Kazakhstani:Ziara ya Papa imeubua shauku ya imani na ujasiri katika mazungumzo.
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Nchini Kazakhstan kulikuwa tayari na heshima ya kina kwa ajili ya Kanisa Katoliki, lakini ziara ya kitume ya Papa Francisko mwezi Septemba, imeleta matokeo kwa ujumla ya kufikiriwa zaidi kuelekea wao kati ya watu mahalia. Hii labda uwepo wake umetoa ujasiri zaidi hata kwa wakatoliki wenyewe. Katika nchi ambayo wakatoliki wanaitwa zizi dogo, kama alivyo sema Papa Francisko na wakati mwingine wanaangukia katika makosa ya kubakia kutazama idadi, na kuhisi kila wakati ni wadogo karibu na kjiona wasio na maana. Kwa hiyo kukaribisha Papa Francisko katika zizi hilo dogo, kumewaimarisha imani yao na katika utume wa kila siku na ambayo sio yao bali ni kazi ya Mungu. Alisisitiza hayo Askofu Yevgeniy Zinkovskiy, askofu msaidizi wa Jimbo la Karaganda na Askofu wa kwanza mahalia nchini Kasakhstan, ambaye amekumbusha juu ya ziara ya Kitume ya hivi Karibuni ya Papa Francisko katika nchi ya Asia ya Kati aliyofanya kuanzia tarehe 13-15 Septemba 2022.
Akizungumza katika vyombo vya habari za kimisionari Fides, Askofu Msaidizi Zinkovskiy, alisema, mada ya mazungumzo ilikuwa kiini cha hotuba zake Papa Francisko, na maneno yake yatabaki kuwa kitovu cha kutazamia kwa imani ya wakatoliki wote wa Kazakhstan. Mazingira ya tamaduni nyingi ambazo wanaishi zinawapeleka kila siku kujibidisha na kufanya kazi juu ya mazungumzo lakini kuanzia na mfano wa Baba Mtakatifu mwenyewe aliowaonesha na kuwapatia ambapo wanaweza kujifungulia tena zaidi mkutano na watu ambao wanatoka katika makabila, tamaduni na dini nyingine. Wanaweza kujifunza kuishi na kupendana wao kwa wao. Mazungumzo yale ni kichipukizi ambacho wataendelea kukuza na mchakato ambao wanategemea kuongeza.
Kuwepo Papa huko jijini Astana umetoa hata fursa ya kusisisitiza juu ya Makubaliano kati ya Vatican na Jamhuri ya Kazakhstan. Hati ile kwa maelezo ya Askofu Zinkovskiy, inawakilisha zawadi kubwa ambavyo itasaidia utume wa Kanisa katika nchi hiyo. Mkataba kama kama ilivyoelezwa na Vatica kiukweli utatoa nafasi kubwa ya kutenda kwa ibara ya 2 ya makubaliano na sehemu zote mbili ya 1998, kurahisisha kukubaliwa kwa ziara na ruhusa za kukaa binafsi watu wa Kanisa na kidini wanaokuwa kutoka nchi za nje na shughuli katika utunzaji wa kichungaji wa waamini wakatoliki nchini Kazakhstan”.
Mbegu hizi zote zilizopandwa na ziara ya Papa zikipaliliwa vizuri na kutunzwa zitaweza kuchipua vizuri, kukua na kutoa matunda, kwa kile ambacho Mungu atapenda katika jumuiya yao ambayo daima ni watu walioko katika mchakato wa safari katika ulimwengu katika kumfuasa Kristo. Alihitimisha. Ikimbukwe kuwa nchini Kazakhstan ina majimbo 4 katoliki yenye jumla ya Parokia 70 tu. Mapadre walipo katika taifa ni 91, miongoni mwake mapadre wa majimbo 61 na watawa ni 30. Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya nchi za nje nchini Kazakhistani zaidi ya milioni 17 ya wakazi, karibia asilimia 26% inaundwa na wakristo, na ni asilimia 1% tu ndiyo ya imani katoliki.