Maaskofu wa Brazil wakati wa hija yao ya kitume jiji Vatican 2020. Maaskofu wa Brazil wakati wa hija yao ya kitume jiji Vatican 2020. 

Brazil:Juma Kuu Takatifu linafundisha kupeleka upendo wa Kristo

Ujumbe wa Rais wa Maaskofu katoliki nchini Brazili katika kipindi cha Juma Kuu ambalo ni juma kubwa la kipindi chote cha liturujia ya mwaka linalowafanya waamini kukua kwa kina ndani ya upendo wa Yesu Mfufuka na kuwezesha udugu katika ulimwengu.

Na Sr. Angella Rwezaula- vatican.

Kuishi Juma Kuu ni kwa ajili ya mateso, kifo na ufufuko wa Yesu, ambalo ni tendo la  hitimisho la maisha ya Kikristo na kwa maana hiyo waamini wote na wenye mapenzi mema nchini  Brazil wanaalikwa hata kuishi kupindi kikubwa  hiki cha mwaka. Amesema hayo Askofu Mkuu Walmor Oliveira de Azevedo, wa Jimbo Kuu Katoliki la Belo Horizonte na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Brazili. Kuishi ni mwaliko wa upendo katika maisha yetu ya ndani. Yesu, Mwana wa Mungu awezaye yote, anakabiliana na uchungu mkali sana na anakufa kwa ajili ya kutuokoa;  anatufundisha kuwa maisha yana maana tu  ikiwa   yanakuwa sadaka kwa ajili ya wema wa jirani.

Maaskofu nchini Brazil
Maaskofu nchini Brazil

Askofu De Azevedo amesema “Wakati maisha yanakuwa sadaka inayojikita juu ya upendo, unashinda hata kifo, maisha yanga’aa na ndio anatufundisha Kristo Mfufuka. Katika ujumbe wake kwa njia ya video, Askofu mkuu amesisitiza, kwamba msingi wa mafundisho ambayo yamo katika Juma Kuu Takatifu, ndiyo, kwa hakika mwaliko wa kupeleka upendo wa Kristo ndani ya maisha yetu na kujikita baadaye kwa udugu wa ulimwengu.

Maaskofu nchini Brazil walipokutana na Papa mnamo 2020
Maaskofu nchini Brazil walipokutana na Papa mnamo 2020

Maisha yetu yageuke kuwa sadaka ya upendo

Ikiwa maisha ya kila mtu yanageuka kuwa sadaka ya upendo hakutakuwa na ugomvi kwa sababu ya kutoelewana ambako ni kwa kawaida , hasa katika kipindi cha uchaguzi (Nchini Brazil Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2022), kuibuka kwa vita kutaacha  nafasi ya Amani. Ubinadamu hautakuwa na tabia za kutojali uchungu wa kaka na dada. Kwa mujibu wa Rais wa Maaskofu amesema kila mmoja atashiriki sehemu yake, ulimwenguni hatimaye kutazaliwa Amani sintofahamu za mahitaji ya jirani hazitakuwapo. Juma Kuu na upendo wa Yesu Mfufuka, uwezeshe kila mmoja kuwa mstari wa mbele katika  ujenzi wa ulimwengu wa haki zaidi, wa mshikamano zaidi na udugu na ndiyo ilikuwa ni  matashi mema ya siku kuu.

14 April 2022, 15:35