Loredana Mantello,Papa anahamasisha maelewano
Na Angella Rwezaula, - Vtican.
Katika mahojiano na Mwandishi wa Habari wa Vatican News, Devin Watkins na Bi Loredana Mantello, mpiga picha wa Kiitaliano ambaye amekuwa akiishi Bahrein kwa miaka kumi na minane, alishirikisha mawazo yake kuhusu maana ya ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini humo. Licha ya kuwa mgeni katika mchi hiyo Bi. Mantello alisema kwamba ziara hiyo huko Bahrein anaiona kama nyumbani kwake yake, na kwakmba anajisikia kukaribishwa sana nchini humo. Mapenzi yake kwa nchi ya Bahrein yanaoneshwa kila wakati. Ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya Papa Francisko nchini, humo Bi Mantello alibainisha kwamba ni ya hisia kubwa sana kwake na kwa jamii nzima.
Ziara hiyo inadhihirisha jinsi nchi ilivyo wazi kwa dini zote, huku akisisitiza na mchango wa mfalme huyo kwa kutoa ardhi ya kujenga Kanisa Kuu la katoliki la Mama Yetu wa Arabia alibainisha Bi Mantello. Kanisa na msikiti katika Manama, ambao ni mji mkuu, alisema kwake ni kuwa karibu sana kimwili, kwani anapokuwa anakwenda kanisani, anauona hata msikiti na kuwa na hisia ya suala la wote ni ndugu.
Papa Francisko yuko nchini Bahrein tangu alhamisi tarehe 3 hadi 6 Novemba. Hii ni ziara yake ya Kitume ya 39 kuwa nje ya nchi na nchi ya 58 kutembelea akiwa kama Papa. Ziara hiyo inaongozwa na kauli mbiu ya kukutana na kutia moyo kwa Wakatoliki katika eneo hilo. Papa Francisko kwa maana hiyo alipofika alikaribishwa na kutoa hotuba na wakati huo huo Ijumaa tarehe 4 Novemba 2022 ameudhuria sherehe za kufunga Kongamano la kwanza kabisa la Bahrain Forum for Dialogue: East and West for Human Coexistence, Yaani Kongamano la Bahrein kwa ajili ya Mazungumzo, Mashariki na Magharibi kwa kuishi pamoja, ambalo limeshuhudia takriban viongozi 200 wa madhehebu mbalimbali waliokusanyika ili kumasisha na kukuza udugu. Baba Mtakatifu Francisko ataendelea kuwa huko ili kuimarisha Imani kwa watu wa Mungu ambapo atarudi Roma mnamo Dominika tarehe 6 Novemba 2022.