.

17 April 2022, 13:51