Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona limehitimishwa
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Toleo la XII la Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona limehitimishwa ambalo liliongozwana kauli mbiu: Kujenga imani. Kwa kujikita katika upendo mkuu wa kukutana kuanzia Alhamisi tarehe 24 hadi 27 Novemba 2022. Tamasha hili limewaona watoa mada 100 waliokabiliana na mada mbali mbali 25 , kuanzia na suala la kazi, ulinzi wa aina mbali mbali za udhaifu, hadi suala la afya na makampuni ya kijamii. Katika mahubiri yake Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu katika misa ya hitimisho la Tamasha kwenye Kanisa Kuu la Verona alisema kuwa inahitaji kuhama katika dhana ya umimi na kufikia upamoja, yaani kuhama kutoka dhana ya ubinafsi na kufikia ile ya jumuiya kwa kutoa nafasi kuu kwa ajili ya wengine. Kardinali Grech akijikita kutazama ujumbe wa Baba Mtakatifu aliowatumia washiriki wa Tamasha hilo, alilisisitiza wito wa kuwa mafundi wa kuaminiana na kupanga katika mipango ili kuwa na ujenzi mmoja ambao kwa hakika ni kwa njia hiyo tu unaweza kweli kusisimama dhabiti katika historia.
Kardinali Grech kwa maana hiyo alisema kuwa "umakini ni kinyume cha kutojali ambayo hupimwa kupitia mwenendo wetu kwa njia ya sinodi na uundaji wa maamuzi yanayohusu maisha ya kikanisa, lakini pia maisha ya kijamii. Hiyo ni Injili inayofanyika mwili leo hii, katika yote ya leo na si katika sehemu moja tu" kwa kuongeza je ubaguzi huu unaotegemea hatua yetu ni umakini au kutojali?” Aidha Kardinali Grech alikumbuka juhudi ya utambuzi ambayo Kanisa linaitwa katika mchakato wa safari ya sinodi, kupitia uwezo huo wa kusikilizana, kwa makini na kwa dhati ambayo unatamani kwamba mhusika mkuu wa historia awe nguvu ya ubunifu ya Roho wa Mungu na sio mipango na mawazo yetu. Ni juhudi zile zile za utambuzi ambazo Papa anarejea anapowaalika wao kama wajasiriamali, wataalamu, watetezi wa ulimwengu wa kitaasisi, wa ushirikiano, wa uchumi na wa kitamaduni' ili kila mmoja katika uwanja wake anaweza kukuza utamaduni wa kukutana na kuaminiana, kwa kufuata mfano wa Padre Adriano Vincenzi ambaye, kwa shauku, alibuni na kuanza mchakato wa safari ya Tamasha hilo muhimu'. Kanisa daima linakesha na kamwe linataka pasiwepo na sintofahamu katika kuhamasisha utamaduni mmoja wa kukutana na wa kuaminiana na ni vizuri kujikabidhi kwa kwa Bwana ajaye ili safari iwe makini siku zote kwa kuwajali wengine.
Naye Askofu Domenico Pompili, wa jimbo katoliki la Verona ,Italia, alithibitisha kwamba “kuweka mada ya uaminifu katikati ya uangalizi kunamaanisha kujishawishi na ukweli kwamba katika jamii ambayo inaelekea kugawanyika, ambayo inaendelea katika vitalu vya upinzani na hivyo ni muhimu zaidi kukuza uwezo huu wa majadiliano. Inaonekana kwake kwamba wako katika hali ya kutoaminiana. Hata hivyo, aliongeza kwamba kuna safu nzima ya vipengele vinavyotufanya tuamini kwamba uaminifu huchochea tabia ya kila mmoja wetu katika maisha ya kila siku. Mafundisho jamii ni uchunguzi wa kipekee wa kuchunguza maendeleo sio tu kwa kuzingatia vigezo vya kiuchumi, lakini kwa kurejea mfululizo mzima wa viashiria, bila ambayo maendeleo, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kiuchumi, huhatarisha kuporomoka. Askofu Pompili kwa hiyo pia anafikiri kuwa mafunzo mbalimbali ya kijamii na hatua za kiuchumi vinahitaji, katika hali ya kila siku, pia kuwa na mapumziko ya kutafakari na kushiriki. Kutoka kwa askofu wa Verona pia wazo juu ya mkasa wa Ischia ambapo mlima ulipasuka na kusababisha maporomoko juu ya makazi ya wat una wengine kufariki. Kwa njia hiyo aliwakumbuka wastu na kwa sababu ni hali nyingine ambayo kwa bahati mbaya inazua swali la kujiuliza juu ya uhusiano kati ya mwanadamu na mazingira ambayo haiwezi kukadiriwa au kupunguzwa kwa kudharau.
Makumi ya watu wa kujitolea kutoka Mfuko wa Fondazione Segni Nuovi yaani wa Ishara Mpya walishiriki hata katika toleo hilo la XII ili kuweza kuonesha juhudi za Kanisa katika maisha ya kila siku ya mfuko huo huko Verona, ambao ni kiini cha toleo hilo. Kwa maana hiyo akizungumza Rais wa Mfuko huo Bwana Alberto Stizzoli alisisitiza kwamba walihisi maisha, uzoefu wa watu wengi ambao walijenga muktadha huo wa kuaminiana. Familia nyingi zilisimulia hali halisi ya kila siku. Katika Tamasha hilo zilifika hata salamu kutoka kwa Rais wa Bunge la Italia Bwana Lorenzo Fontana. kwa mujibu wake aliandika kwamba ni kusaidia kujenga utamaduni ambao unajikita juu ya kuheshimiana, juu ya majadiliana na juu ya kushirikishana. Aidha alikumbusha kuwa Papa Francisko alisema kwamba majadiliano ni katika kujenga njia moja ambayo inawezekana kutembea pamoja na inapohitajika, madaraja kuhusu kukutana na kusaidiana. Jumuiya inahitaji kugundua umuhimu wa kukutana kwa ajili ya kujenga mazungumzo na mwingine na kusaidia kushinda migawanyiko na ubinafsi.
Kwa upande wa mwanasosholojia wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mauro Magatti, alisema mkutano huo umekuwa mzuri, lakini sio rahisi katika kipindi chochote cha historia na hata leo hii. “Tunaona kwamba kuna kufungwa sana, migongano mingi, kukataa kwingi na hivyo hebu tufikirie juu ya suala la wahamiaji, bila shaka, au kufikiri juu ya suala la Ukraine. Lakini hatupaswi kuvunjika moyo kwa sababu hatupaswi kamwe kuuchukulia mkutano kuwa jambo la kawaida.” Ni hamu, kwa mwanasosholojia, ambayo inahitaji shauku yetu na kwa vyovyote vile kuhamasisha kila mara. Walakini roho ya Italia ipo mara kwa mara. Inapendeza kuona kunapokuwa na hali hizi, hata zile za majanga, kuna watu wengi wenye uwezo wa kujitolea kwa wengine na kuwajali wengine”.