Mchakato wa Sinodi wa Kanisa la Italia: Mkutano wa Kitaifa kwa wahusika wa majimbo yote ya Italia ulifanyika tarehe 13-15 Mei 2022 Mchakato wa Sinodi wa Kanisa la Italia: Mkutano wa Kitaifa kwa wahusika wa majimbo yote ya Italia ulifanyika tarehe 13-15 Mei 2022 

Italia:Muhtasari wa kitaifa wa Sinodi ya Majimbo ya Kanisa la Italia

Baraza la Maaskofu Italia walikabidhi kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu hati ya Kitaifa ya Hatua za kisinodi 2021-23.Katika Mtandao wamechapisha Mhutasari wake ambao unabainisha:“Kuna mihtasari 200 ya majimbo na 19 iliyofafanuliwa na vikundi vingine kwa ujumla vya kurasa zaidi ya 1,500,iliyopokelewa na Sekretarieti Kuu ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ofisi ya kitaifa kwa ajili ya Mawasiliano Kijamii ya Baraza la Maaskofu nchini Italia imetoa Mhutasari wa hatua ya kijimbo ya Maandalizi ya Sinodi 2021-23 inayoongozwa na Kauli mbiu: “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume,” ambapo Baraza hilo lilikabidhi kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu mnamo tarehe 15 Agosti 2022.  Sinodi ina maana ya mchakato wa kisinodi ambao utahitimishwa mnamo 2023 kwa hatua ya ulimwengu mzima, mara baada ya ile ya kibara. Hata hivyo Waraka  huowa Maaskofu unaopatikana mtandaoni, ambao unatoa muhtasari wa njia iliyochukuliwa katika mwaka wa kichungaji  wa 2021-2022, uliojitolea kuwasikiliza na kuwashauri Watu wa Mungu. “Hatua  ya kwanza imeoanishwa kwa ushauri wa Maaskofu,  na  mchakato wa Sinodi ya Makanisa nchini Italia, ambao unazidi kuuishwa maeneo mbalimbali kwa mapendekezo na mipango. Muhtasari, kwa hivyo, pia unatoa muhtasari wa mwaka wa kwanza wa mchakato wa Sinodi , ambao hadi 2025 utaundwa katika hatua tatu: awamu ya  kwanza ni masimulizi kuanzia (2021-2022 na 2022-2023); awamu ya hekima (2023-2024); tatu  awamu ya unabii (2025)”.

Mkutano mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia kwa ushiriki wa Papa Francisko mwezi Mei 2022

Katika Muhtasari huo unaripotiwa kwamba uhusika ulikuwa mpana na tofauti: kuanzia  kwa Makanisa mahalia katika matamshi yao (majimbo, parokia, maeneo ya kichungaji na katika sehemu zao zote, kwa juhudi za kufikia ulimwengu wa siasa, taaluma, shule na vyuo vikuu, hadi mahali pa mateso na matibabu, hali za upweke na kutengwa. Licha ya kutokuwa na uhakika na mashaka, hasa katika awamu ya kwanza, Makanisa nchini Italia yamejaribu kushinda ubinafsi, mashaka na vipingamizi na wameweka: kikundi cha uratibu wa kitaifa ambacho kimeanzishwa, na karibu vikundi 50,000 vya sinodi vimeundwa, na wawezeshaji wao, kwa ujumla vya ushiriki wa watu nusu milioni. Zaidi ya wawakilishi 400 wa majimbo waliratibu kazi hiyo, pamoja na timu zao. Kuna mihtasari 200 ya majimbo na 19 iliyofafanuliwa na vikundi vingine kwa jumla vya kurasa zaidi ya 1,500, iliyopokelewa na Sekretarieti Kuu ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI) mwishoni mwa mwezi Juni 2022. Michango mbalimbali iliyopokelewa haijatajwa kwa jina, lakini imeingizwa ndani ya maandishi katika utajiri na wingi wao.

Sio kuzungumzia sinodi tu lakini kuiishi

Katika mhutasari huo aidha unabainisha kwamba hawakuzungumza tu juu ya sinodi, lakini pia waliishi, kwa kuzingatia juhudi zisizoweza kuepukika kama vile katika kazi ya timu ya majimbo, mapadre, mashemasi, walei, wanaume na wanawake watawa pamoja, vijana na watu wazima, na ushiriki wa  Askofu, katika usindikizaji wa busara na bidii ya parokia na ukweli unaohusika, katika ubunifu wa kichungaji uliowekwa, katika uwezo wa kupanga, kuhakiki, kukusanya,na kurudishwa kwa jamii. Muhtasari huo kadhalika unasisitiza kwamba: “Uzoefu uliofanywa umekuwa wa kusisimua na wa kuzaa matunda kwa wale ambao wamekubali kuthubutu kwa kujihusisha katika mazingira mengi na imesaidia kuhuisha miili ya ushiriki wa kikanisa; imesaidia kugundua upya uwajibikaji unaotokana na hadhi ya ubatizo na imeruhusu uwezekano wa kushinda maono ya Kanisa lililojengwa karibu na huduma ya watu wa wakfu ili kuelekea kwenye Kanisa la 'huduma kamili', ambalo ni ushirika wa karama na huduma tofauti”.

Madhumuni kumi kutokana na tafakari za majimbo

Katika sehemu ya kati, hati inawasilisha madhumuni kumi ambayo  ni tafakari zilizoibuka kutoka kwa maandishi ya majimbo  yaliyopangwa kwa  kusikiliza, kukaribisha, mahusiano, kusherehekea, mawasiliano, kushirikisha, mazungumzo, nyumbani, vifungu vya maisha na mbinu.  Wingi wao, umebainishwa kuwa hauwakilishi kikomo cha kushindwa, kwa njia ya uendeshaji wa usawa au kiheararkia lakini kusaidia kuhifadhi wingi wa kimsingi wa uzoefu wa Makanisa nchini Italia, pamoja na aina mbalimbali za lafudhi na hisia ambazo zimevukwa na ambazo wao ni wabebaji. Upambanuzi juu ya miunganisho ya majimbo na ufafanuzi wa madhumuni kumi ulifanya iwezekane kubainisha baadhi ya vipaumbele ambavyo, kwa lengo la kulisha na kusaidia Njia ya Sinodi ya Makanisa nchini Italia kwa ushirikiano na mchakato unaoendelea katika ngazi ya ulimwengu.

Kuunganishwa misingi ya njia na kijiji, kishemasi na malezi ya kiroho

Vile vile, iliamuliwa, kuunganishwa pamoja kwa misingi mitatu inayofafanuliwa kama maeneo ya ujenzi wa sinodi ambapo awali ni njia na kijiji ambapo ni kwa (kusikiliza ulimwengu wa maisha, ule wa ukarimu na nyumba (ubora wa uhusiano na miundo ya kikanisa) na ile ya kishemasi na malezi ya kiroho. Maeneo haya ya ujenzi yanaweza kubadilishwa kwa uhuru na kila Kanisa mahalia na  litaweza kuongeza moja ya nne ambayo huongeza kipaumbele kutokana na njia iliyochukuliwa katika mwaka wa kwanza. Kwa mujibu wa mhutasari huo, inakumbusha kwamba ile ya ujenzi ni picha inayoonesha hitaji la kazi ambayo inadumu kwa wakati, na ambayo si ndogo ya kuzuiwa na mpangilio wa matukio, lakini inalenga utambuzi wa njia za kusikiliza na uzoefu wa sinodi iliyfanyiwa uzoefi, ambapo usomaji wake kwa upya ndio mahali pa kuanzia kwa awamu zitakazofuata za mchakato wa safari ya sinodi ya kitaifa ”.

20 August 2022, 12:23