Bahrain:Ziara ya Papa inaonesha Ufalme kama mahali pa kuishi na kuvumilia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tarehe 28 Septemba 2022, ilitolewa Taarifa kutoka vyombo vya habari Vatican kwamba kwa kupokea mwaliko wa Mamlaka ya kiraia na kikanisa, Papa Francisko atatimiza ziara ya kitume katika nchi ya Ufalme wa Bahrain kuanzia tarehe 3 hadi 6 Novemba 2022 kwa kutembelea mji wa Manama na Awali katika fursa ya Jukwaa la Bahrain kwa ajili ya Mazungumzo: Mashariki na Magharibu kwa ajili ya ubinadamu wa kudumu. Kwa maana hiyo tangazo hilo linathibitisha jitihada za chaguzi ya familia ya kifalme ya Al Khalifa, nia ya kukubali msimamo wa Ufalme kuwa mahali pa mazungumzo, ukarimu wa uvumilivu na kuishi kwa amani kati ya tambulisho nyingi na jumuiya ya imani, katika ulimwengu ambao daima umezugwa na migogoro ya miibuko ya kidini na mabishano ya ustaarabu. Hii ndio picha ambayo vyombo vya kitaifa kama Al Ayyam Al Bahrain inavyoonesha zaidi mara baada ya tangazo kuhusu ziara ya kitume Papa ijayo, katika kuzungukia suala hilo hata kwa upande wa maridhiano ya wakuu wanaojulikana mahalia wa jumuiya za kikristo.
Kwa mujibu wa Padre Fayad Charbel, kuhani wa Kanisa la Moyo Mtakatifu la Manama, amebainisha kuwa ziara ya kipapa huko Bahrain itachangia kuonesha wote kuwa Bahrain ni nchi ya mazungumzo na kuishi pamoja katika ulimwengu uliojaa migogoro ya kivita. Padre Saba Haidousian, Paroko wa Jumuiya mahalia ya Kigiriki-Kiorthodox, amesisitizia umuhimu wa ziara ya kipapa kwa ajili ya Ufalme na kwa ajili ya Nchi za Mashariki zote huku akikumbusha kuwa Mfalme Hamad bin Isa Al Khalifa kwa muda sasa anafuatilia kwa makini kufanya Bahrain kuwa nafasi moja ya kuishi kwa amani na uhuru kati ya jumuiya mbali mbali za imani.
Jukwaa la Mazungumzo ya Mashariki na Maghari kwa ajili ya kuishi kibinadamu kwa manaa hiyo inawakilisha hata fursa kwa ajilia ziara ya kitume ya Papa Francisko, ambayo itajikita juu ya Bahrain na umakini wa kimataifa, kwa kuruhusu watu wote kuweza kuishi kati ya tofauti ambao inawakilishwa kwenye maisha ya Ufalme. Hata mkutano wa Papa Francisko na Mfalme Hamed, amesisitiza Hani Aziz, mchungaji wa Kanisa la Kiinjili huko Manama, kwamba itakuwa ni fursa kwa ajili ya kutuma ujumbe mkubwa kwa nchi za Mashariki ya Kati, ili iwe huru dhidi ya vita ambavyo vimewasumbua sana watu wote na kuzuia hata kufikiria wakati ujao wenye matarajio kwa wote. Maoni mengine yanasisitizia juu ya uhuru kamili ambao wakristo wa Bahrain wanaweza hatimaye kuadhimisha kweli katika lugha zao na kuhudumu sakramenti zao.
Katika nembo rasmi ya ziara ya Papa Francisko kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwenye tovuti rasmi ya baharainpapalvisit.org, “inaunganisha bendera ya Ufalme wa Bahrain na Vatican, chini kama mfano wa mikono iliyoinuliwa juu pamoja kwa Muumba, kama kutoa wito kwa ajili ya amani”. Tawi la mzeituni katikati lina maana ya tunda la amani inayotolewa na Mwenyezi Mungu. Katika nembo kwa mujibu wa maelezo wanabainisha kuwa Meneno “Papa Francisko, yameandikwa kwa rangi ya blu katika kutaka kuelezea kuwa ziara ya kipapa imekabidhiwa kwa maombezi ya Bikira Maria, “Mama Yetu wa Arabia” ambaye ni msimamizi wa Kanisa Kuu na kwamba ni zawadi ya Ufalme wa Bahrain kwa Kanisa Katoliki la nchi hiyo.
Historia ya falme ya Bahrain
Historia ya Bahrain inahusu eneo ambalo leo linaunda hakika ufalme wa Bahrain. Na Bahrain ndiyo makao ustaarabu wa Dilmun. Nchi hiyo ilipata umaarufu tangu zamani kwa kuvua lulu bora kuliko zote duniani hadi karne ya 19. Ufalme wa Bahrain ulikuwa kati ya maeneo ya kwanza kuongokea Uislamu mnamo mwaka 628 Bk.Baada ya kipindi cha utawala wa Waarabu, Bahrain ilitekwa na Wareno mnamo mwaka 1521 hadi 1602 walipofukuzwa na Shah Abbas I wa nasaba ya Safavid chini ya Dola la Uajemi. Mnamo mwaka 1783, ukoo wa Bani Utbah uliteka Bahrain kutoka kwa Nasr Al-Madhkur na tangu hapo nchi ilitaawaliwa na ukoo wa Al Khalifa, Ahmed al Fateh akiwa hakimu wa kwanza wa Bahrain. Tangu mwaka 1820 Visiwa hivyo pamoja na Qatar na Falme za Kiarabu vilikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20. Na tangu mwaka 1820 hao walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20. Falme hizo zilikuwa chini ya usimamizi wa Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.