Siku ya Kimisionari duniani 2022:kuzuia wahamiaji ni kuzuia ndugu katika imani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika fursa ya kuelekea kwenye kilele cha Siku ya Kimisionari duniani, itakayofanyika Dominika tarehe 23 Oktoba 2022, kwa kuadhimishwa na maparokia yote duniani, Askofu Mkuu Gian Carlo Perego, wa Jimbo Kuu katoliki la Ferrara Italia na Rais wa Mfuko wa Wahamiaji (Migrantes) wa Baraza la Maaskofu Italia amethibitisha kuwa: “Kuzuia kukaribisha wahamiaji maana yake ni kuzuia kaka na dada zetu hata katika imani”. Hata hivyo katika ujumbe wa tukio la Siku hiyo kwa mwaka 2022, Askofu Mkuu Perego amesisitiza kwamba Baba Mtakatifu Francisko alielezea kwa dhati juu ya nafasi ya wahamiaji kwa namna ya pekee kwamba wakimbizi ni kama mashuhuda wa imani na umuhimu wa kukaribishwa kwa nchi wanapofikia.
Katika maelezo ya kifungu hicho kwa sababu ya mateso ya kidini, na hali za vita, vurugu, alisema wakristo wengi wanalazimika kukimbia katika ardhi zao kuelekea nchi nyingine. Kwa maana hiyo kuna furaha kubwa ya kaka na dada hao ambao hawajifungii katika mateso, bali wanashuhudia Kristo na upendo wa Mungu kwa Nchi ambazo zinawakarimu. Kwa ufafanuzi alisema katika hilo alikuwa anashauri Mtakatifu Paulo VI kwa kuwafikiria uwajibikaji ambao unasubiri wahamiaji katika Nchi ambazo zinawapokea (Evangelii nuntiandi, 21). Kiukweli, kwa kufanya uzoefu kama uwepo wa waamini wa mataifa mengi yanatajirisha sura za parokia na kuzifanya kuwa za ulimwengu na zaidi kuwa katoliki. Matokeo yake, utunzaji wa kichungaji wa wahamiaji ni shughuli za kimisionari ambazo hazitakiwi kudharauliwa na ambazo zinaweza kusaidia hata waamini mahalia wanapofikia kugundua furaha ya imani ya kikristo waliyoipokea.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Perego amesema hata nchini Italia, wahamiaji wanatoka karibu nchi 190 na wakimbizi kutoka karibu nchi 60. Kupitia historia zao maisha yao ambayo yanazungumza, na kwa kutumia tena maneno ya Baba Mtakatifu, alisema, wanatambuliwa hata shida na mateso kwa ajili ya imani yao zaidi ya vita, mabadiliko ya tabianchi, na umaskini. Kwa maana hiyo wahamiaji na wakimbizi ni sura na historia za matumaini ambazo zinamwilisha hata maisha ya kikristo ya jumuiya zao, ambapo karibu ni wakatoliki wahamiaji 900.000 nchini Italia, kwa kuongezea idadi ya Wakristo mwaka huu na ambao kiukweli wanasaidia kugunda furaha ya imani na kutoa msukumo na mwamko wa kutembea pamoja.