Tafuta

Vijana wanauchumi wako Assisi katika tukio la  "Economy of Francesco" Vijana wanauchumi wako Assisi katika tukio la "Economy of Francesco" 

Prof.Bruni:Assisi,vijana wanaonesha matumaini ya wakati ujao ulio bora!

Profesa Luigino Bruni,mkurugenzi wa kisayansi wa tukio la “Uchumi wa Francisko” anathibitisha katika vipaza sauti vya Vatican News kwamba mpango unaoombwa na Papa sio tangazo tu,lakini ukweli. "Unaweza kuona kinachotokea shukrani kwa vijana wa Amerika Kusini na barani Afrika ".

Na Angella Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko anaratajia kwenda Assisi, Jumamosi tarehe 24 Septemba kuunganika na washiriki wa Tukio la Uchumi wa Francisko, Harakati iliyoanziwa kwa msukumo wake, ambapo ni vijana 1000 waliounganika kutoka nchi 120 ulimwenguni.  Hawa ni wajasiriamali vijana na wachumi, wenye lengo la kutoa roho mpya kwa ajili ya uchumi kwa kutaka kutengeneza michakato ya ujumuishaji.  

Economy of Francisko
Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022
Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022

Siku ya kwanza ya “Uchumi wa Francisko! huko Assisi Septemba 22,2022 ilifunguliwa kwa mfululizo wa mijadala na meza za mduara kutoka pande zote ili kuwasilisha mavuno, yaani kile ambacho  kimefanywa kutokana na mipango iliyofanywa duniani kote ili kushughulikia masuala ya kiuchumi na changamoto za kisasa. Wanauchumi vijana na wajasiriamali walishiriki mbegu na matunda yaliyotawanyika katika kanda mbalimbali za sayari.

Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022
Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022

Hayo ndiyo aliyosisitiza  Profesa Luigino Bruni, mkurugenzi wa kisayansi wa Uchumi wa Francisko katika vipaza sauti vya Vatican News, akizungumza kuwa Harakati ya kimataifa iliyozaliwa kwa msukumo wa Papa Francisko iko wazi kwa wote, kwa mchango wowote ule unaokwenda katika mwelekeo wa amani na haki.

Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022
Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022

Akifafanua kuhusu roho aliyoishi wakati wa ufunguzu wa ‘Uchumi wa Francisko’, Frofesa Luigino alisema kwamba shukrani nyingi na zisizo na kikomo kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwaamini vijana hawa. Papa ni mmoja wa wachache duniani wanaofanya hivyo. Kiuhalisia kila mtu anaongelea vijana lakini vijana wako nje ya maeneo muhimu katika jamii ya leo hii. Hivyo shukrani kubwa kwa Papa na furaha yake  binafsi kuona jinsi shauku  imekuwa kitu zaidi ya matarajio yote. Na ni ajabu kuona vijana hawa 1000 wa dunia wakiwa pamoja na kuona kwamba  wakati uliopita Ulaya iliyofungwa na utaifa, na ambayo inajifunga yenyewe katika vita. Vijana wanataka zaidi, kwani wanataka kukutana, amani na udugu. Kuna matumaini makubwa ya mustakabali mwema kutokana na vijana.

Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022
Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022

Na kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi (CO2) ndio mwongozo unaoongoza uchaguzi wa mpango wa "Uhifadhi wa Uumbaji" katika muktadha wa Uchumi wa Francisko. Mkuu wa mpango huo, Giuseppe Lanzi, amekumbuka baadhi ya chaguzi madhubuti zinazoambatana na hafla iliyopangwa katika jiji la Umbrian hadi Septemba 24, kwa mfano, alisema hawahatumii chupa za plastiki, watumii nyenzo za kutupwa. Badala yake wamewapati vijana chupa na kuna vitoa maji vya kujaza. Kwa chakula wamefanya uchaguzi sahihi, vyakula vinatoka katika maeneo ya tetemeko la ardhi huko Umbria, ili kusaidia eneo hilo, na kutokana na ukweli uliopokonywa kutoka kwa uhalifu uliopangwa, na wakati huo huo, chaguzi hizi zina thamani muhimu sana katika kupunguza athari za mazingira za chakula .

Seti ya ikolojia kwa vijana wa Uchumi wa Francisko

Kwa maana hiyo Wanauchumi vijana  waliofika Assisi kwa ajili ya Uchumi wa Francisko pia walipewa vifaa maalum:  vifaa vya kuoshwa na vinavyoweza kutumika tena ambavyo wamesambaza hata kwa watoto. Wanatumia bidhaa zinazoweza kuharibika na kuoza. Aliendelea kueleza Bwana Lanzi kwamba kusaidia watoto kuelewa.mantiki ya mkusanyiko tofauti. Ni muhimu kila kijana akafahamu hili na anawajibika kugawanya taka kwa usahihi.Wamepatia vijana hao ili , pia kuwasaidia katika kutafakari kwao, daftari; pamoja na kutafuta mawazo.

Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022
Vijana wanauchumi wa Francisko wako Assisi 22-24 Septemba 2022

Ndugu msikilizaji wa Vatican News, baba Mtakatifu Francisko anaratajia kwenda Assisi, Jumamosi tarehe 24 Septemba kuunganika na washiriki wa Tukio la Uchumi wa Francisko, Harakati iliyoanziwa kwa msukumo wake, ambapo ni vijana 1000 waliounganika kutoka nchi 120 ulimwenguni.  Hawa ni wajasiriamali vijana na wachumi, wenye lengo la kutoa roho mpya kwa ajili ya uchumi kwa kutaka kutengeneza michakato ya ujumuishaji.

Habari 23 Septemba
23 September 2022, 16:40