2022.08.30 Mama Teresa: Hakuna upendo ulio mkuu, ndio kichwa cha filamu  ya historia yake 2022.08.30 Mama Teresa: Hakuna upendo ulio mkuu, ndio kichwa cha filamu ya historia yake  

No Greater Love ni Filamu ya mama Teresa ili kujifunza historia yake!

Shirika la Kijeshi liitwalo 'Knights of Columbus' limetoa filamu kuhusu Mama Teresa.Filamu hiyo inaongozwa na kichwa"No Greater Love” yaani “hakuna upendo ulio mkubwa”.Ina nyenzo za video ambazo hazijawahi kutolewa,kwa kutoa maelezo ya kina na matokeo ya historia ambayo kwa hakika inaonekana kutojulikana sana.Nia ya filamu ni kuonesha pia wito wake,lakini pia utume wa wake unavyoendelea bado ulimwenguni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Inaonekana ni vigumu kuongeza chochote kwenye wasifu na historia nyingi kuhusu Mama Teresa wa Calcutta. Lakini filamu ya No Greater Love yaani "hakuna upendo ulio mkuu zaidi” iliyotayarishwa na  Shirika la Kijeshi, “Knights of Columbus” na kuwasilishwa  jijini Roma mnamo tarehe 31 Agosti 2022 mara baada ya onesho la kwanza katika Chuo cha Amerika Kaskazini mnamo tarehe 29 Agosti iliyopita, ina faida ya kutoa undani zaidi kwa historia inayojulikana,  lakini ambayo  hajasimuliwa vya kutosha na  kwa  kina. Filamu hiyo imegawanywa katika sura zinazoelezea nyakati muhimu za maisha ya Mama Teresa, iliyogawanyika na mahojiano na wamisionari wa kike na kiume wa Upendo;  wasifu wa Mama Teresa, na  wakati huo huo filamu sio tu uchunguzi wa maisha ya mtakatifu, lakini pia inatoa mtazamo wa jumla wa maisha ya mtakatifu huyo kuanzia na  kazi kubwa ambayo Wamisionari wa Upendo walioasisiwa na Mama Teresa duniani kote , kwa mfano  huko Brazili, katika mashamba ya mpaka kati ya Mexico na Marekani, nchini Ufilippini na kwingineko.

Mama Teresa wa Kalkuta
Mama Teresa wa Kalkuta

Historia ya Mama Teresa kiukweli inajulikana kwani alizaliwa huko Skopje katika familia ya Waalbania, ya watu walio wachache katika lundo la Kibalkani. Mama Teresa akiwa kijana alihisi msukumo wa kuwa mmisionari hivyo alijiunga na Masista wa Loreto na akaondoka kwenda nchini India, ambapo alianza kufanya kazi kama mwalimu. Ilikuwa baada ya hali halisi ya kushangaza na hali halisi ya ndani, katika mitaa, baada ya ghasia huko Calcutta, ambapo aliweza kutambua kwamba dhamira yake ilikuwa awali ya yote kuwa upande wa maskini. Hakika, pamoja na maskini zaidi, kwa sababu hiyo ilikuwa kigezo cha jumla. Kutoka na  wito huo ndipo ilizaliwa  kazi ambayo imechimba mizizi duniani kote, ambayo inaanzia kwenye vitongoji vilivyo  duni kabisa vya Calcutta na kuenea hadi Bronx na katika utunzaji wa watu wa mwishoni wa karne iliyopita na sasa kama vile, wagonjwa wa UKIMWI walitengwa, na kama walivyokuwa hata wenye ukoma wakati wa kipindi cha Yesu. Hii ni kazi ya kimya na muhimu, inayotambuliwa na ulimwengu wote. Mnamo 1979, Mama Teresa alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel, na huko Oslo alitoa hotuba ya kugusa moyo ambapo alishutumu mataifa ambayo yanahalalisha utoaji mimba kama maskini zaidi.

Mama Teresa wa Kalkuta
Mama Teresa wa Kalkuta

Na  baadaye kuna urafiki wa kina na Mtakatifu Yohane Paulo wa II, ambaye alitaka uwepo wa  nyumba ya Wamisionari wa Upendo ifunguliwe moja kwa moja jijini Vatican na  ambayo bado wamo hadi leo hii. Lakini hata hiyo katika historia yake, hapakosekani marejeo ya giza la roho, kwa maana ya nyakati za shida ya kiroho ambapo kwa wale wote walioitwa kwenye maisha ya utakatifu kadhalika wanapitia. Hata hivyo kile ambacho ni cha nguvu zaidi katika filamu hiyo juu ya yote ni picha kama lazima zinavyopaswa kuwa. Na hii ni kwa sababu watayarishaji waliweza kupata ufikiaji kamili wa hifadhi ya Wamisionari wa Upendo, pia kupata filamu ambazo hazijachapishwa au zisizojulikana sana, ambayo ni pamoja na ile ya Mama Teresa mhudumu wa ajabu wa Ekaristi.

Siku ya Kutangazwa Mtakatifu Mama Teresa wa Kalkuta
Siku ya Kutangazwa Mtakatifu Mama Teresa wa Kalkuta

Patrick Kelly, Mkuu wa Shurika la Ndugu wa Huduma wa Columbus amesisitiza kwamba filamu hiyo ilizaliwa “shukrani kwa uhusiano wa uaminifu kati ya Shirika hilo (Knights of Columbus) na Wamisinari wa Upendo (Missionaries of Charity”). Zaidi ya hayo yote, Virgil Dechant, mtangulizi wake Kelly kama Mkuu wa Shirika hilo alikuwa rafiki wa kibinafsi wa Mama Teresa, na kutoka hapo ushirikiano ulianza, kwa kuzingatia kwamba upendo huo ndiyo kanuni msingi ya Shirika hilo  (Knights of Columbus”. Katika barua iliyotumwa kwa Kelly,  Mkuu wa shirika hilo, Papa Francisko alishukuru kwa mipango ambayo inasaidia, kwa njia ya ubunifu, kufanya bidii ya uinjilishaji kupatikana hasa kwa vizazi vipya.

Siku ya Kutangazwa Mtakatifu Mama Teresa wa Kalkuta
Siku ya Kutangazwa Mtakatifu Mama Teresa wa Kalkuta

Naye Kardinali Sean O'Malley, askofu mkuu wa Boston, nchini Marekani katika uwakilishi wa filamu hiyo alisimulia historia ya Padre ambaye, mara baada ya kufa, alitaka kuona kuzimu na ambaye baada ya kufika huko alikuta kila kitu kimepangwa vizuri na kutulia. “Si kufikiria kama kila kitu kingekuwa hivi kizuri sana”, alisema huyo mtu baada ya kufika huko. Lakini jibu likuwa kwamba:  “Haikuwa hivyo hadi watawa walipofika”.....  Kardinali alisema hii ni  historia ambayo kimsingi inaelezea heshima na mazingatio ambayo kazi ya Wamisionari wa Upendo wanafurahisha kwa huduma yao. Kadinali O'Malley pia alikumbusha kuwa alikutana na Mama Teresa alipokuwa mseminari, na kwamba alikuwa na mashaka ya kwenda, lakini kisha akaenda akifikiri kwamba kungekuwa na watu wachache. Na pale kulikuwa na mwanamke huyo mdogo, aliyevaa kama mwanamke wa Kihindi, mwenye sari na Kadinali alifungua kikao kwa sala, na mwanamke huyo akathibitisha jinsi alivyokutana na Mama Teresa katika mojawapo ya makazi duni ya Calcutta, kwa kujieleza yeye binafasi. Kardinali kwa hakika  alivutiwa na mwanamke huyo mdogo yaani Teresa wa Calcutta.

Mama Teresa na Papa Yohane Paulo mnamo 25 Mei 1983
Mama Teresa na Papa Yohane Paulo mnamo 25 Mei 1983

Alipoteuliwa kuwa askofu wa Fall River, katika wakati mgumu sana katika maisha ya Kanisa, Kardinali O'Malley amebainisha alimwandikia Mama Teresa, ambaye tayari alikuwa ametuma Wamisionari wake katika jimbo alilopitia na aliwaomba watawa wake wengine walete uponyaji na faraja na mara moja,  watawa  walifika katika Fall River, na baadaye Mama Teresa akaja kuwatembelea. Ziara hiyo ilikuwa tukio kubwa kwani maelfu ya watu waliingia mitaani kumkaribisha. Kardinali O’Malley alihitimisha kwa kusema kwamba: “Wito wake umegusa maisha ya kiroho ya watu wengi”. Naye Padre Brian Kolodiejchuk, msimamizi wa Mchakato wa kutangazwa kuwa mtakatifu kwa Mama Teresa, alisisitiza kuwa filamu hiyo inasaidia kukumbusha kazi kubwa na wito wa mama huyo na kwamba inatoa ujumbe kuwa "Calcutta iko kila mahali, kwa sababu kila mahali kuna maskini zaidi na huko, kazi ya upendo inapaswa kutendeka". Wakati huo huo naye Sista Myriam Therese, mkuu wa kanda wa Wamisionari wa Upendo, alisema kwamba "inapendeza kuona watu waliobadilisha maisha yao kwa sababu wamezungukwa na upendo wa Mungu" na kwamba "Mama Teresa ni mbeba upendo huo". Naye David Naglieri, ambaye aliongoza filamu hiyo, alisema kwamba hawakutaka wasifu, tu bali walitaka kuonesha wito wake wa kina, lakini pia kuonesha jinsi gani utume wa Mama Teresa unavyoendelea ulimwenguni kote.

MAMA TERESA WA KALKUTA
01 September 2022, 16:04