Ujumbe wa CEI wa Siku ya 45 ya Maisha 2023:tuukatae utamaduni wa kifo unaokuzwa na itikadi za uchumi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya 45 ya Kitaifa ya Maisha kwa mwaka 2023, nchini Italia imefafanulia kwa mada kutoka katika kifungu cha kibiblia kisemacho kuwa, Kwa sababu Mungu hakuifanya mauti, wala haufurahi upotevu wa walio hai. Maana aliviumba vitu vyote vipate kuwepo na vizazi vya ulimwengu ni vyenye kuleta wokovu na hamna ndani ya hivyo sumu ya kungamiza(Hekima 1:13-14). Katika ujumbe uliotayarishwa na Baraza la Kudumu la Maaskofu wa Italia {CEI} wanasisitiza kwamba, katika wakati wetu, wakati maisha yanakuwa magumu na yenye kuwa na mahitaji, wakati inaonekana kwamba changamoto haziwezi kushindwa na mzigo hauwezi kubebeka, mara nyingi zaidi katika kufikia hata suluhisho la kushangaza la kifo ni vema kueneza utamaduni wa maisha dhidi ya kifo.
Nyuma ya suluhisho hilo inawezekana kutambua kilichopo hasa masilahi ya kiuchumi na itikadi ambazo zinajidhihirisha kana kwamba ni za busara na huruma, wakati kumbe sio muafaka kabisa. Na hii inatokana zaidi na mtu anaposhindwa kumlea mtoto, au hamkutaka, wakati anajua kuwa atazaliwa mlemavu au anaamini kuwa atamwekea vizingiti na mipaka ya kumnyima awe huru au kuweka maisha yake hatarini kama majukumu na sadaka... kwa maana hiyo suluhishi mara nyingi ni kufikia kutoa mimba. Na bado hati hiyo ya Maaskofu inaendelea kuorodhesha sababu nyingi ambazo zinasababisha kutokubali maisha kwamba mwingine anaposhindwa kustahimili ugonjwa, anapoachwa peke yake, anapopoteza tumaini, wakati ambapo huduma ya matibabu haipo, anashindwa kustahimili kuona mpendwa wake anateseka na hivyo njia ya kuweza kutoka inaweza kujumuisha ile ya euthanasia au kusaidiwa kujiua. Wakati wa kukarimu na kuunganisha wale wanaokimbia vita au umaskini kunahusisha matatizo ya kiuchumi, kiutamaduni na kijamii, na watu wanaopendelea kuachwa kwenye hatima yao, na kuwahukumu kwa kifo kisicho haki. Hivyo, hatua kwa hatua, utamaduni wa kifo unazidi kuenea.
Katika ujumbe wa Maaskofu katika fursa hiyo ya 45 ya Siku ya Maisha, unasisitiza zaidi kwamba Bwana aliyesulubiwa na kufufuka, lakini pia ni sababu sahiki, ambayo anatuonesha njia tofauti kwamba ni kutoa na sio kifo bali uzima. Yeye anatuonesha jinsi inavyowezekana kufahamu maana na thamani yake hata tunapoiona kama dhaifu, ya kutishiwa na ya kuchosha. Inatusaidia kukaribisha hata kwa ugumu wake mkubwa wa ugonjwa huo na ujio wa polepole wa kifo,na wakati huo huo kufungua siri ya asili na mwisho. Inatufundisha kushiriki nyakati zote ngumu za mateso, magonjwa mabaya, ya mimba ambayo inaweza kutuweka katika mipango isiyosawazika na kukosa msimamo. Katika ujumbe huo wa Baraza la Maaskofu Italia unabainisha pia kwamba ni lazima kujiuliza ikiwa jaribio la kutatua matatizo ya kuwaondoa watu lina ufanisi kweli. Je, tuna uhakika kwamba utoaji wa mimba kwa hiari hunaondoa jeraha kubwa linalotokea katika roho za watu wengi ambao wamefanya hivyo? Je, tuna uhakika kwamba kujiua kwa kusaidiwa au euthanasia inaheshimu kikamilifu uhuru wa wale wanaochagua na mara nyingi wamechoshwa na ukosefu wa utunzaji na uhusiano, na kuonesha upendo wa kweli na wa kuwajibika kwa wale wanaowasindikiza katika kufa? Je, tuna uhakika kwamba kufungwa kwa wahamiaji na wakimbizi na kutojali sababu zinazowahamisha ni mkakati madhubuti na wa heshima wa kudhibiti kile ambacho si dharura tu?
Kwa njia hiyo kuchagua kifo kama suluhisho huleta swali zito la kimaadili, kwani linatilia mashaka thamani ya maisha na ya mwanadamu. Imani msingi katika maisha na wema wake, kwa waamini waliokita mizizi katika imani ambayo hutusukuma kuona uwezekano na maadili katika kila hali ya kuishi, inabadilishwa na kiburi cha kuhukumu ikiwa na wakati gani maisha, hata kama ya mtu mwenyewe anastahili kuishi, ikichukua haki ya kukomesha. Siku ya Maisha Kitaifa ipyaishe kwa wafuasi wa kikatoliki katika Injili ya uzima, jitihada za kufichua utamaduni wa kifo, uwezo wa kukuza, na kuunga mkono hatua madhubuti katika kulinda maisha, na ili waweze kujikita zaidi kuhamasisha nguvu na rasilimali nyingi zaidi, Ujumbe huo muhimu kwa ajili ya Siku ya maisha unahitimishwa.