Tafuta

Kardinali mpya wa Jimbo Kuu Katoliki Singapore Askofu Mkuu William Goh na Papa Francisko 27 Agosti 2022 Kardinali mpya wa Jimbo Kuu Katoliki Singapore Askofu Mkuu William Goh na Papa Francisko 27 Agosti 2022 

Kardinali wa kwanza Singapore ameahidi kunzisha taasisi ya utafiti wa maelewano ya kidini

Kanisa Kuu la Singapore litaanzisha kuhamasisha maelewano ya kidini kupitia Taasisi ya Utafiti.Haya yamebanishwa na Kardniali wa kwanza wa Singapore mara baada ya tukio la kuundwa kwa makardinali wapya mnamo tarehe 27 Agosti 2022.Kardinali Goh amebainisha kuwa shughuli ya mazungumzo ya kidini yanatokea shukrani kwa uvumilivu wa kusuka mahusiano ya kibinadamu na kiroho.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali wa kwanza nchini Singapore, Askofu mkuu William Goh, amethibitisha kuwa atahamasisha maelewano ya kidini barani Asia kwa kuweka nguvu ya mazungumzo kati ya dini tofauti. Mazungumzo ya kidini maana yake ni kufanya mahusiano na watu, licha ya mipaka ya kidini kwa lengo la kushirikiana na kuhamasisha amani katika jamii katika bara la Asia na ulimwenguni. Hii ni sehemu ya utume wa uinjilishaji wa Kanisa katika hali halisi ngumu kama ile ya Asia, alisisitiza.

Kardinali William Goh Seng Chye akisalimiana na marafiki na ndugu
Kardinali William Goh Seng Chye akisalimiana na marafiki na ndugu

Kardinali Goh, mmoja wa Makardinali 20 mapya waliundwa na Papa Franisko  mjini Vatican mnamo tarehe 27 Agosti  2022, ambaye kwa mji wake huko nchini Singapore ataanzisha kwa maana hiyo Taasisi ya utafiti wa kujifunza mitindo ambayo ina hamasisha  urafiki na wengine, viongozi wa kidini, na baadaye kuishirikisha kwa maaskofu wote Barani Asia. Kwa mujibu wake amesema kwamba wakati uliopita wa mataifa ya Asia mara nyingi walikuwa wanaomba Kanisa Katoliki la Singapore mashauri na mazoezi mema ili kuweza kuishi kwa namna ya kuleta matunda ya utamaduni mwingi na mazungumzo tofauti ya kidini.

Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali
Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali

Askofu Mkuu Goh amesema  kuwa shughuli ya mazungumzo ya kidini yanakuja shukrani kwa uvumilivu wa kusuka uhusiano wa mahusiano ya kibinadamu na kiroho. Na zaidi ni muhimu kusaidita taasisi hata serikali ya Singapore ambayo kwa vyovyote vile  inatamani kuhamasisha umoja, kwa kutoa msaada hata hivyo bila  kuwa shirika ambalo linahamasisha au linaongoza mchakato.Serikali ya Singapore amesema inawatazama kanisa  kama washirika kwa sababu lengo kuu kwa namna ya pekee ni mchango wa ujenzi wa jamii kuwa bora. Maaskofu kwa maana hiyo wanataka kuishi maisha ya maelewano na Singapore. Wanafanya kazi na serikali katika kujua thamani ya pamoja na serikali ambalo linawategemea.

Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali
Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali

Kardinali ameongeza kusema kuwa wao wanaturudia kusema na serikali kwa sababu mbali na hayo yote dini  haijihusishi na siasa. Askofu Mkuu alisema: “Kanisa katoliki halidharau imani nyingine na halitafuti mamlaka ya kisiasa, bali linashirikiana na kushirikishana na taasisi za kiraia,” Kuchaguliwa kwake kuwa Kardinali mwaka huu 2022 kumefika wakati ambapo jimbo Kuu  la Singapore linaadhimisha miaka 200 ya uinjilishaji.

Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali
Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali

Kwa kuelekeza kwamba  kama wabatizwa, ambao wanaweza kuwa wajenzi wa mazungumzo na amani, Kardinali amethibitisha kuwa wao kama viongozi wa Kanisa, wanahusiano wa dhati na wanaheshimiana na kusaidiana pamoja. Jwa njia hiyo wao wanawaweza si kushirikishana,  na kuaminika , lakini angalau kushirikishana thamani za ulimwenguni ambazo ni upendo, haki, amani na maelewano. Wanawaishi thamani hizi  kwa roho ya Kristo ambaye ni kisima. Singapore ni nchi ya dini ambayo asilimia 80 ya watu wake wanakiri imani pamoja na kuwa serikali ya kilei. Kwa maana hiyo hawapaswi kudharau umoja wa kidini katika chi yao na wanapaswa kuhakikisha kuwa viongozi wa dini wanabaki hivi na kuheshimiana mmoja na mwingine kwa kutoa mfano kwa waamini.

Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali
Kardinali William Goh Seng Chye akivalishwa kofia ya ukardinali

Katika ngazi binafsi, Askofu Mkuu wa Singapore amesema wanapaswa kutia moyo wakatoliki ili kujua dini za watu wengine, lakini pia mazungumzo ya kidini ni kwa ajili ya kila mmoja mwenye shauku na ukomavu katika imani yao. Haiwezekani kuzungumza na wengine ikiwa hawajuhi  imani yao binafsi. Katika roho hiyo inawezekana kuwa shuhuda wa dhati wa Kristo na watu wa imani nyingine amehitimisha. Singapore ni taifa lenye dini nyingi na makabila mengi kwa watu ambao wanakadiriwa milioni 5,7. Sehemu kubwa ya wachina ni Wabudha na sehemu kubwa ya wazalendo wa kabila la Malesi ni waislamu. Wakristo wanawakilisha karibu asilimia 15% ya watu wote, Jimbo kuu la Singapore, ambalo linafunika kisima kizima, linakaridiliwa kuwa na wakatoliki 360,000 waliogawanyika katika maparokia 32.

KARDINALI WA KWANZA NCHINI SINGAPORE
01 September 2022, 15:00