Tafuta

2022.08.17 Sr Yasintha Godfrey Kala,(SDS)Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Mungu Mwokozi(SDS)kushoto akiwa na Sr.Petronilla Mkagoa SDS katika Makao Makuu ya Shirika huko Masasi Tanzania 2022.08.17 Sr Yasintha Godfrey Kala,(SDS)Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Mungu Mwokozi(SDS)kushoto akiwa na Sr.Petronilla Mkagoa SDS katika Makao Makuu ya Shirika huko Masasi Tanzania 

Sr.Yasintha,SDS:Karama yetu ni kufanya wema na upendo wa Yesu Mwokozi ujulikane!

Shirika la Mungu Mwokozi(SDS lilianzishwa na Mwenyeheri Francis Maria wa Msalaba Jordan,likiwa na matawi matatatu:mapadre na mabruda(1881),watawa wa kike Wasalvatoriani(1888).Karama yao ni kufanya wema na upendo wa Yesu Kristo Mwokozi wa dunia ujulikane.Haya yalithibitishwa na Sr.Yasintha Godfrey Kala(SDS)Mama Mkuu wa Shirika la masista wa Mungu Mwokozi,Tanzania katika mahojiano na Vatican News.

Na Sr. Angella Rwezaula - Vatican.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican hivi karibuni ilikutana na kuzungumza na Sr. Yasintha Godfrey Kala ambaye ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Mungu mwokozi(SDS) kwa upande wa Tanzania ambapo katika mahojiano hayo alifafanua juu ya shirika lao kuwa lilianzishwa na Mwenyeheri Francis Maria wa Msalaba Jordan, likiwa na matawi matatu ya Mapadre na Mabruda wasalvatorian mnamo mwaka 1881 na baadaye masisita wasalvatoriani mnamo mwaka 1888 na baadaye wasalvatorian walei walianzishwa. Mwanzilishi wao aliguswa sana na kufungu cha Kibiblia kutoka Mwinjili Yohane 17, 3 ambapo karama yao inachotwa humo isemayo: "Kufanya wema wa Yesu Kristo Mwokozi wa Dunina ujulikane kwa watu wote, sehemu zote na kwa namna yoyote ile ambayo roho wa Mungu anawaongoza".

Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa SDS Tanzania Sy Yasintha na Sr Petronilla Mkagoa SDS
Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa SDS Tanzania Sy Yasintha na Sr Petronilla Mkagoa SDS

Sr. Assuntha kwa ufafanuzi zaidi kuhusu shirika hilo alisema kwa upande wa Tanzania shirika lao lilianzishwa mnamo mwaka 1957, ambapo masisita wao wa kwanza walifikia katika  sehemu mmoja iitwayo Mnero, ambayo kwa wakati huo lilikuwa ni katika jimbo la Nachingwea na baadaye walikwenda Masasi, Tanzania ambapo tayari jimbo lilikuwa limebadilika na kuitwa jimbo la Tunduru Masasi. Kuhusu idadi ya watawa na sehemu zao za utume, Mama Mkuu wa shirika la masisita Wasalvatoriani Tanzania alisema kwa sasa ni masisitia 69 na kuna wengi waliotangulia mbele ya haki ya Mungu lakini walio hai ni 69 na wanafanya utume katika majimbo manne: Jimbo la Tunduru Masasi, Jimbo la Mbinga, Jimbo la Mahenge na Jimbo Kuu la Dar Es Salaam Tanzania.

Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa SDS Tanzania Sy Yasintha na Sr Petronilla Mkagoa SDS
Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa SDS Tanzania Sy Yasintha na Sr Petronilla Mkagoa SDS

Hata hivyo wako pia nje ya Nchi kama vile Kenya, katika jimbo katoliki la Kakamenga ambao kuna masisita wanafanya utume huko pia wana nyumba nyingine jijini Nairobi. Nyumba hiyo ina masista Wasalvatoriani mchanganyiko kutoka Tanzania, Congo na Msumbiji. Hao wanakaa hapo lakini pia wakiwa masomoni katika vyuo mbali mbali na kozi. Kadhalika masisita hawa wana nyumba au jumuiya 15 nchini Tanzania. Hivi karibuni wamefungua hata nyumba nyingine mpya ya utume huko Angola ambbapo kuna masisita na wengine wanatarajia kwenda huko kuwaunga mkono. Watawa hao wanafanya kazi na jumuiya hiyo inatakuwa  vile vile mchanganyiko wa watawa kutoka Tanzania na Congo ili kuishi pamoja katika utume wao wa hospitalini na kufundisha dini. Sr. Yasintha pamoja na kuelezea shughuli hizo pia amefafanua kipengeleza kingine kinachohusu miito ambayo ni zawadi kutoka kwa Bwana kwamba, kwa upande huo wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwani wapo wafuasi ambao wanawafuata na kuwa kama inavyojulikana uhai wa shirika lolote lile unategemea na wanachama wapya ambao wanajiunga". Kwa njia hiyo wanaweza kumshukuru Mungu kuwa wapo, wanafuata nyuma na wataendeleza shirika. Kwa sasa wanao manovisi 11, mapostulanti 6 na kandidate 22  na wote hao wako katika nyumba za malezi wakielendelea kufundwa.

Mwanzilishi wa Shirika la Mungu Mwokozi Mwenyeheri Francis Maria wa Msalaba
Mwanzilishi wa Shirika la Mungu Mwokozi Mwenyeheri Francis Maria wa Msalaba

Mama Makuu akijikita juu ya utume wao kwa ujumla ni huduma ya wagonjwa, mahospitalini, kufundisha dini shuleni na shughuli za kichugaji kama vile kufundisha katekesi shuleni  na shughuli nyingine za kichungaji, pia hata kutoa huduma kwa watoto wale wanaoishi katika mazingira magumu na ndiyo maana wao wanayo hosteli Masasi, Tanzania ambapo kuna wasichana wanaoishi hapo na ndilo lengo hasa kwa ajili ya watoto wa kike na jengo hilo lilijengwa kwa ajili yao ili kuwasaidia wale ambao wanakosa nafasi ya kwenda shule za bweni kutokana na wazazi wao kukosa uwezo. Sr. Yasintha alieleza kwamba wasichana hao wanafika na kukaa hapo kwa kasaidiwa kila kitu hata kuwalipia gharama. Hata hivyo kuna watoto pia ambao wanasaidiwa na watawa wakiwa kwa wazazi wao, hiyo ni kutokana kukosa Hosteli ya kiume na hawawezi kuwabagua wakati wanahitaji msaada.

Pamoja na kuelezea mafanikio hayo  Mama Mku hakukosa kuelezea hata changamoto ambazo wanakabiliana na kwamba kama ilivyo kila sehemu yoyote ile haikosi changamoto,  na kwa maana hiyo kama shirika wana changamoto hasa zile zinazotokana na utandawazi. Kwa njia hiyo suala hili linawaathiri kama watawa kwa sababu amesema, kwa sasa vijana wanaowapokea ni vijana ambao wako kimtandao zaidi, wanafahamu kutumia simu, wamezaliwa na  wamezikuta, wanafahamu kuzutumia kwa vyovyote vile na kuwa na uwezo.  wakati huo huo wanapo jiunga na shirika utakuta Mlezi mwenyewe anachokijua ni kupiga na kupokea simu tu, mambo mengine hajuhi. Kwa maana hiyo Sr  Yasintha alisema kuwa "kumuunda kijana huyo ambaye amejiunga nao ili aweze kufuata mfumo wao wa maisha ya kitawa inakuwa ni changamoto na inachukua muda".

Sr Petronilla Mukagoa, Sr Laurina Kokutona,Papa Paulo VI na Kardinali Lauriane Rugambwa
Sr Petronilla Mukagoa, Sr Laurina Kokutona,Papa Paulo VI na Kardinali Lauriane Rugambwa

Kwa upande wa changamoto nyingine ni kuhusiana na mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa ambapo pia yanaathiri uchumi na mpangilio mzima wa maisha yao kama watawa. Kwa ufafanuzi zaidi juu ya hilo Mama Mkuu alibainisha,  kwa mfano wakiangalia wanapo badilisha viongozi wa kisiasa, mabadiliko yanaathiri katika uendeshaji wa Taaisi zao kama shule na mahospitali. "Akija huyo anasema hili; na inapokuwa sasa imezoeleka anapofika mwingine anafika na mikakati yake, lakini katika mikakati hiyo kama shirika wakati mwingine unakuta tunaumia kwenye uendeshaji wa shule hizo au taasisi nyingine yoyote na hiyo kiukweli katika shirika letu ni changamoto". Mama Mkuu wa Shirika la Masista Wasalvatoriani alisema kwamba changamoto nyingine zipo kama kawaida japokuwa zinakuwa ndani ya uwezo wao ambapo wanaweza kuzitatua.

Tukio la 2022 kwa wasalvatoriani mwaka wa shukrani kutangazwa mwenyeheri Francis Maria wa Msalaba

Katika shirika lao kama Wasalvatoriani kwa mwaka huu wamekuwa na kumbukizi muhimu kwa sababu, Mwanzilishi wao wa Shirika alitangazwa kuwa mwenyeheri mnamo tarehe 15 Mei 2021 na kama shirika walijiwekea kufanya Mwaka wa kutoa shukurani na kilele cha kuhitimishwa ilikuwa ni tarehe 21 Julai 2022. Kwa mwaka mzima, Sr Yassintha alisema umekuwa wa kutoa shukrani kwa namna mbali mbali kama vile kufanya mafungo, matendo ya huruma, ili kumshukuru Mungu kwa neema na baraka ambazo amewajalia na makuu hayo ambayo amekirimia shirika lao kwa sababu waliongojea kwa kipindi  kirefu na hatimaye mwanzilishi wao akatangazwa kuwa mwenyeheri.

Katika kuhitimisha mahojiano na Vatican News, Mama Mkuu wa Shirika la Masisita wa Mungu Mwokozi (SDS) Tanzania alitoa ushauri  kwa wasikilizaji wa Vatican News kwamba watembee kwa pamoja kisinodi kama mwaliko wa mababa wa Kanisa kuwa kila mmoja atimize wajibu wake, lakini pia hasa kutambua umuhimu wa kila mmoja katika uhai wa Kanisa na wanakanisa zima. Sr Yasintha aliwaalika pia watu wote kuwaombe viongozi wa Kanisa kwamba wako katika kipindi kigumu cha Sayansi a Teknolojia,  hivyo wanahitaji sala zetu, kama waamini ili kuungana pamoja kuwaombe kama vile  Musa alivyo kuwa akiwaombea wana wa Israeli: Alikuwa anananua mikono juu kuwaombea na wao walishinda katika vita na alipokuwa  akichoka kwa kushusha mikono yake walipigwa na maadui zao; na wenzake wakagundua jinsi ambavyo walipaswa kusaidia wakatengeneza mwinuko kama matofali ili asichoke kuinua mikono na ndipo wakashinda (rej Kut 17,8-16). "Hivyo hivyo nasi viongozi wetu kuna mahali wanaweza wakachoka, tusipende kuwalaumu, kuangalia zaidi mabaya yao, lakini tupige magoti kumwomba Mungu awasaidie ili Mungu naye asikilize sala na sadaka zao ambazo wanatoa kwa ajili yetu". Mama Mkuu aliongeza kusema kwamba huo ndio ushauri aliopenda kuwashauri wasilikizaji.

MAHOJIANO NA SR YASINTHA (SDS) MAMA MKUU WA SHIRIKA LA WASALVATORIANI TANZANIA
17 August 2022, 16:32