Tafuta

2022.08.29 Picha ya pamoja mara baada ya misa ya kufunga kongamano la V la Viwawa ,Agosti 2022  huko Tabora, Tanzania. 2022.08.29 Picha ya pamoja mara baada ya misa ya kufunga kongamano la V la Viwawa ,Agosti 2022 huko Tabora, Tanzania. 

Kituo cha Vijana Nala-Dodoma:Vijana na waamini kuchangia kituo ili kuimarisha malezi na makuzi

“Ni muhimu kuwa na kituo cha vijana katika maelezi na makuzi yao,kama asemavyo Papa kwamba haijalishi uzoefu wa kibinadamu,maisha ya kiroho,hali ya uchumi na kijamii,utamaduni na shughuli zinazompatia kijana mahitaji yake msingi,kwani vijana wote wanakaribishwa ili kupyaisha imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake.Mwaliko kwa vijana wote ni kuchuchumilia utakatifu na maisha adili”.Hayo yalinukuliwa na Padre Minga Mratibu wa Vijana TEC,kwa Vatican News,mara baada ya Mkutano wa VIWAWA.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kongamano la Tano la Kitaifa la Vijana Wakatoliki Wafanyakazi Tanzania, (VIWAWA), lilihitimishwa hivi karibuni mnamo tarehe 8 Agosti 2022 ambalo lilifanyika katika Jimbo Kuu katoliki la Tabora Tanzania huku likiongozwa na kauli mbiu: “Simama nimekuteua uwe shahidi wa yale uliyoyaona.” (Mdo 26: 16).  Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican ikizungumza na Padre Adolf Minga, Mratibu  wa Vijana, Baraza la Maaskofu Tanzania TEC, mara baada ya Mkutano huo, alisema  kwamba mkutano huo ulikuwa awali ya yote ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai na Utume aliowapatia Mungu. Kuona wapi wamefaulu na wapi wameshindwa. Ni vema kuwasaidia vijana wengi kwa kila njia katika kujikwamua na maisha yao kiroho na kimwili hasa katika kukutana kwa pamoja.  Na ni muhimu kuwa na kituo cha vijana katika maelezi na makuzi. Padre Minga alisema “Hii ni kama asemavyo Papa Francisko kwamba “haijalishi uzoefu wa kibinadamu, maisha ya kiroho, hali ya uchumi na kijamii, utamaduni na shughuli zinazompatia kijana mahitaji yake msingi, kwani vijana wote wanakaribishwa ili kupyaisha imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Mwaliko kwa vijana wote ni kuchuchumilia utakatifu na maisha adili”.

Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora

Akiendelea na ufafanuzi zaidi Padre Minga alieleza  jinsi ambavyo kwa neema ya Mungu, maudhurio hata kwa mwaka huu yalikuwa mazuri na muhimu kwani vijana wapatao 2500 kutoka majimbo yote 34 katoliki Tanzania waliweza kufika. Mada zilizotelewa zilikuwa ni kama zifuatavyo: Kijana ni shahidi wa Yesu; Uzalendo na siasa; kilimo cha kisasa; Athari za Ushirikina kwa vijana; Vijana na Utandawazi; Vijana na Ujasiliamali; Vijana na maisha yangu; na hatimaye  vijana na maamuzi stahiki.  Wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Misa iliongozwa na Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki la Singida  ambaye ni Mwenyekiti wa Idara ya Utume wa Walei  Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC), wakati huo huo Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, akisaidiana na Askofu Eusebius Alfred Nzigilwa wa Jimbo Katoliki  la Mpanda walifunga tukio hilo, na  mgeni  rasimi alikuwa ni  Mheshimiwa Innocent Bashungwa, Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), na kuudhuriwa na  waamini Watu wa Mungu, Walezi wa vijana wa kutosha,  viongozi mbali mbali wa dini na  serikali na waalikwa kutoka nchi za nje kama vile: Burundi, Rwanda, Ivory Coast, Ethiopia, Malawi, Kenya, Uganda pamoja na Italia. Mkutano ujao wa VIWAWA unatarajiwa kufanyika mnamo mwaka 2025. Katika mkutano wao  kwa mujibu wa Padre Minga amethibitisha kuwa wamejiwekea malengo ya kufikia hasa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha vijana NALA–Dodoma katika Mji Mkuu wa Tanzania.

Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora

Kuhusiana na kituo hicho Padre Minga amewasilisha  kwa vyombo vya habari Vatican, (Idhaa ya Kiswahili) Barua iliyoandikwa na Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki la Singida ambaye ni Mwenyekiti wa Idara ya Utume wa Walei Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC. Kwa mujibu wa barua hiyo iliyoelekezwa kwa :wakurugenzi na Walezi wa vijana Jimbo(VIWAWA;TYCS; TMCS  na SKAUTI KATOLIKI);  Mkurugenzi wa Walei Jimbo, Mwenyekiti wa Walei Jimbo;  vijana wote na waamini wote wa Mungu, kuhusu kuomba mchango kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. Askofu Mapunda katika barua iliyoandikwa mwanzoni mwa mwaka huu 2022 inabainisha kwamba: “Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwa kutambua umuhimu wa kijana katika Kanisa, limeona yafaa kuwa na huduma ya vijana inayojitosheleza ambapo vijana wataimarishwa zaidi kiroho, kiimani na kupata majibu ya maswali mbali mbali katika maisha yao ya kutumikia Mungu”.

Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora

Hata hivyo Askofu Mpunda katika barua hiyo pia alibainisha jinsi ambavyo- “vijana hao kwa juhudi zao wenyewe waliweza kununua ekari 8 za kiwanja huko Nala Dodoma na kuwa na Hati miliki ili kujibu kiu ya vijana”. Kwa maana hiyo “Katika mkutano wa 77 wa Maaskofu kwa sauti moja walikubaliana kuazimia kupitia Idara ya vijana  kwamba kila kijana waweze kuchangia kiasi cha kima cha chini kabisa cha shilingi elfu moja kabla ya mwezi Septemba mwaka huu 2022”.  Kutokana na hilo, Mratibu wa Vijana Kitaifa amehimiza  tena kwamba “Mwezi Septemba unakaribia, na kwa yule ambaye bado hajafanya hivyo, basi ni wakati hajachelewa, anakumbushwa kufanya hivyo”. Katika barua hiyo pia inaelezea jinsi ambvyo mchango huo utakavyotumika kwamba: “Kwa mchango utakaopatikana ni kwa ajili ya kujenga Holi la Mikutano, kujenga Hostel, jengo la Utawala, kujenga fensi ya eneo, ujenzi wa Kanisa na kutengeneza viwanja vya mpira na mengineyo muhimu kwa ajili ya vijana”.

Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora

Makadirio ya ujenzi huo yalikuwa ni bilioni tano, hivyo  Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania, waliweza kuteuwa hata  Dominika moja ambayo iweze kutumika katika kutoa  mchango  kwa ajili ya idara ya vijana Kitaifa na ambayo walionelea ifanyike  kitaifa katika “Sherehe za Bwana Wetu Yesu Kristo Mfalme”, itakayofanyika  mnamo tarehe 20 Novemba 2022. Kwa njia hiyo kila mmoja anaalikwa kuchangia kwa ukarimu wake na  kwamba sadaka yote kwa siku hiyo iweze kuchangia kituo hicho cha vijana na utume wa vijana. Katika barua hiyo aidha inaweka maelekezo muhimu ya uwasilishaji wa fedha kwa kila jimbo.

Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora
Mkutano wa V Kitaifa wa VIWAWA Tanzania Agosti 2022 huko Tabora

Katika mahojiano hayo na  Padre Adolf anakumbusha tena na tena kwa dhati juu ya uchangiaji huo wa kwanza wa vijana wote  shilingi elfu moja na  kwa kila mwaamini  mwenye mapenzi mema ili kufikia Mwezi unaoanza Septemba 2022 uwe umekamilisha, na wakati huo huo kujiandalia na uchangiaji kitaifa kwa siku iliyopangwa na maaskofu, “ili kuweza kufikisha lengo hili muhimu na ufanisi wa vijana wetu wa Kanisa letu, la leo na kesho na kwa Taifa zima, ili  kuwa na kituo chao muhimu cha makutano”. Kwa kuongezea Padre Minga alisema: “Shukrani kuu kwa Mgeni rasmi wa kufungua Mkutano huo, Mh. David Mwakiposa Kihenzile, Rais wa Msalaba Mwekundu,Tanzania na Mbunge wa Mufindi ambaye alichangia milioni mbili kwa ajili ya kituo na Waziri Bashungwa ambaye kwa siku ya kufunga mkutano huo alitoa shilingi milioni tano kwa ajili ya kituo hicho. Padre Minga kwa kuhitimisha alisema: “ili kituo kikamilike milioni 21 zinahitajika kwa awamu ya kwanza, mwanzoni mwa mwaka huu 2022, ambapo tunahitaji milioni tano ambazo ni kuanzia kazi”.

KONGAMANO LA V LA VIWAWA TANZANIA 2022
29 August 2022, 17:14