Tafuta

Ujumbe wa Mababa wa AMECEA kwa Watu wa Mungu Ukanda wa Nchi za AMECEA kwa Mwaka 2022 kuhusu utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote. Ujumbe wa Mababa wa AMECEA kwa Watu wa Mungu Ukanda wa Nchi za AMECEA kwa Mwaka 2022 kuhusu utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote. 

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA: Ujumbe Kwa Watu wa Mungu 2022

Ibada ya Misa Takatifu katika kufunga Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA imeongozwa na Kardinali Polycarp Pengo Ujumbe wa Mababa wa AMECEA kwa watu wa Mungu ukasomwa kwa lugha ya Kiswahili na Mheshimiwa Padre Anthony Makunde Katibu mkuu mpya wa AMECEA. Maadhimisho ya Mkutano Mkuu wa 21 wa AMECEA kwa mwaka 2026 utafanyika Kampala, nchini Uganda.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati AMECEA, linaloundwa na Nchi 8 ambazo ni: Zambia, Malawi, Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Ethiopia na Eritrea, kuanzia tarehe 10-18 Julai 2022 linaadhimisha mkutano wake mkuu wa 20 Jijini Dar es Salaam. Djibout na Somalia zimealikwa kushiriki kama nchi watazamaji. Mkutano huu ambao umefungwa rasmi kwa Ibada ya Misa Takatifu, Dominika tarehe 17 Julai 2022 umenogeshwa na kauli mbiu: “Utunzaji wa Mazingira kwa Ajili ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu.” Hii ni kauli mbiu inayochota maudhui na utajiri wake kutoka katika Waraka wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko, “Laudato si” yaani “Sifa iwe kwako” juu ya utunzaji wa nyumba ya wote” unatoa kipaumbele cha pekee katika ulinzi na utunzaji wa mazingira nyumba ya wote. Ibada ya Misa Takatifu katika kufunga Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA, Dominika tarehe 17 Agosti 2022 kwenye Viwanja vya Msimbazi Centre Jimbo kuu la Dar Es Salaam imeongozwa na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Dar Es Salaam.

Mababa wa AMECEA Wametoa ujumbe wa mshikamano Afrika Mashariki na Kati
Mababa wa AMECEA Wametoa ujumbe wa mshikamano Afrika Mashariki na Kati

Ujumbe wa Mababa wa AMECEA kwa watu wa Mungu Ukanda wa Afrika Mashariki umesomwa kwa lugha ya Kiswahili na Mheshimiwa Padre Anthony Makunde Katibu mkuu mpya wa AMECEA. Mababa wa AMECEA wametangaza kwamba, maadhimisho ya Mkutano Mkuu wa 21 wa AMECEA kunako mwaka 2026 utafanyika Jijini Kampala, nchini Uganda. Ni ujumbe unaotoa utangulizi kuhusu AMECEA, Shukrani kwa TEC na Serikali ya Tanzania, Ujumbe wa dhima ya mkutano wa 20 wa AMECEA, Mgogoro wa kiikolojia, hofu na mashaka ya Mababa wa AMECEA kuhusu mazingira Ukanda wa AMECEA, ushauri makini unaokwenda sanjari na uhamasishaji wa utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote. Mkazo umeelekezwa zaidi katika masuala ya elimu bora ya mazingira na kwamba, Mababa wa AMECEA wataendelea kuragibisha utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote na mwishoni, ni ujumbe wa mshikamano wa udugu wa kibinadamu kwa wale wote waliotharika kutokana na mabadiliko ya tabianchi, vita, kinzani na migogoro mbalimbali. AMECEA inaiombea Kenya ili uchaguzi wake hapo tarehe 9 Agosti uweze kuwa huru, haki na kweli ili amani iweze kutawala nchini Kenya kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu tarehe 9 Agosti 2022.

Tamko AMECEA 2022
17 July 2022, 15:11