Jukwaa la watawa nchini India Jukwaa la watawa nchini India 

India:Watawa wako thabiti katika imani karibu na waliokandamizwa

Jukwaa Watawa kwa ajili ya haki na amani ambao wako thabiti katika imani ya liwa karibu na waliokanadamizwa katikati ya taabu limefanyika kuanzia tarehe 22-25 Septemba 2022.Katika hitimisho wametoa tamko kuwa kama watawa kwa ajili ya kujitolea kwa haki na amani wanaelezea wasiwasi kwa kuzorota hali yao kitaifa kwa kila ngazi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuwa manabii katika Kanisa ambalo mara nyingi huharibiwa na matambiko, kubaki imara katika imani, iliyoshikamana na Kristo Yesu, katikati ya dhiki itokanayo na uchaguzi wa kusimama karibu na maskini na walioonewa ndiyo ilikuwa nia kwa washiriki wa taasisi na mashirika ya kitawa ya kike na kiume kutoka majimbo 16 nchini India, waliokusanyika pamoja tangu tarehe 22 hadi 25 Septemba  2022 huko Hyderabad katika jimbo la India la Telangana kwa ajili ya  mkutano wa kitaifa wa “Jukwaa la Kidini kwa  ajili ya Haki na Amani”.

Katika tamko lao la mwisho wa Jukwaa hilo lengo ni kukuza utambulisho wao kama watawa na kujibu ishara za nyakati, kuanzia Waraka wa Kitume wa Papa Francisko kwa watu wote waliowekwa wakfu, aliyokuwa ametoa wakati wa Mwaka wa Maisha ya Watawa mnamo tarehe  21 Novemba 2014). Ambapo Papa Francisko katika Waraka huo alikuwa amebainisha “Mwaka huu pia unatuita kuishi sasa kwa shauku. Kumbukumbu ya shukrani ya siku zilizopita inatuhimiza, kwa kusikiliza kwa makini kile Roho anachosema kwa Kanisa leo, hii ili kutekeleza kwa njia ya kina zaidi vipengele vya msingi vya maisha yetu ya kuwekwa wakfu”.

Sr. M. Nirmalini, Rais wa Kitaifa wa Baraza la Umoja wa Watawa nchini India, alikumbusha ombi la Papa kwa watawa kuamsha ulimwengu, kwa kushuhudia kwamba kuna njia nyingine ya kuwa, ya  kutenda na kuishi, na maisha ya kinabii. Sr. Nirmalini aliongeza kusema kuwa  ili kuamsha ulimwengu watawa  lazima wasikilize furaha na vilio vya ulimwengu unaozunguka na wito wa Mungu. Mahali walipo, kile wanachokiona na jinsi wanavyosikiliza, kila kitu ni muhimu. Wanapoutazama ulimwengu, hataona upendo wa ajabu , wema, uzuri na ukarimu tu, lakini pia wataona watu na dunia wakiteseka bila sababu, wakiomba jibu, na kwa maana hiyo wao wameitwa kutoa jibu. Naye kiongozi wa Muungano wa Kitaifa wa Harakati za Watu (NAPM), Meera Sanghamitra, akigusia masuala ya kijamii yanayoikumba jamii ya India, alionesha njia za kufuata, matumaini, uponyaji na maelewano, pamoja na mapambano, mshikamano na kujitolea kwa jamii ya sasa, hasa katika  muktadha wa kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kidini.

Uchambuzi wa hali ya India, uliopendekezwa na hati ya watawa  wa India kama ulivyo wakilishwa katika shirika la habari za kimisionari wanabainisha kuwa: Kama watawa kwa ajili ya kujitolea kwa haki na amani wanaelezea wasiwasi wao  kwa kuzorota kwa hali yao ya  taifa kwa kila nyanja. Viashiria vya kimataifa leo hii vinaiweka India kwenye upande wa chini. Maskini nchini India wanazidi kuwa maskini kila siku; matajiri na wenye uwezo wanaendelea kujinufaisha kwa gharama zao wenyewe na kujikusanyia mali nyingi kupita kiasi. Makabila ya Adivasi wanaibiwa ardhi zao. Wadalits na vikundi vingine vidogo bado vinanyimwa utu, usawa na haki. Dini ndogo (hasa Waislamu na Wakristo) wanalengwa kwa matamshi ya chuki na mateso, huku siasa kwa utaratibu zikiendelea kuwadharau na kuwatia pepo kwa ajenda ya migawanyiko na vurugu. Kutovumilia kunaongezeka.

Sheria zisizo za kikatiba za kupinga watu kubadilika zimechukua nafasi kubwa leo hii. Kanuni za Kazi zinaenda kinyume na haki za wafanyakazi na zinapendelea makampuni makubwa yenye faida. Hali ya kusikitisha ya wafanyakazi wahamiaji ilidhihirika wakati wa karantini mnamo Machi 2020. Wavuvi huko Kerala na sehemu zingine za nchi wanapigana dhidi ya kampuni zinazokusudia kuharibu maisha yao. Ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumekuwa na athari kubwa kwa maisha ya watu masikini.

27 September 2022, 16:05