Ivory Coast:Uchimbaji madini wa siri na unyakuzi wa ardhi unatishia idadi ya watu
Na Angella Rwezaula, – Vatican.
Kama ilivyo nchini Ghana, kwenye taarifa yao ya tarehe 16 Novemba 2022 uchimbaji haramu wa dhahabu pia ni tatizo nchini Ivory Coast ambalo linahatarisha afya ya wakazi na kuharibu mazingira. Kwa maana hiyo Maaskofu nchini Ivory Coast wanatoa mwaliko kwa serikali kuimarisha mapambano dhidi ya unyonyaji wa dhahabu wa kinyemela. Wito huo humo kwenye ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa Ivory Coast (Cecci) katika Siku ya 26 ya Kitaifa ya Amani, iliyoadhimishwa tarehe 15 Novemba 2022. Katika ujumbe uliowafikia Shirika la habari za Kimisionari Fides, maaskofu wanakumbusha kuwa shughuli haramu ya uchimbaji madini, imeenea kwa kasi nchini Ivory Coast katika miaka ya hivi karibuni na inasababisha kuzorota kwa hali mbaya ya maisha kwa ujumla.
Uchimbaji wa dhahabu usiojali na uharibifu wa mazingira
Kukimbilia kwa wachunguzi wa madini ya manjano sio bila athari katika maeneo wanayokaa, na kusababisha shida kubwa za kiafya, kwani athari za utumiaji wa zebaki ni hatari kwa idadi kubwa ya watu ambayo huwekwa wazi kila wakati. Aidha Maaskofu wamebainisha kwamba uharibifu wa misitu na mazao, uchafuzi wa maji chini ya ardhi ni uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na shughuli hizo. Uchimbaji dhahabu usiojali, sio tu kwamba husababisha uharibifu wa mazingira, lakini pia umesababisha mapigano makali na vyombo vya kutekeleza sheria vinavyojaribu kuzuia shughuli hizi haramu. Kwa mfano, huko Kokumbo, tarehe 13 Oktoba mwaka huu, kulikuwa na mapigano ambayo yalisababisha vifo vya watu 5 na majeruhi 22, ikiwa ni pamoja na vikosi vya ulinzzi 6 na mawakala 4 wa ulinzi wa misitu.
Homa ya dhahabu na vijana kutelekeza shule kwa kutafuta fedha ya haraka
Matokeo mengine yenye athari mbaya na kubwa ya kijamii ni homa ya dhahabu ambayo inashikia sana kwa watu wa Ivory Coast (lakini pia kuna watafiti wengi kutoka mataifa jirani na hata kutoka China), ni kutelekezwa shule kwa upande wa vijana, ambao wanavutiwa na ahadi ya kupata faida ya papo hapo. Huko Bengassou, mashariki ya kati ya nchi, zaidi ya wanafunzi elfu moja wameacha masomo yao kutafuta utajiri katika mgodi haramu wa Bocanda, kulingana na kile kinachoibuka kutokana na kulinganisha kwa wanafunzi walioandikishwa mwaka 2021 hadi 2022. Na hiyo inaongeza pia biashara haramu ya watoto na vijana ili waajiriwe katika migodi haramu.
Wakulima lazima wanufaike na ulinzi wa nguvu ya umma
Tatizo jingine lililobainishwa na Maaskofu nchini Ivory Coast ni lile la unyakuzi wa ardhi (Land Grabbing):uliofafanuliwa kama tishio jingine kwa ajili ya maendeleo na usalama wa chakula nchini humo. Kwa maana huyo maaskofu wamebainisha kwamba ununuzi mkubwa wa ardhi ya kilimo unaofanywa na baadhi ya mataifa ya kigeni ni changamoto inayohusu kila mtu na hasa serikali. Kitendo hicho, ambacho kinapendelea mazao ya kukodishwa, kinashutumiwa kama aina mpya ya ukoloni wa kilimo na mashirika mbali mbali yasiyo ya kiselikali NGOs na idadi fulani ya mashirika ya wakulima, Maaskofu wanasisitiza. Kwa maana hiyo wamsema kwamba wao wanakabiliwa na mtindo huo wa uwekezaji wa kigeni, hivyo wanakaribisha serikali zao kuchukua hatua ya upande wa wakulima kwa kusema kwamba wao pia ni waundaji wa mali na, kwa hivyo, lazima wanufaike na ulinzi wa nguvu ya umma.