Tafuta

Raia wameandamana kufuatia na tukio la Mamlaka ya Nchi kumwondoa Uaskofuni Askofu wao Rolando Alvarez  wa Nicaraguan Raia wameandamana kufuatia na tukio la Mamlaka ya Nchi kumwondoa Uaskofuni Askofu wao Rolando Alvarez wa Nicaraguan  

Nicaragua:Polisi na mawakala wa kijeshi wamwondoa Askofu Álvarez kwa nguvu uaskofuni!

Askofu Rolando José Álvarez ameondolewa kwa nguvu usiku katika makao ya kiaskofu ya Matagalpa mahali alipokuwa kifungo cha nyumbani na mapadre na walei tangu mwanzo wa mwezi huu.Polisi walimpeleka na wenzake huko Managua.Jambo ambalo limeibua mara moja maandamano ya raia na mshikamano na askofu alikutana na Kardinali Leopoldo Brenes,Askofu Mkuu wa Managua.Wasiwasi pia wa Katibu Mkuu wa UN,Bwana Guterres.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katikati ya usiku, wa tarehe 18 Agosti 2022 vikosi vya polisi na mawakala wa kijeshi wa Nikaragua walivamia jengo la kiaskofu la jimbo katoliki la Matagalpa, ambapo Askofu Rolando José Álvarez na baadhi ya mapadre, waseminari na walei walikuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu tarehe 4 Agosti 2022. Mawakala hao waliwachukua kwa nguvu watu 9, akiwemo askofu, kulingana na baadhi ya mashahidi, katika msafara wa magari manane. Jimbo lenyewe kwenye mitandao ya kijamii lilitoa taarifa ambayo ilizua taharuki kwa raia. Mamia ya watu, waliposikia kengele za Kanisa zikilia huku polisi wakivamia Uaskofuni walikaribia kujaribu kumlinda askofu huyo na wengine. Katika taarifa ya polisi imebainishwa kuwa Askfofu Alvarez, kama watu wengine wote waliokamatwa, walipelekwa Managua, Askofu huyo akiwa chini ya kizuizi cha nyumbani katika makazi yake ya kibinafsi na wengine 8 kwenye kambi ya polisi kwa uchunguzi.

Mkutano na Kardinali Brenes

Kardinali Leopoldo Brenes, askofu mkuu wa Managua na makamu rais wa Baraza la Maaskofu wa Nikaragua, aliweza kumtembelea Askofu Álvarez na kufanya naye mazungumzo marefu. Hali yake ya kimwili imezorota, lakini Jimbo Kuu la  Managua baadaye lilisema katika taarifa, kwamba  roho yake na ari yake ni imara. “Tunafahamu kwamba maombi ni nguvu ya Mkristo  na tunakualika kuendelea kumwomba Kristo ili kuliombea na kulichunga kundi lake hili dogo. Tunatumaini kwamba sababu na kuelewana vitafungua njia kwa ajili ya ufumbuzi wa hali ngumu na ngumu kwa kila mtu”,  tamko hilo linasema na  kwamba  ni vema kuwa na  Mshikamano na Kanisa nchini Nicaragua baada ya mashambulizi dhidi ya uhuru wa kujieleza".

Wasiwasi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Guterres,amesikitishwa sana na kizuizi kikubwa cha nafasi ya demokrasia na kiraia nchini Nicaragua na hatua za hivi karibuni dhidi ya mashirika ya kiraia, ikiwa ni pamoja na yale ya Kanisa Katoliki, kama vile uvamizi wa kiti cha maaskofu huko Matagalpa. Hiki ndicho Farhan Haq,msemaji wake alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Umoja wa Mataifa. Bwana Guterres,  aliendelea msemaji  wake kwamba  anasisitiza wito wake kwa serikali ya Daniel Ortega kuhakikisha kulindwa kwa haki za binadamu za raia wote, hasa haki za ulimwengu kwa wote,  mkutano wa amani, uhuru wa kujumuika, mawazo, dhamiri na dini na wito wa kuachiliwa kwa watu wote waliozuiliwa kiholela. Hatua hiyo pia ililaaniwa na Katibu wa Umoja wa Nchi za Marekani (OAS), Luis Almagro.

Mshikamano kwa Askofu  Álvarez

Askofu  José Domingo Ulloa, Askofu Mkuu wa Panama, katika taarifa yake kwa Vatican News, alifafanua kile kilichotokea kama kigeugeu na sababu ya hofu na maumivu kwa Kanisa zima la Amerika ya Kusini. Askofu wa Panama anaungana  na sauti ambazo wanaomba mara moja kuachiliwa kwa Askofu Rolando na heshima kwa hadhi yake kama mtu na kama mchungaji wa Kikatoliki. Hatimaye, Askofu Ulloa aliinua sala mbinguni kwa ajili ya Nikaragua, watu wake wa heshima na Kanisa lake ambalo leo linakabiliwa na mateso.  Kwa upande wake, Kituo cha Nicaragua Haki za Kibinadamu zililaani shambulio dhidi ya Baraza la Maaskofu wa Matagalpa na kukamwatwa kwa Askofu Rolando Álvarez na makuhani wengine na walei walioandamana naye, wakitaka heshima kwa uadilifu wao binafsi na maisha yao.

Ni matukio ya hivi karibuni tu katika mfululizo wa matendo ya mateso

Katika tukio hili ujumbe  mwingi wa mshikamano na udugu umefikia Kanisa la Nikaragua katika siku za hivi karibuni: kutoka kwa Mabaraza ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini na kutoka na Vatican. Miongoni mwa mengine, Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika Kusini (Celam),  Costa Rica, Guatemala, Honduras, Bolivia, Mexico, Uruguay, Ecuador, Brazil, Peru, Colombia na Argentina wameshutumu vikali uadui unaoongezeka wa serikali dhidi ya Kanisa na kuhimiza kujenga amani. Kitendo cha nguvu cha usiku wa leo ni cha hivi punde zaidi katika mfululizo wa ishara za mateso dhidi ya Kanisa Katoliki nchini Nicaragua linalotuhumiwa kuunga mkono wapinzani wa serikali ya Sandinista ya Daniel Ortega.

KANISA LA NICARAGUA LINATESWA
20 August 2022, 09:16