Tafuta

Picha ya Bikiria Maria wa Rosari huko Pompei, Italia. Picha ya Bikiria Maria wa Rosari huko Pompei, Italia. 

Italia:Kutafakari Yesu na Macho ya Maria!

Kutafakari Yesu na macho ya Maria” ndio mada iliyoongoza Kongamano katika madhabau ya Bikira Maria wa Pompei katika kumbu kumbu ya miaka 20 ya waraka wa ‘Rosarium Virginis Mariae’ wa Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo 2002 na miaka 150 ya kufika kwa wakili Bartolo Longo katika mji huo.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Jumatano tarehe 19 Oktoba 2022 Askofu Mkuu Tommaso Caputo, Msimamizi wa Kitume wa Madhabahu ya Bikira Maria wa Rozari Takatifu  huko  Pompei  alitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano  kuhusu  Mwaka wa Longhian uliofunguliwa mnamo tarehe Mosi Oktoba  2022 katika  mji wa Maria kwa lengo la kukumbuka kuwasili  kwa Mwenyeheri Bartolo Longo huko Pompei. Ni tukio ambalo lilitokea  mnamo mwezi wa Rosari  mwaka 1872 na vile vile  miaka 20 ya Barua ya Kitume iitwayo Rosarium Virginis Mariae , kwa ajili ya Rozari Takatifu ya Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 16  Oktoba 2002, wakati Mtakatifu Yohane Paulo II alipotia saini, katika fursa ya  katekesi  katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican. Kwa kuongozwa na mada  “Kutafakari Yesu na macho ya Maria”, skofu Mkuu Caputo  alielezea juu ya Mwanzilishi wa Madhabahu hiyo Bartolo Longo alivyo kuja kugeuka kuwa chombo cha mpango wa Mungu kwa njia ya Mama Maria.  Askofu Mkuu alisema Miaka mia moja na hamsini iliyopita wakili kijana alifika, kwa sababu za kitaaluma, katika bonde ambalo yeye mwenyewe alifafanua kama 'ukiwa', lililokaliwa na wakulima mia kadhaa waliolazimishwa kuishi na malaria na wizi kama majambazi.  

Oktoba 1872 Bartolo Longo alisikia msukumo wa ndani

Mnamo Oktoba 1872, Bartolo Longo alisikiliza msukumo wa ndani, ambao alisema hawataacha kuurudia kusema “'Ikiwa unatafuta wokovu, sambaza Rozari. Ni ahadi ya Maria. Yeyote anayeeneza Rozari yuko salama! Yeye, akiongozwa na Roho Mtakatifu, aliyatia ndani maneno hayo na kugundua mapenzi ya Mungu kwake. Hakuwahi kuondoka Pompei. Tangu wakati huo na katika maisha yake marefu, kwa uaminifu daima hadi uvuvio wa awali, akawa chombo cha mpango wa Mungu, aliyepatanishwa na Maria; mpango ambao kila siku unashangaza zaidi na unastahili mshangao. Alisisitiza. Na kwa kuongeza aliuliza je mngao huko hukoje? Bila Rozari kusingekuwa na kuwasili Pompei kwani mnamo  tarehe 13 Novemba 1875, sanamu ambayo watu wote wanaiheshimu  na isingekuwa na hatua nyingine muhimu, kama vile mwanzo wa ujenzi wa madhabahu, mnamo tarehe 8 Mei  1876 au uzinduzi wa kwanza wa kazi nyingi za upendp wa  kituo cha watoto yatima wa kike  mnamo  tarehe 8 Mei 1887.   

Bila Rosari jiji la Pompei lisingetokea

Bila Rozari, Jiji jipya la Pompei, lililoanzishwa kama Manispaa mnamo 1928, lisingetokea. Baba Mtakatifu Benedikto XVI pia alimzungumzia Longo ambaye tarehe 19 Oktoba 2008, alikuwa na hija huko Pompei. Askofu Mkuu Caputo alikumbuka maneno haya: Longo akiongozwa na upendo, aliweza kubuni mji mpya, ambao ulizuka karibu na  mahali patakatifu pa Maria, karibu kama nuru ya  mwanga wa imani na matumaini. Ngome ya Maria na ya upendo, isiyotengwa na ulimwengu, si, kama wasemavyo, 'kanisa kuu jangwani', lakini iliyoingizwa katika eneo la Bonde hili ili kuikomboa na kuitangaza [...] Je ni nani angeweza kufikiri kwamba hapa, kando ya mabaki ya kale ya  Pompei  pangetokea madhabahu Takatifu ya Maria na yenye umuhimu wa kimataifa? Na kazi nyingi za kijamii zinazolenga kutafsiri Injili katika huduma madhubuti kwa watu walio katika shida zaidi? Ambapo Mungu hufika, na jangwa huchanua!”

 Karram: Tusali Rosari kwa kufikiria hata vita vingine

Mwenyekiti wa Harakati ya Wafokolari Margaret Karram, katika hotuba yake tarehe 19 Oktoba kwenye Kongamano la mada “Kutafakari Yesu kwa Macho ya Maria  katika Madhabahu ya Bikira Maria huko  Pompei  Italia alisema kuwa, kilichomshangaza zaidi siku hiyo kutoka katika Barua ya Kitume ya Rosarium Virginis Mariae’, miaka 20 tangu kuchapishwa kwake, ni wito maalumu  ambao hadi sasa unahitajika sana kwa namna ya pekee ya kusali Rosari ili kuomba kwa Bikira zawadi ya amani. Haiwezekani kuwa kinyume katika miezi huu ambayo tunaishi moja kwa moja na uchungu wa mgogoro kati ya Urussi na Ukraine, katika milango ya bara la Ulaya , lakini si tu hilo kwa kufikiria hata Nchi nyingine ambao zinasimuliwa au hapana kwenye vyombo vya habari kama vile Yemen, Siria, Libia, Afghanistan na nchi nyingine.

Kwa mujibu wa Bi  Karram  aliwaeleza jinsi ambavyo hivi karibuni alisikia wito wa nguvu wa kutafuta sana uhusiano na Mungu kutoa muda sana kutafakari na  sala.  “Nilitambua kwamba siku zangu ziliwekwa alama na ajenda iliyojaa mipango, nikilazimika kuchagua kile ambacho ningekipa kipaumbele, nilihisi ndani ya wito kwa muhimu, kukita mizizi katika Mungu: Yule ambaye nimemchagua kuishi. Ni kwa njia hiyo tu, nilikuwa na hakika, ningeweza kutoa mchango wangu kuelekeza maisha yangu na yale ya Jumuiya ya Waasisi zaidi na zaidi kuelekea Injili, kiini cha  kila kitu. Kwa hivyo ndipo lilizaliwa hitaji la kupendekeza kwa Jumuiya nzima ya Wafocolari kwa miezi michache ijayo, ya kuimarisha maisha ya ndani na sala, ili watu binafsi na jumuiya nzima waweze kuigundua tena na kuiishi kama mazungumzo ya kweli na mazungumzo ya dhati na Mungu.

16 Oktoba 2002 Mtakati Yohane Paulo II alitia saini Waraka wa Rosarium Viriginis Mariae

Tarehe 16 Oktoba 2002, Mtakatifu Yohane Paulo II alitia saini Waraka wa Kitume “Rosarium Virginis Mariae wakati katekesi yake katika  Uwanja wa Mtakatifu Petro. Chiara Lubich pia alikuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambaye katika  barua yake, Baba Mtakatifu aliikabidhi Rozari Takatifu ili Jumuiya hiyo iweze kuitangaza duniani. Kwa maana hiyo alieleza mwenyekiti wa Wafokalari kwamba anakumbuka vizuri mnamo 2002, wakati Mtakatifu Yohane Paulo II alipomwandikia Chiara pia kuwakabidhi Wafocolari jukumu la kushirikiana katika kutangaza Rozari Takatifu, hasa katika mwaka huo wa kukweka wakfu. Je ni kwa sababu gani , kwa kujibu alisema Labda ni  kwa sababu Harakati ya Wafokolari  inaitwa rasmi 'Kazi ya Maria na Chiara daima alifikiri kwamba ni yeye aliyahamasisha hali ya kiroho ya Umoja  ambao husaidia kutimiza agano la Yesu, “Ili wote wawe kitu kimoja'”(Yn 17:21). Bi  Karram alikumbuka jinsi  ambavyo Bikira alivyokuwa kama nyuzi ya dhahabu ya maisha yake  lakini ibada inaweza tu kuonekana katika hatua halisi na hasa, katika kusaidia wale wanaoomba msaada. Yeye binafsi alishuhudia jinsi anavyojitahidi  sana na angependa kukupitishia wao pia   kwamba Maria leo ​​ hii kuliko wakati mwingine wowote anamwalika, anawaalika kuweza kumwiga. Je ni kwa njia gani? Alielekeza kwamba ni kwa kukusanya kila chozi, kila kilio…, kila hali ya kukata tamaa ambayo tunakutana nayo; anatuita tuihusishe ili kutoa upendo, kuondokana na mioyo ya chuki, kama alivyosema baba Mtakatifu Francisko na  kuwa mbegu za matumaini kwa ulimwengu kila mahali.

Askofu Mkuu Sorrentino: Tunahitaji bado wokovu

Na kwa upande wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Assisi-Nocera Umbra-Gualdo Tadino na wa  Foligno alithibitishwa kuwa ubinadamu ni kazi nzuri kutoka mikononi mwa Mungu na ambao ulisafishwa kutoka katika dhambi. Katika Rosari kuna wokovu. Katika hotuba yake ambayo ilisindikizwa na safari ya Barua ya Kitume ya  “Rosarium Virginis Mariae” ya Mtakatifu Yohane Paulo II  aliweza kumulika baadhi ya mantiki kadhaa. Kwa mujibu wake alisema kwamba  katika wakati huu unaangaziwa na  vita vya Ukraine,wameelewa kwamba ubinadamu wetu ulitoka katik uzuri kwenye mikono ya Mungu na uliharibiwa na dhambi ya asili na sehemu ya kwanza ya vurugu kati ya Kaini na Abeli. Ilikuwa ni mfululizo usio na mwisho wa matukio ya vurugu. Na bado ni leo hii yanaendelea. Kwa maana hiyo tunahitaji wokovu, ambao kwa Kiebrania ni Yehoshu’a, kwetu sisi ni Yesu”.

'Yeyote aenezaye Rosari ameokoka'

Katika sentensi ya Maria kwa Bartolo Longo, 'Yeyote anayeeneza Rozari ameokoka!' Mama yetu anamkabidhi Mungu ili amrudishe kwa ubinadamu. (…). Katika 'Rozari ya Bikira Maria (Rosarium Virginis Mariae', Mtakatifu Yohane Paulo II, kama Papa wa Rozari, Leo XIII, aliianzisha  Rozari kwa utume wa aina  mbili. Kwa ajili ya familia na amani. Familia haimaanishi kama kifungo cha ndoa tu, lakini vilevile kama muungano wa jumla wa ulimwengu.  Na amani kwa ujumla ya kijamii na kwa ulimwengu wote. Askofu Mkuu Sorrentino akiendelea na hotuba yake alisema Mtakatifu Yohane Paulo II alitaka kusaidia Kanisa kufanya mageuzi kutoka katika ibada hadi kutafakari, kutoka katika  kukutana na Mama hadi kufikia ‘shule’ ya Mama”. Kwa njia hiyo  ni lazima, tunaposali Rozari, kuwa kama Maria, kumwiga: “Rozari inakuwa mfanano, si ibada tu, bali ni safari tunayoifanya na Maria, moyo wa Maria, macho yake, ambayo kwayo ni lazima tumtazame Yesu. Kitendo hicho kinatokana na Rozari, kwani uzoefu na kazi ya Mwenyeheri Bartolo Longo inaonesha wazi kwamba yeye ni nabii mkuu kwa sababu kazi za upendo ni kama  upande wa pili wa sarafu ya medali na hivyo maneno ya Rosario yanageuka kuwa vitendo alihitimisha Askofu Mkuu Sorrentino.

MIAKA 20 YA WARAKA WA ROSARIUM VIRGINIS MARIAE
22 October 2022, 10:11