Kanisa Nchini Argentina linahimiza na kutia moyo wa utetezi wa maisha tangu kutungwa kwake mimba hadi kifo cha kawaida cha binadamu. Kanisa Nchini Argentina linahimiza na kutia moyo wa utetezi wa maisha tangu kutungwa kwake mimba hadi kifo cha kawaida cha binadamu. 

Eutanasia,Kanisa la Argentina linatia moyo kutetea maisha

Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Maisha,Walei na Familia nchini Argentina ilichapisha tafakari kufuatia kutangazwa kwa miswada mbalimbali kuhusu mwisho wa maisha katika mabaraza yote mawili ya Bunge la Kitaifa.Wazo pekee la Maaskofu wanasema kwamba:“Sisi sio mabwana wa maisha kwa hivyo tunajiweka kwenye huduma yake.Ni muhimu kusindikiza na dhiki ya mtu anayeteseka na maumivu yake ya kimwili na kiroho."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Maisha, Walei na Familia (CEVILAF) ya Baraza la Maaskofu wa Argentina (CEA) katika tafakari iliyochapishwa tarehe 18 Agosti, wakati wa mapendekezo ya sheria za euthanasia zinazojadiliwa imebainisha kwamba “ .Hata katika magonjwa ambayo hayawezi kutibika, wagonjwa wote lazima wasaidiwe na kusindikizwa ili maisha yao yaheshimiwe hadi kifo cha kawaida. Sisi sio mabwana wa maisha na kwa hili tunajiweka kwenye huduma yake”. Tume hiyo imeandika kwamba: “Katika hali zote thamani yao lazima iwekwe juu ya yote na ni wajibu wa kuwatunza watu katika hatua zote, hasa katika mazingira magumu yao”. Pia Tume hiyo ya maaskofu wanakumbuka mojawapo ya mafundisho ya Papa Francisko kuhusu mada hii kwamba: “Euthanasia na kusaidiwa kujiua ni kushindwa kwa kila mtu. Jibu ambalo tunaitwa ni kutowaacha kamwe wale wanaoteseka, kamwe kukata tamaa, bali kutunza na kupenda kutoa matumaini”.

Huduma shufaa ni muhimu ithaminiwe

Tume hiyo ya Baraza la Maaskofu wa Argentina(CEVILAF) inasisitiza kwamba huduma shufaa na muhimu lazima ithaminiwe, ambayo hupunguza maumivu katika magonjwa makubwa, kusaidia wale wanaoteseka na kuzaa matunda mengi kwa mwanadamu na familia yake” pia kusisitiza kwamba “ni muhimu kusindikiza na dhiki ya mtu anayeteseka na maumivu yake ya kimwili na kiroho. Jukumu sahihi la dawa ni kuponya”, wanakumbsha, “lakini pia kupunguza na kubinafsisha mchakato wa kifo. “ Kuondoa maisha sio njia ya kupunguza mateso. Utunzaji wa maisha na pendekezo la kuitumikia wakati wote ni utume wetu, kila mmoja kutoka mahali pake pa kujitolea na shuhuda mwaminifu”.

Utamaduni wa kifo na kubagua

Tume ya Maaskofu  nchini Argentina inaona kwamba wano wanakabiliwa na dhihirisho jipya la utamaduni wa kifo na wa kutupa kwa wakati mmoja, mbele ya watu ambao kila siku wanaomba kutunzwa kwa maisha yao na mahitaji muhimu kama vile afya, kazi, nyumba na ardhi. Kwa maana hiyo, inafaa kukumbusha kuwa tarehe 30 Desemba 2020,  Rais wa Argentina, Alberto Fernandez, alitia saini amri ya kutangaza sheria ya utoaji mimba. Lakini ujumbe huo unafafanua kuwa hata kama jamii haiwezi kuondoa mateso, inaweza kujitolea kwa nguvu zote kwa ajili ya maisha ya wale wanaoteseka. Tume ya Maaskofu inabainisha kwamba “Watu wa Argentina wana historia tajiri kwa maana hii, katika uwanja wa mshikamano na katika dawa yenyewe. Hatumuachi mtu peke yake na kwa miaka mingi tumeunda njia mbadala nyingi za kusindikiza na maumivu ya mwili na kiroho na sayansi na ubinadamu”, wamesisitiza huku  wakitaja uzoefu wa Hospitali na Cottolenghi.

Kumwomba Mungu pasiwepo nafasi ya sheria za kutenga maisha wale wanaoteseka

Kwa kurudi kwenye hali mbaya ya janga hilo, Tume ya Maaskofu wa Argentina ya utetezi wa maisha (Cevilaf ) inasema tena kwamba katika kipindi hicho wafanyakazi wa afya walichukua mateso ya wanaume na wanawake wengi wanaokufa na kulia kwa kupoteza maisha ambayo walikuwa wamewafanyia kazi bila kuchoka. Kuhusiana na hilo, ndipo wametoa wito kwamba: “Kwa kustahi uhai unaokuja kwetu kutoka kwa Mungu na ambao sisi hatumiliki, kwa kufikiria watu wengi sana ambao wamejitolea kutunza maisha wakiwa wahudumu wa afya, kwa heshima, kwa wale ambao hawapo tena na waliokufa miaka ya hivi karibuni, tunamwomba Mungu kwamba katika nchi yetu pendwa pasiwepo nafasi ya sheria zinazoacha kando na kuwatenga kwenye meza ya maisha wale wanaoteseka zaidi”.

Matamko ya maaskofu kwa ajili ya utetezi wa maisha tangu kutungwa hadi kifo cha kawaida

Katika miaka ya hivi karibuni, maaskofu wa Argentina wametoa matamko mengi juu ya uharaka wa kutetea maisha kuanzia kutungwa kwa mimba hadi kufikia kifo cha asili. Mojawapo ya hizo ilikuwa tarehe 31 Desemba 2020, ambapo Sekretarieti ya Kitaifa ya Familia, ambayo ni sehemu ya Tume ya Maaskofu ya Maisha, Walei na Familia, iliita “siku ya huzuni kwa Argentina” kufuatia kuhalalishwa utoaji mimba nchini. Kwa hivi sasa nchini tangu  tarehe 6 Desemba 2021 kile kinachoitwa “Sheria ya Alfonso  juu ya Haki ya kusaidiwa kufa kwa heshima ilipitishwa na Baraza la Manaibu, na baadaye mnamo Aprili 2022 sheria ya “kifo kizuri” iliwasilishwa kwa Baraza la Mawaziri. Seneti na sheria nyingine inayojadiliwa ni ile ya “kukatizwa kwa maisha kwa hiari”. Wote watatu wana, kama mashirika yanavyoripoti, lengo lile lile: kwamba mtu anayeugua ugonjwa usiotibika anaweza kuamua wakati wake wa  kufa.

UTETEZI WA MAISHANCHINI ARGENTINA
20 August 2022, 11:04