Tafuta

Katika Mkutano Mkuu wa 76 umetangazwa Rais mpya wa Baraza la Maaskofu Italia CEI Kardinali Zuppi kati ya watatu waliopelekwa kwa Baba Mtakatifu. Katika Mkutano Mkuu wa 76 umetangazwa Rais mpya wa Baraza la Maaskofu Italia CEI Kardinali Zuppi kati ya watatu waliopelekwa kwa Baba Mtakatifu.  

Kardinali Zuppi ni Rais Mpya wa Maaskofu wa Italia

Papa Francisko amefanya uteuzi mara baada kuwakilishwa majin ya watatu waliochaguliwa na CEI katika Mkutano Mkuu jijini Roma.Rais anayemaliza muda wake Kardinali Bassetti alisoma taarifa kutoka kwa Papa Francisko.Kardinali Zuppi ni mzaliwa wa Roma,mwana Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,mchungaji wa Kanisa Kuu la Bologna tangu 2015,na anajulikana kwa kujitoa kwake kwa ajili ya waliotengwa na wasio na uwezo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa amechagua. Huyo ni Kardinali Matteo Maria Zuppi, mwenye umri wa miaka 66, ambaye ni askofu mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bologna, ambaye ndiye rais mpya wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI). Uteuzi huo umekuja asubuhi tarehe 24 Mei 2022, muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa 76 wa CEI unaofanyika Hilton karibu na Uwanja wa Ndege kimataifa wa Fiumicino, Roma. Hata hivyo uchaguzi huo umetokea mara baada ya maaskofu kutoka pande zote za Italia kufanya uchaguzi wa watu watatu kwa ajili ya uteuzi wa mwisho wa rais ambaye angechukua nafasi ya Kardinali Gualtiero Bassetti, mwenye umri wa  80, na ambaye ni askofu mkuu wa Perugia-Città della Pieve.

Na alikuwa ni Kardinali  Bassetti aliyemaliza  muhula wake wa w Urais kwa miaka mitano na kutoa ufunguzi wake wa mwisho Jumanne asubuhi,  24 Mei 2022  kwa kusoma taarifa  ya Baba Mtakatifu kuhusiana na  chaguo la Kardinali Zuppi, kuwa wa kwanza kati ya watatu waliowasilishwa kwake.  Kwa maana hiyo mara baada ya tamko hilo, maaskofu waliokuwapo walilipokea kwa kishindo cha  makofi ambacho kimerudia tayari  historia  iliyofanyika katika muongo wa 1969-1979, wakati  Baraza la Maaskofu Italia (CEI) waliongozwa na askofu mkuu Antonio Poma wa Bologna.

Kabla ya kuwasili Bologna, ambako Papa Francisko alimteua kuwa Askofu mkuu mnamo tarehe 27 Oktoba 2015,akimrithi Kadinali Carlo Caffarra, Kardinali Zuppi, anayejulikana na wote kama ‘Don Matteo’ na bado anaitwa hivyo, alianza historia yake ya kibinafsi na ya kikuhani jijini Roma. Kiukweli, alizaliwa katika mji mkuu, katika familia ya watoto sita: yeye ni wa tano. Hatua ya kwanza muhimu ni mnmo 1973, miaka ambayo alisoma katika shule ya sekondari ya Virgilio, mahali ambapo aliweza hata kukutana na David Sassoli, aliyekuwa rais wa baadaye wa Bunge la Ulaya (na ambaye hivi karibuni Kardinali  Zuppi aliadhimisha misa ya mazishi yake mnamo Januari 14 mwaka huu) na kuunda uhusiano wa kina na wa kudumu na Andrea Riccardi, mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.

Kwa maana hiyo  Zuppi alinza kushiriki Jumuiya na kushirikiana katika shughuli za huduma kwa wale ambao wanahitaji msaada kwa mfano kutoka katika shule maarufu kwenda kwa  watoto waliotengwa wa makazi duni ya Roma, hadi kufikia mipango ya wazee ambao wako peke yao na wasiojitegemea, wahamiaji na wakimbizi, wasio na makazi, wagonjwa mahututi , walemavu na wanaokula dawa za kulevya, wafungwa na waathirika wa migogoro. Vile vile hata katika hatua za kiekumene kwa ajili ya umoja kati ya Wakristo hadi kwa ajili ya mazungumzo ya kidini, ambapo hayatasaulika yaliyota mkutano  huko Assisi.

Akiwa na umri wa miaka 22, baada ya kuhitimu masomo ya Fasihi na Falsafa katika Chuo Kikuu cha La Sapienza, kwa tasnifu katika Historia ya Ukristo, Kadinali wa baadaye alijiunga katika seminari ya jimbo la Roma huko Palestrina, akifuatilia kozi za maandalizi ya upadre katika Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano na kupata  digrii ya taalimungu. Tarehe 9 Mei 1981 alipewa daraja la Upadre kwa ajili ya mapadre wa Palestrina na mara baada ya hapo akawa  Padre wa Parokia ya Kanisa Kuu la Kiroma la Mtakatifu  Maria huko Trastevere, kwa kuchukua nafasi ya Askofu Paglia.

24 May 2022, 17:31