Picha ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Amecea katika Uwanja wa Kitaifa wa (Mkapa) DSM Tanzania,10 Julai 2022:Mkutano uliongoza na mada ya utunzaji wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja Picha ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Amecea katika Uwanja wa Kitaifa wa (Mkapa) DSM Tanzania,10 Julai 2022:Mkutano uliongoza na mada ya utunzaji wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja  

AMECEA:Bi Kessy,Utunzaji wa Mazingira uanzie nyumbani!

Ikiwa mwezi moja umepita mara baada ya Mkutano Mkuu 20 wa AMECEA kufanyika jijini Dar Es,Salaam,tunaendelea kukumbusha mada waliyojikita nayo ya utunzaji wa Mazingira.Vatican News ikizungumza na baadhi ya washiriki kama vile Bi Angela Kessy wa Parokia ya Salasala Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam Tanzania,alihimiza utunzaji wa mazingira kuanzia na familia nyumbani.“WAWATA isali kwa ajili ya mapadre”.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Ni mwezi mmoja umepita sasa tangu kumalizika mkutano Mkuu wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA) ambao ulianza tarehe 10 na kuhitimishwa mjini Dares Salam Tanzania  tarehe 18 Julai 2022. Katika Mkutano wao mada kuu ilikuwa juu ya utunzaji wa mazingira kwa kuuenzi Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko wa Laudato Si, ambapo kwa hakika Maaskofu wa Kanisa Katoliki katika Ukanda huo wa Afrika Mashariki wamekiri kwamba kuna mgogoro wa kiikolojia ambao kwa kiasi fulani unasababishwa na mwanadamu katika eneo hilo lote na kwingineko. Katika mada hiyo na mkutano huo bado kumbu kumbu ni hai na tuna mengi sana na tutaendelea kujikumbusha yale yaliyojitokeza na ambayo yataongoza hasa katika utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja na mikakati yao waliyojiwekea ili katika jumuiya zao ndogo ndogo ziwe mwendelezo na msimamo wa utunzaji wa mazingira; kupambana kwa kila hali katika utetezi huo wa mazingira.

Maaskofu wa AMECEA
Maaskofu wa AMECEA

Mwenyekiti wa AMECEA Askofu Charles Kasonde  wakati wa kuhitimisha misa aliwashukuru watanzania kwa ukarimu wao wa kuwakaribisha wajumbe wa Mkutano wa 20 wa AMECEA uliofanyika nchini Tanzania huku akisema ili nchi jirani zionje ukarimu na amani sawa. Aliyasema hayo alipokuwa akitoa mahubiri yake katika Misa Takatifu ya kufunga Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA katika viwanja ywa  kituo cha Msimbazi Jimbo Kuu la Dar es Salaam ambapo alisisitiza kuwa Neno la Mungu linahimiza  kuwa waaminifu, wakarimu, kuendelea kuwa imara na pia kuamini katika nguvu ya Injili. Katika somo la kwanza la kitabu cha Mwanzo, Ibrahim alitembelewa na watu watatu kwenye makazi yake; akawapokea na kuwaandalia chakula. Huu ni mtazamo wa mioyo ya Waafrika.” Kutokana na hili alisema, “Hii ni dhihirisho la utamaduni wa Kiafrika na hili ndilo tumeliona na kushuhudia na uzoefu hapa Tanzania tangu tulipofika… nashukuru kwa hilo. Huu ndio uchangamfu wa Mwafrika na pia ukarimu wa watanzania kisima cha amani. Tunapenda kuziombea nchi jirani ili zionje amani na upendo. Ninataka kusisitiza hatua ya ukarimu, kutoa nje. Tunahimizwa kuwa wema na pia kujitambulisha na ndugu na dada zetu”.

Misa wakati wa Mkutano wa AMECEA
Misa wakati wa Mkutano wa AMECEA

Askofu Kasonde pia alisisitiza kuwa kila mbatizwa ameitwa kushuhudia upendo wa Yesu Kristo ambapo kutakuwa na nyakati za misukosuko, majaribu na dhiki “Hatupaswi kukata tamaa bali tuwe imara na kushuhudia ukweli ambao tumeupata kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Na hii ni faraja kwamba kila tunapokutana na matatizo na pia matatizo katika utume wetu tusikate tamaa bali tubaki waaminifu kwa Mungu, na hiyo ndiyo roho ya umisionari, roho ya askari wa Kristo. Acha kile tunachofanya kihamasishwe na Neno la Mungu. Kipaumbele ni kupokea neno la Mungu ili kile tunachofanya kiwe kutoka kwa upendo wa Kristo na kutoka kwa upendo huo tuliopata kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Na kisha tutatoka, kama tunavyofanya hapa tumekuja kumwabudu Bwana, tusikilize neno lake ambalo linaweza kusema nasi, anaweza kutusaidia kutafakari”. Pia aliongeza kuwa kwa kuongozwa na neno la Mungu, kila mmoja anapaswa kuwa tayari kutoka nje ya utume, kwenda kufanya kazi nzuri ya uwezo wake, kwani ndivyo Bwana anatuomba

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki AMECEA
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki AMECEA

Hata hivyo akisoma Risala wakati wa Misa ya kufunga Rais wa AMECEA Askofu Charles Kasonde wa Zambia, alisema kuwa kung’ang’ania maliasili mara nyingi kumesababisha migogoro na vita, jambo ambalo linafanya ‘kilio cha Mama Dunia na maskini kuwa zaidi. Askofu Kasonde alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki, msukosuko wa kiikolojia kwa sasa unathibitishwa na athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi ambayo ni pamoja na ukame, mafuriko na vimbunga, pamoja na majanga mengine ambayo yanazidi kuwa tishio kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi na kwa maendeleo endelevu, mustakabali wa maisha ya watu. Maaskofu hao pia walieleza kusikitishwa na kasi ya misitu kuharibika haraka kutokana na matumizi ya kuni, uchomaji mkaa na shughuli za ujenzi wa miundombinu huku wananchi wakiwa hawafanyi jitihada za kutosha kupanda miti upya. “Tuna wasiwasi sawa kuhusu uchimbaji madini na ukosefu wa mifumo madhubuti ya usimamizi wa taka. Tunafahamu kwamba kushughulikia masuala haya kunagusa haki ya kiuchumi na haki. Kwa hivyo, haziwezi kushughulikiwa vya kutosha bila kuzingatia ipasavyo kutoa njia mbadala kama vile kukuza matumizi ya nishati ya jua na upepo na njia zingine za kujipatia riziki. Hata hivyo, haya yote yanachangia uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa mazingira katika eneo la AMECEA, " alisisitiza Askofu Kasonde

Askofu Kasonde wa Zambia ni Rais wa AMECEA
Askofu Kasonde wa Zambia ni Rais wa AMECEA

Pamoja na hayo Maaskofu hao walilipongeza zaidi Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), serikali, majimbo, Jumuiya za Kikatoliki, wanaume, wanawake na watu wote wenye mapenzi mema ambao wanachukua hatua za kulinda viumbe hai kama vile upandaji miti na kusafisha miji. Maaskofu pia walisisitizia wito wa kampeni kali ya uhamasishaji wa mazingira katika ngazi ya msingi ya jamii ili kuongeza uelewa kwamba: “Tunasisitiza wito wa kampeni kali ya uhamasishaji katika ngazi msingi ya jamii ili kuongeza uelewa na kuboresha mawasiliano yetu na watu kuhusu utunzaji wa mazingira katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo na ngazi ya familia".

WITO WA UENDELEZAJI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KUTOKA AMECEA

Katika mahojiano na Bi Angela Benedikt Kessy, kutoka Parokia ya Sala sala, Jimbo kuu Katoliki la Dar Ess Salaam Tanzania, na ni mama WAWATa yaani Umoja wa Wanawake Katoliki Tanzania, aliweza kuhimiza utunzaji bora wa mazingiria hasa kuanzia na watoto na familia nyumbani na umuhimu  wake  kwa kukumbuka enzi zake utotoni na  kutoa mfano walivyokuwa wakitekeleza hayo wakiwa watoto na vijana. Bi Kessy alielezea juu ya shughuli za WAWATA katika Kanisa hasa kwa kutoa mfano bora wa kunyonyesha vijana walioko katika malezi ya  seminarini na aibainisha juu ya umuhimu wa kuombea kila  mseminari kwa sala. Suala hili yeye binafsi anaonelea kwamba kwa maaskofu wanaweza kufanya hivyo kuwakabidhi kila mama mseminari mmoja mmoja ambaye asindikizwe na mama hao wakisali kwa ajili yao.

Utunzaji bora wa Mazingira Lauda si
Utunzaji bora wa Mazingira Lauda si

Pamoja na hayo na ubunifu mwingi alio nao mama huyo pia ni mtunzi wa vitabu kadhaa vya sala ambavyo kwa Tanzania vinajulikana kwa mfano ameandika 'kitabu cha nguvu ya sala', 'kitabu cha Padre Pio', ambacho ameeleza kuwa ni matumaini ya wanaoteseka na kitabu kingine ni 'Antonio wa Padua' na wakati huo huo kitabu kitakachofuata hivi karibuni, kinaitwa "Mama Tazama Mwanao Padre". Kitabu hiki kwa mujibu wa Bi Kessy amekiandika kwa ajili ya kutoa heshima ya Mapadre ambapo yeye mwenyewe anawaita mapadre kwamba ni " maua" na kwamba yeye anataka kumwagilia maji safii kupitia kitabu hicho kwa madhumuni makubwa kwamba kila  mama anatakiwa kuwa anajua Padre ni nani na ili aweze kuchukua nafasi ya kwanza kama ile ya mama Maria aliyoichukua wakati anamlea mtoto wake Yesu. Kutokana na hilo ndipo wito wa Bi Kessy ameutoa kwa wa mama wote kwamba wanakaribishwa kuungana pamoja ili kuhakikisha kwamba wanawaombea mapadre kila siku.

USHUHUDA WA BI ANGELA KESSY KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
19 August 2022, 12:49